Kwenye suala la kuongezwa kwa mishahara sitaki kuwa mnafiki. Kikwete ni rais pekee katika historia ya nchi hii ambaye ameweza kuongeza mishahara ya wafanyakazi hadi kiasi cha asilimia zaidi ya 200 katika kipindi cha miaka isiyofikia kumi aliyokuwepo madarakani.
Lakini changamoto aliyonayo Kikwete ni kushindwa kusimamia uchumi imara wenye mfumko mdogo wa gharama za maisha. Kutokana na kushindwa kusimamia hilo, wafanyakazi wamejikuta kila kinachoongezeka hakitoshi kumudu hali ya maisha ya wakati husika. Na wakati mwingine kupanda kwa gharama za maisha kumekuwa ni kukubwa zaidi ukilinganisha na mishahara inayoongezwa.
Changamoto nyingine ambayo ameshindwa Kikwete kuikabili ni uwiano wa mishahara kati ya kada moja na nyingine. Tutorial assistant wa chuo Kikuu ambaye ana degree moja. Analipwa mshahara milioni moja na kidogo, wakati mwalimu wa secondary ambaye na yeye ana degree moja analipwa mshahara laki nne na kidogo kama siyo tano. Hapa uwiano upo wapi, ilihali wote wana degree moja na ni wafanyakazi wa serikali? Basi na mwalimu wa sekondary alipwe angalau laki tisa au milioni moja amkaribie kidogo huyo tutorial assistant?
Mwalimu wa secondary mwenye masters analipwa around laki nane, wakati wafanyakazi wa kada zingine wanalipwa hadi milioni moja na laki nane. Tofauti ya milioni moja nzima, ilihali wote ni waajiriwa wa serikali. Hapa haki ipo wapi? ukizingatia wote wana qualifications zinazofanana?
Na la mwisho ni kwamba mazingira ya kazi ya mwalimu ni magumu na yasiyo na nafasi ya kumruhusu mwalimu kujikwamua kimaisha. Anachokipata mwalimu ni kile kinachoitwa hand to mouth. Hawezi kujenga wala kusomesha mtoto wake kwenye angalau shule ya private. Wakati wafanyakazi wengine wa serikali wakilipwa mishahara mikubwa sana, na marupurupu kibao. Safari za kila kuchapo. Je mwalimu ana marupurupu gani? Hata hayo malimbikizo tu kuyapata ni shida.
Halafu angalia treatment anazozipata kutoka kwa maafisa elimu na waratibu kata. Yaani ni shida tupu. Mwalimu anadharaulika kwa kweli siyo uongo. Ile heshima aliyokuwa nayo mwalimu wakati wa Nyerere imekwisha kabisa. Najiuliza kwanini wakati wa Nyerere kulikuwa na usawa kati ya wafanyakazi wa serikali, halafu leo kunakuwa na gap kubwa sana kati ya wafanyakazi wa serikali wenye elimu sawasawa?