Walimu tusipokee mabango ya kusifiasifia siku ya Mei Mosi, tubebe jumbe za kweli

Suleiman mchawi WA Rhymes

JF-Expert Member
Apr 24, 2022
412
990
Habari zenu,

Naenda moja kwa moja kwenye point.
Najua kwa wakati huu wale watu wanaokula kulingana na urefu wa kamba zao “chawa “ wa mama wako kwenye taratibu za kutengeneza mabango ya kusifiasifia ili tuje tupewe walimu.

Naombeni TUKATAE

Ni nani asiyejua kuwa maisha yetu walimu yamekuwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na kutokusikilizwa sisi walimu shida na kero zetu, na tabia ya kutumika na wanasiasa kama ngazi ya kufikia malengo yao iishe mara moja, badala yake walimu tujitambue ipasavyo.

Naomba walimu wote tujitahidi kubeba bango zenye jumbe zinazolenga moja kwa moja kero zetu serekalini na Watanzania wote waweze kuona kuwa sasa, walimu tunajisimamia kwa ukamilifu katika kujitetea na si kama dhana ovu inayotambaa kuwa walimu hatujitambui na ni WAOGA.

Tuache uoga kwa sababu tusipojisemea sisi nani atatusemea ??

Tunataka heshima ya kuwa mwalimu ya enzi za nyerere kurudi mara moja, lakini ni kwa jasho kwelikweli na tujivike moyo wa chuma na akili ya shaba ili kwa pamoja tufike kwenye adhma yetu na kaliba ya ualimu irudi na heshima ya hali ya juu.

TUSIBWETEKE,
LICHA YA BAADHI YA WATAWALA WALIOPITA KUWA WALIMU KWA TAALUMA LAKINI BADO HATUJAFIKIA MAISHA AMBAYO KILA MWALIMU ANA PASWA KUISHI KUTOKANA NA UMUHIMU WA KALIBA YETU NCHINI, NA HII INAONYESHA KUWA “ TUMESAHAULIKA”

IMG_5137.jpg


TUSIMAME PAMOJA WALIMU!!!
TUACHE UOGA!!!
INAWEZEKANA

kwako msomaji
Ni yule yule
Asante.
 
Hili lingewezekana endapo kungekuwa na vyama huru vya wafanyakazi, vyama vingeshindana kwa hoja hiyo siku ya Mei Mosi. Badala yake wanasiasa wanafurahia waalimu kuendelea kukandamizwa
 
Back
Top Bottom