Walimu wajipanga kuanzisha benki yao

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
WALIMU WAJIPANGA KUANZISHA BENKI YAO


Friday, 17 September 2010 08:14

Gedius Rwiza

WALIMU wapatao 200,000, wameamua kuanzisha benki ya kwao ili pamoja na mambo mengine, waitunmie katika kupitishia mishahara yao.

Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch, alisema jana jijini Dar es Salamu kuwa kwa sasa walimu hao wako mbioni kufunga akaunti zao katika benki nyingine, ili wawe katika nafasi nzuri ya kuendesha benki yao.


Alisema benki hiyo ya walimu, pia itasaidia walimu kuondokana na usumbufu wanaoupata katika mikopo kutoka kwenye mabenki mbalimbali nchini,.


Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CWT, benki huyo ya walimu, inatarajiwa kufunguliwa mwakani.

"Walimu wamekuwa wakisumbuka sana katika kupata mikopo katika mabenki mbalimbali hapa nchini na wanaobahatika kupata mikopo hiyo, riba ni kubwa kuliko kawaida," alisema Oluoch.

Oluoch alisema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa CWT wa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ,katika semina elekezi .

Alisema walimu wamekuwa wakipata matatizo mengi ya huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na kutozwa riba kubwa na kwamba wakati sasa umefika kwa kundi hilo kufungua benki yao.

"Tumeamua kufungua benki ya walimu nchini ili kuwawezesha walimu kuboresha maisha yao. Tunaamini kuwa kwa hatua hiyo watakuwa wanapata mikopo a bila kubembeleza,"alisema Oluoch.

Alisema mpango wa kuanzisha benki hiyo ulipitishwa rasmi naMei mwaka huu, katika mkutano mkuu wa CWT, uliofanyika mkoani Arusha.

"Tumekubaliana kwamba hisa za benki hiyo zitanunuliwa na walimu wenyewe ili kuiongezea faida benki yetu," alieleza.

Oluoch alifafanua kuwa maandalizi ya kuanzishwa kwa benki hiyo yalianza kwa kujenga majengo ya ghorofa mbili katika mikoa yote ya Tanzania Bara, majengo ambayo sasa, yatatumika kama ofisi za benki hiyo.

"Kwa sasa tumeshajenga majengo ya ghorofa mbili kila mkoa. Lengo letu ifikapo mwakani, mikoa yote Tanzania Bara itakuwa na majengo hayo. Hatuna haja ya kutafuta sehemu za kupanga kwa ajili ya shughuli zetu za kibenki,"alisema Oluoch.

Kwa mujibu wa Oluoch uendeshaji wa benki hiyo pia utatiwa nguvu na serikali.
Oluoch pia alizungumzia tatizo la walimu kunyimwa malipo ya likizo na kupandishwa madaraja kwa sababu ya kukosa risiti, jambo ambalo alisema si sahihi.

Hata hivyo aliubebesha mzigo uongozi wa chama hicho ngazi za wilaya na mkoa, kufuatilia tatizo hilo kwa karibu na kuhakikisha kuwa walimu wanapata haki zao.
"Napenda kuwafahamisha walimu wote hakuna mtu anayetakiwa kuombwa risti ya kusafiria. Ikitokea unanyimwa madai yako kwa kukosa risiti toa taarifa kwenye chama," alisema Oluoch na kuongeza:



My Take:
Kuna haja ya secta za serekali kujitegemea sasa kama:

  1. BANK OF JWTZ
  2. BANK OF POLICE
  3. BANK OF NSSF
  4. BANK OF TANZANIA WORKER-TUCTA
  5. BANK OF LUTHERAN CHURCH
  6. BANK OF CATHOLIC CHURCH
  7. BANK OF ISLAMIC
  8. BANK OF HINDUS
  9. BANK OF WAMA
  10. BANK OF YOUTH
  11. BANK OF WOMEN
  12. BANK OF LEGION
  13. BANK OF PRISON
  14. NK..NK..NK
 
Back
Top Bottom