Walimu wa sasa ni wavivu na walalamikaji tu!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,076
29,631
Najua itaudhi wengi lakini ukweli lazima usemwe.

Nachelea kusema kuwa walimu kwa maana ya walimu wa shule za sekondari na msingi wa miaka hii ni wavivu,masharobaro na wanaotumia muda kulalamika badala ya kufanya kazi yenye tija.

Walimu wa leo wana mchango mkubwa katika kukwamisha ufaulu wa wanafunzi kwani ni wavivu,machekibobu na wenye hulka ya ulalamishi tofauti kabisa na enzi za Mwalimu Magufuli.

Kwa kiasi kikubwa kwa miaka takribani kumi ya Kikwete tumeshuhudia uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu hasa hasa kwenye eneo la rasilimali watu...tumeshuhudia madeni ya walimu yakilipwa huku yale ya watumishi wengine kama vile afya,mahakama,kilimo yakiwekwa pembeni.

Leo hii ukisikia madeni ya walimu basi yatakuwa ni ya mwezi wa desemba 2015 au januari 2016...lakini madeni ya kada nyingine ni kuanzia 2010 na pengine nyuma ya hapo lakini hajalipwa.

Katika sekta iliyoajiri kuliko zote kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ni sekta ya elimu...pengine ndio maana serikali ikajikuta inazoa makanjanja,machekbob na wavivu kuja kutufundishia wajukuu zetu na matokeo yake tunayaona kwenye ufaulu.

Ifike mahali walimu muwe wazalendo kama wafanyakazi wengine wa umma wanaolitumikia taifa bila kulalamika pamoja na kwamba wana madai makubwa ya stahili zao.

leo hii mwalimu akiajiriwa linatumwa fungu maalum la subsistance allowance lakini daktari akiajiriwa atasubiri neema za OC ...

Nashauri kama kuna Mwalimu anaona ananyanyasika sana huko serikalini aache kazi na sio kutujazia malalamiko as if hakuna watanzania wengine wenye matatizo.

Zamani tulikuwa tunawatambua walimu kwa umahiri wa kufundisha leo hii tunawatambua walimu kwa umahiri wa kuongea na media.

Niendelee kuwapongeza wahadhiri wa vyuo vikuu kwani pamoja na maslahi yao kuwa hayakidhi mahitaji lakini wanachapa kazi hadi usiku kwenye vyuo mbalimbali.

Nashauri serikali ibane zaidi admission criteria za ualimu ili kuondokana na masela kwenye tasnia ya ufundishaji.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Mtoa mada hongera kwa kufikirisha kichwa kwa kiasi kidogo.
Ungefikiri zaidi ya hapo ungeona changamoto zilizopo kwenye kibarua cha ualimu na ungeainisha changamoto hiyo pamoja na aina ya wanafunzi waliopo mashuleni.
Sipati shida sana kwa hili kwani kuna usemi unasema" thinking is difficulty that's why most of people judge"
 
Wewe ulishawahi kuangalia hata homework ya Mtoto wa ankali/shemeji yako mpaka ujione leo hii unamjua mwalimu nje ndani?
 
jina lako tu linaonesha jinsi ulivyo ''jinga'' yaani ww ni kubwa la majinga duniani ,ungekuwa karibu ningekuzaba kofi, muulize mama magufuli'
 
Mtoa mada hongera kwa kufikirisha kichwa kwa kiasi kidogo.
Ungefikiri zaidi ya hapo ungeona changamoto zilizopo kwenye kibarua cha ualimu na ungeainisha changamoto hiyo pamoja na aina ya wanafunzi waliopo mashuleni.
Sipati shida sana kwa hili kwani kuna usemi unasema" thinking is difficulty that's why most of people judge"
Kuna sekta isiyo na Changamoto hapa Tanzania...kwa nini siku zote mnataka ku-paint picture ya kwamba changamoto ni kwenye shule na walimu pekee wakati kuna maeneo kama mahakama na mahakimu,Zahanati na wahudumu wa afya ni maeneo yanayohitaji intervention ??

Kuhusu aina ya wanafunzi naweza kukupinga kwani kwa sasa wanafunzi wanaoingia mashuleni kwa kiasi flani hawana utapia mlo kulinganisha na miaka 50 iliyopita kwa hiyo tatizo litabaki kwenu walimu....
 
Wewe ulishawahi kuangalia hata homework ya Mtoto wa ankali/shemeji yako mpaka ujione leo hii unamjua mwalimu nje ndani?
Ukanjan

Ukanjanja wenu unanifanya nitumie mda mwingi kumfundisha mtoto huku nyumbani kwa sababu mnakuwa mmemlisha 'sumu'
 
Ahahaha,Serikali huwa inatafuta mbuzi wa kafara mara zote pale inapo feli!
Ao wanafunzi wataendelea kufeli tu,kama Serikali ya CCM itashindwa kuziboresha shule zake!Punguzeni upigaji wa Pesa za Wananchi ktk IPTL,ESCROW,EPA, na ufisadi mwingine na kisha pesa hizo zielekezeni Ktk shule zenu za Serikali kwa kuzijenga vizuri na miundo mbinu yake,na pia kuboresho maslahi ya walimu muone kama hawatafaulu
 
si ajabu ukawakuta mitandaoni wanangoja kukushambulia ualimu wa siku hizi ni sekta wanayokimbilia watu waliopata maksi za chini huwezi kutegemea waliofeli wafaulishe wanafunzi nawapongeza walimu wachache pamoja na changamoto wanazopata bado wanafanya kazi zao kwa uweledi
 
Ahahaha,Serikali huwa inatafuta mbuzi wa kafara mara zote pale inapo feli!
Ao wanafunzi wataendelea kufeli tu,kama Serikali ya CCM itashindwa kuziboresha shule zake!Punguzeni upigaji wa Pesa za Wananchi ktk IPTL,ESCROW,EPA, na ufisadi mwingine na kisha pesa hizo zielekezeni Ktk shule zenu za Serikali kwa kuzijenga vizuri na miundo mbinu yake,na pia kuboresho maslahi ya walimu muone kama hawatafaulu
Ha ha ha....Uzoefu unaonesha kuwa maslahi ya walimu yalipokuwa duni wanafunzi walifaulu vizuri sana ...rejea miaka ya 90s na early 00s
 
Ulivyojinga unadhihirisha uelewa finyu wa masuala ya elimu,unafikiri matokeo mabovu ya mitihani yanasababishwa na walimu.Huu ni ujinga wa karne,mwalim ni sehemu tu ya viashiria vya ubora wa elimu.Tunapozungumzia mazingira magum ya mwl hatusemi mshahara,ni pamoja na vitendea kazi(teaching&learning resources).Lazima utambue pia teaching is a psychological work,inahitaji psychological readiness ya wanafunzi na wazazi.Ni ukengeuke wa uelewa na fikra wa kusikia kuamini kua wanafunzi wanafeli kwakua walimu wanalalamika.Remember bad results in every public sector is caused by silence of stakeholders.
 
Hivi mwaka 97 au 93 kwa mfano hayo mazingira unayoyataka yalikuwepo?
Mbona vijana walikuwa wanafaulu hadi kukosa nafasi pamoja na maksi zao kuwa juu?

Remember :Good results in a public sector can never be a product of yelling instead of hardworking..!
 
Kuna sekta isiyo na Changamoto hapa Tanzania...kwa nini siku zote mnataka ku-paint picture ya kwamba changamoto ni kwenye shule na walimu pekee wakati kuna maeneo kama mahakama na mahakimu,Zahanati na wahudumu wa afya ni maeneo yanayohitaji intervention ??

Kuhusu aina ya wanafunzi naweza kukupinga kwani kwa sasa wanafunzi wanaoingia mashuleni kwa kiasi flani hawana utapia mlo kulinganisha na miaka 50 iliyopita kwa hiyo tatizo litabaki kwenu walimu....
Napata shida hata kukujibu, inaupeo mdogo sana kufikiri.
Mwl anahaki kudai haki zake, kwa kuwa aliemfikisha hapa alipo ni serikali. Hao Madk, lawyers Wote hawatoshi. Ni Mwl nde anatakiwa awaandae. unalalamika nn.

Hujui kwa nn wengine wapo kimya? baki hivyo ulivyo
 
Hivi mwaka 97 au 93 kwa mfano hayo mazingira unayoyataka yalikuwepo?
Mbona vijana walikuwa wanafaulu hadi kukosa nafasi pamoja na maksi zao kuwa juu?

Remember :Good results in a public sector can never be a product of yelling instead of hardworking..!
Wew kweli jinga nabishana nabishana na field outskirted person.Haujui hata kufany reflective comparative analysis.Ni vyema ukajua mwl ni facilitator,kizaz cha 1900s huwezi kulinganisha na kizazi cha 2000s fearless generation,lakin pia hujui hata mfumo wa upgrade ni tofaut kwa sasa,idadi ya wanafunzi nk.its politically dominated system that concur guantitative education system.level moja kwenda nyingne lazima ufaulu,what is happening nw,hakuna mthan wa drs la nne wala form2,the only thing can make students develop reading habits is restrictive evaluation.Mlikua mnashabikia siasa za kijinga kuintervene elimu,leo unakuja na mystereous arquements.udhaifu wa hoja zako ni kuamin kua wanafunzi wanafeli kwakua walimu wanalalamika.Athari za quickfix kwenye elimu is not like massacre but deadly longrun effects.
 
Hivi mwaka 97 au 93 kwa mfano hayo mazingira unayoyataka yalikuwepo?
Mbona vijana walikuwa wanafaulu hadi kukosa nafasi pamoja na maksi zao kuwa juu?

Remember :Good results in a public sector can never be a product of yelling instead of hardworking..!
Hiyo miaka usisahau na wizi wa mitihani,
1998 mitihan ilifutwa ikafanyika January 1999.
 
Ha ha ha....Uzoefu unaonesha kuwa maslahi ya walimu yalipokuwa duni wanafunzi walifaulu vizuri sana ...rejea miaka ya 90s na early 00s
kweli we jingalao,unajua ni kwanini wanafunzi walifaulu bila kujali mazingira duni ya kazi na masilahi hafifu ya kifedha?ni kwa sababu walimu wengi walikuwa hawajuhi haki zao!walitimiza wajibu kwa moyo wote,wakidanganywa kuwa ualimu ni wito!ila vijana wa leo waliongia uko tunajua kuwa ualimu ni kazi kama zingne!una haki zako inabdi uzidai na una wajibu wako kutimiza!
 
Najua itaudhi wengi lakini ukweli lazima usemwe.

Nachelea kusema kuwa walimu kwa maana ya walimu wa shule za sekondari na msingi wa miaka hii ni wavivu,masharobaro na wanaotumia muda kulalamika badala ya kufanya kazi yenye tija.

Walimu wa leo wana mchango mkubwa katika kukwamisha ufaulu wa wanafunzi kwani ni wavivu,machekibobu na wenye hulka ya ulalamishi tofauti kabisa na enzi za Mwalimu Magufuli.

Kwa kiasi kikubwa kwa miaka takribani kumi ya Kikwete tumeshuhudia uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu hasa hasa kwenye eneo la rasilimali watu...tumeshuhudia madeni ya walimu yakilipwa huku yale ya watumishi wengine kama vile afya,mahakama,kilimo yakiwekwa pembeni.

Leo hii ukisikia madeni ya walimu basi yatakuwa ni ya mwezi wa desemba 2015 au januari 2016...lakini madeni ya kada nyingine ni kuanzia 2010 na pengine nyuma ya hapo lakini hajalipwa.

Katika sekta iliyoajiri kuliko zote kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ni sekta ya elimu...pengine ndio maana serikali ikajikuta inazoa makanjanja,machekbob na wavivu kuja kutufundishia wajukuu zetu na matokeo yake tunayaona kwenye ufaulu.

Ifike mahali walimu muwe wazalendo kama wafanyakazi wengine wa umma wanaolitumikia taifa bila kulalamika pamoja na kwamba wana madai makubwa ya stahili zao.

leo hii mwalimu akiajiriwa linatumwa fungu maalum la subsistance allowance lakini daktari akiajiriwa atasubiri neema za OC ...

Nashauri kama kuna Mwalimu anaona ananyanyasika sana huko serikalini aache kazi na sio kutujazia malalamiko as if hakuna watanzania wengine wenye matatizo.

Zamani tulikuwa tunawatambua walimu kwa umahiri wa kufundisha leo hii tunawatambua walimu kwa umahiri wa kuongea na media.

Niendelee kuwapongeza wahadhiri wa vyuo vikuu kwani pamoja na maslahi yao kuwa hayakidhi mahitaji lakini wanachapa kazi hadi usiku kwenye vyuo mbalimbali.

Nashauri serikali ibane zaidi admission criteria za ualimu ili kuondokana na masela kwenye tasnia ya ufundishaji.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Mimi ni mwalim,nna madai ya mshahara wa 2013 hadi leo sijalipwa,nadhan hata sekta ya ualim huijui wewe,nyamaza,hivi umesoma comment za mkuu wa shule wa Ilboru kwenye mwananchi la Jana??nenda kasome research za kina Kitila Mkumbo wamefanya sana kwenye changamoto za elimu,na labda nikueaidie nchi hii kuanzia walimu wa msingi hadi maprofesa huko vyuoni shida ni zilezile,me wakat nasoma UDSM wahadhir waligoma kama siku 2 sababu ya mishahara....wewe unaanza kutaja mahakama sijui afya hao si kila siku wanapishana na vitakrima,mwalimu hana alawansi yoyote uijuayo wewe,kuna baadh ya shule walim huchaanga pesa wanunue sukar ya kuandalia chai.Why hao private wanafanya vizur?moja wapo miundombinu mizur na maslah mazur.
 
Back
Top Bottom