Walimu wabobezi O level masomo ya science Dsm

mwitasa

Senior Member
Dec 28, 2013
199
476
Nina vijana wangu mwezi ujao wanamaliza mtihani wao wa darasa la saba. wakimaliza tu mwezi wa 10 nataka waanze kusoma tuition mkoa wa Dsm kwenye masomo ya science ya form one ambayo ni mathematics, physics, chemistry na biology.

Lengo kufikia January wanapoenda kuanza kidato cha kwanza angalau wawe wamemaliza topics za masomo tajwa.

Mwenye taarifa ya kituo chenye walimu wabobezi kufundisha tuition masomo tajwa kilichopo Dsm anijuze. Ikiwezekana hata jina la mwalimu katika kila somo tajwa hapo juu.
 
Mkuu wakifaulu
Nipe kazi ya kuwatafutia shule za boarding za serekali zenye hostel huku mkoani moshi na kilimanjaro kwa ujumla

Ili wasome kwa raha mustarehe

Ada ni 500000-650000 kwa mwaka
Call
0764616353
 
  • Kwa mtindo huu watoto hawaeezi kuwa wabunifu wala kumudu maisha ya kawaida.
  • Kuanzia darasa la tano mtoto ananyweshwa dozi ya kufa mtu ili afaulu shule za vipaji.
  • Mwanzoni wa November waanza kumezeshwa materials za sek ili ticha wa twisheni asionekane hafundishi.
  • Akianza sec mwendo ni uleule - hakuna likizo wala wikiendi - mtoto yupo bize kumaliza home work za kutafuta thamani ya X.
  • Amechakazwa na kanuni mbalimbali za kutafuta thamani ya X, akihitimu chuo anakosa kazi, kisha anapewa maneno ya fedheha - JIAJIRI.
  • Elimu nje ya darasa inanisaidia sana kupambana na uhalisia wa maisha.
  • N B: Sina nia mbaya na mleta thread.
 
Waweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani mkuu japo si mara zote. Wapo watoto wanaomezeshwa hizo x kuanzia primary hadi A level wakamaliza chuo na kujiajiri na kuwa wabunifu wa kutisha.

Pia ni kweli kabisa kuwa wapo vijana wengi tu wanao achiwa muda wa kutosha kipindi cha likizo wakiwa primary hadi A level ila wakabakia kuwa wabunifu kwenye kuvuta bangi, kucheza Kamari, vibaka wasiyoweza kujiajiri hata kuuza karanga.

Hivyo ubunifu wa mtoto katika maisha nje ya elimu ya darasani inategemea kichwa cha mtoto husika
 
Back
Top Bottom