Walimu wa kiswahili nchini Rwanda.

UKAWA2

JF-Expert Member
Apr 22, 2014
2,182
1,970
Wadau ebu naombeni mwenye ufahamu zaidi juu ya hili suala anifafanulie. Mwezi April, Rais Magufuli alipokea ujumbe kutoka kwa Rais kagame kupitia kwa waziri wa elimu wa nchi hiyo na miongoni mwa mabo ambayo Magufuri alimwahidi Kagame ni pamoja na kwamba yuko tayari kupeleka walimu wa kiswahili kufanya kazi nchini humo.

Kwa uelewa wangu nilielewa kwamba Rais Magufuli yuko tayari kufanya hivyo pale ambapo serikali ya Rwanda italeta ombi hilo au itakuwa na uhitaji wa wataalam hao wa lugha kutoka Tanzania na hivyo nikakaa kusubiria hadi hilo litokee. Cha ajabu,ukiangalia ktk website ya ubalozi wa Rwanda kuna maombi mengi sana ya walimu wa kiswahili wakiomba kufundisha nchini Rwanda sasa nashindwa kuelewa huu utaratibu ukoje?,Hawa ndio walimu ambao Magufuli aliahidi au hawa wanajaribu bahati zao wenyewe moja kwa moja kupitia kwa serikali ya Rwanda bila serikali ya Tanzania kuhusika?

Naombeni kujuzwa, tafadhali
 
Hizo taarifa ni za uongo taarifa rasmi itatangazwa na wizara husika kuhusu watu wanaotakiwa kwenda huko stay turne mda ukifika watasema tu
 
Kwenye website ya Ubalozi wa Rwanda mbona sijaona tangazo lolote la kazi
 
si unatumia smartphone sio just google it-ubalozi wa Rwanda tanzania
 
Back
Top Bottom