Walimu waitaka serikali ilipe malimbikizo ya trilioni1.060/-

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimepongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuanza kulipa madeni ya walimu, lakini imekumbushia deni lake linalofikia Sh trilioni 1.060 kutokana na malimbikizo ya kuanzia mwaka wa fedha wa 2013/14 hadi Desemba mwaka jana.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ezekiah Oluoch wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madai ya walimu na upungufu wa walimu shuleni.

Oluoch alisema kuanzia mwaka wa fedha wa 2013/14 hadi Desemba mwaka jana, katika mwaka wa fedha wa 2016/17 serikali imewalipa walimu 182,882 jumla ya Sh bilioni 124.6 sawa na asilimia 10.5 ya deni linalodaiwa katika kipindi hicho.

Alisema CWT inapongeza jitihada hizo, japokuwa hazijakidhi matarajio ya walimu ya kulipwa kwa asilimia mia.

Akizungumzia deni hilo katika kipindi hicho, alisema limeendelea kukua na kufikia Sh trilioni 1.06 sawa na asilimia 89.5 ya kiasi kilichokuwa kinapaswa kulipwa ambacho hakijalipwa.

Akizungumzia mchanganuo wa madai ya walimu, Oluoch alisema mafao ya walimu wastaafu 6,044 pamoja na tozo ni Sh 556,048,000,000, madeni yasiyohusiana na mishahara zaidi ya walimu 150,000 wanadai jumla ya Sh 180,000,000,000.

Alisema madeni ya mishahara ya walimu waliopandishwa madaraja Januari hadi Machi 2016, walimu 85,945 wanadai jumla ya Sh 301,374,312,000 na kwamba deni hilo linaongezeka kila mwezi kwa kiwango cha Sh 25,114,526,000 kuanzia Januari hii hadi Juni, 2017 ambapo lisipolipwa hadi Juni, 2017 kutakuwa na ongezeko la Sh 150,687,156,000 ambayo haikuingizwa kwenye deni la hadi Desemba, 2016.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CWT alisema ni matumaini yao kuwa serikali itachukua hatua za haraka, kuwalipa walimu madeni yao na kuwaajiri walimu wote waliohitimu, badala ya kuwaacha mitaani ambapo wataajiriwa wakiwa wamesahau mbinu za ufundishaji.

“Walimu wanajua kwamba fedha zipo, kinachotakiwa ni utashi wa Rais John Magufuli. Akiamua hata leo, fedha zote za walimu zitalipwa hata wiki hii,” alisema Oluoch.

Chanzo: Habari Leo
 
tetetetete walimu kanga na sukari za ccm zikwisha tetetetete sibirieni uchaguzi 2020 mtasikilizwa sasa tuko tunajenga uwanja wa ndege na kuwakamua masikini ili BAJETI YA MWAKA 2016..2017


SWISSME
 
ni bora muwe mnanyamaza tu kuliko kila kukicha kutupigia makelele kwenye vyombo vyetu vya habari kwa porojo zenu..nyie ni watu wa seminar za elf 20 per day kwa mda wa siku 2 mnatulia..endeleeni kutulia hivyo hivyo!!!
 
Kwa kuwa serikali ilisitisha kupandisha madaraja,na stahiki nyingi za watumishi,deni ni kubwa mnooooo!!!

Hao ni waalimu tu wanadai trilioni,hujagusa wanajeshi,polisi, na kada nyingine zote,msijeshangaa watumishi tu wakawa wanadai karibu trilioni tatu kwa ujumla.
 
Waalimu mngeionea huruma serikal. Yani inaangaika kukopa trilion mbili mpaka sasa haijafanikiwa. Tanesco nayo karbia nusu trillion. Hebu vuteni subira kidogo
 
Walimu na nyie nao hizo ngojera zetu imbeni mkichoka mtalala ,CWT ina wanasiasa sio wapigania UHURU.
 
Hao viongozi wa CWT ni bure kabisa sijui akili zao wameshikiwa,
Kuna mambo mengi sana yamefanywa kwenye awamu hii lkn wamekua kimya leo ndo wanaliona hilo la malimbikizo?
1. Mkataba wa bodi ya mikopo umevunjwa wao wapo kimya.
2. Mkataba wa Ongeze la mshahara kila July mosi umevunjwa wao wapo kimya

Yaani hii inchi sijui tutafika lini
 
Back
Top Bottom