Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 25,301
- 40,931
Habari wanaJF,
Leo asubuhi wakati nawahi katika mishemishe za hapa na pale,nikiwa katika katika daladala kulikuwa na wadada watatu ambao walitawala stori ndani ya gari huku wakicheka kwa sauti bila kujali kuwa ni kero kwa watu wengine.Tulipofika katika kituo chao cha kushuka ambacho kinaitwa shule,kumbe wale ni Waalimu wa shule ile,kwakua daladala ilikuwa imejaa sana Konda alikua anachukua nauli kwa mtu anayeshuka.Wale wadada pamoja na mzee mmoja wa makamo kumbe ni Waalimu wa shule hiyo jirani na kituo.Zogo kubwa likatokea baada ya wote kuonyesha vitambulisho vya dogo Paul Makonda,konda akawa analaumu kwann nyie mkae gari moja huku mkijua hamlipi nauli? Zogo limepelekea hadi kutupiana maneno ambayo si ya staha masikioni mwa watu waliokuwepo eneo lile.
NIlikuwa nimekaa karibu dereva nikamuuliza huu mpango alioanzisha dogo Makonda kumbe upo nilidhani umekufa,akasema mwanzoni Waalimu mwanzoni walikuwa wanaogopa na saizi wameanza kuutumia bila woga kabisa,akaendelea kunieleza kwamba,inawezekana ugumu wa maisha umechangia na mm ninampango wa kuhama hii njia maana kuna shule nyingi sana pamoja na kikosi cha Jeshi,ivyo kuna siku unaweza beba abiria ukajua niwalipaji kumbe nusu yao si walipaji,imetupunguzia sana mapato kwakweli hasa sisi watu wa daladala za njia hii.
Shikamoo Waalimu......................