A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mwalimu ambaye nimeajiriwa chini ya mradi wa GPE-TSP Mjini Musoma ambao unasimamiwa na TAMISEMI, tangazo la kuitwa kazini lilitutaka turipoti kuanzia 18/8/2025 na mwisho ilikuwa 31/8/2025.
Walimu wapatao 544 tuliripoti kwa awamu ya kwanza katika vituo tulivyopangiwa, na kuanza majukumu tuliyopewa kama Walimu.
Kinachotuchanganya mpaka sasa ni hatujui mkataba ukoje na miongozo ikoje, nini hatima yetu baada ya kumaliza mkataba.
Suala lingine ni kuhusu posho; hatupewi kwa wakati, mfano tulipofika kazini mwezi Agosti wengi wetu tulilipwa Novemba baada ya kufuatilia tukaambiwa walichelewa kufanya malipo kwa sababu ya kuchelewa kupokea taarifa zetu wakatuahidi kuwa baada ya hapo posho yetu tutapata kwa wakati sahihi kila mwezi.
Ajabu ni kuwa mwezi Desemba hatukupewa posho yetu na wakati huo tunatakiwa turudi kazini. January hii..Wengi tuna familia, hii ina maanisha tuna majukumu pia.
Sasa swali tunalojiuliza n tutarudi vipi kazini wakati hatujalipwa na ukizingatia wengi wetu tulipelekwa mikoa ya mbali tofauti na mikoa tunayoishi.. Hizo nauli za kwenda kazini tunazitoa wapi?a
Kibaya zaidi tukiwaambia viongozi wetu kama Maafisa Elimu wanatujibu majibu ya hovyo na yenye kukera kabisa, yaani kana kwamba tunawasumbua.
Maana wengi wetu tumeona haina haja ya kurudi kazini bora tuendelee na harakati zetu.
Pia soma:
~ Serikali yatoa magari 12 kwa wadhibiti ubora shule Wilaya
~ OWM–TAMISEMI 1,500 Volunteer Teaching Jobs | GPE–TSP 2026