Walimu wenzangu wa ajira mpya, naomba mtupe taarifa kuhusu malipo ya pesa za kujikimu na nauli ktk halmashauri zenu.
Mimi niko halmashauri ya wilaya ya Missenyi. Mpaka sasa hatujapewa chochote na njaa inauma sana. Walimu wapya wa huku tunatamani kurudi ktk tempo zetu.
Jibu lao ni kwamba 'pesa hazijafika', wakati tunasikia kua kuna halamshauri zingine walishalipwa. Hivi hizo halmashauri walizolipwa, walitoa pesa Kenya, au Somalia?Kila mmoja atupe taarifa kuhusu hali ya malipo ktk halamahsauri aliyopangiwa, ili na wengine tupate nguvu za kwenda kudai.