Walimu poleni kwa yote mnayopitia,Sala zenu zitajibiwa Siku moja.

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
687
1,455
Walimu wengi wanatokea kwenye familia zenye background ya kipato cha chini,wengi wamesoma shule za kawaida sana,wachache ninao wafahamu walio na degree walipata division one na two pekee sababu iliyofanya kuuchagua ualimu ni urahisi wa kupata mkopo na ajira,

Fuatilia wanafunzi wanaosoma Udsm Education,utashangaa baadhi wana division one hata point NNE au hata zaida ya hapo,watanzania tujifunze kuthamini kazi za watu wengine,walimu nao ni watu,wana hisia,natamani mngejua maisha wanaoishi huko vijijini,ambako maji,vyoo na huduma zingine ni just day dreaming.
 
Respect sana kwa ulichokisema ndugu. Walimu wanapata shida sana na ukicheki watu wanawadharau na kudhani ni watu waliofeli. Labda wangetembea na vyeti vyao kama mabango ndo wangepewa heshima
 
Acheni kujifariji nyinyi walimu mkiambiwa ukweli mnadhani kama mnaonewa.Ukweli wa bila kumung'unya maneno ualimu ni kichaka na jabali kamili la waliofeli hebu rejeeni hii kauli inayotawala katika jamii zetu "eti umefel hata ya ualimu?"
 
Walimu wengi wanatokea kwenye familia zenye background ya kipato cha chini,wengi wamesoma shule za kawaida sana,wachache ninao wafahamu walio na degree walipata division one na two pekee sababu iliyofanya kuuchagua ualimu ni urahisi wa kupata mkopo na ajira,

Fuatilia wanafunzi wanaosoma Udsm Education,utashangaa baadhi wana division one hata point NNE au hata zaida ya hapo,watanzania tujifunze kuthamini kazi za watu wengine,walimu nao ni watu,wana hisia,natamani mngejua maisha wanaoishi huko vijijini,ambako maji,vyoo na huduma zingine ni just day dreaming.

Mimi walimu nawapenda, kwani wamenisomesha na kunielimisha, bila wao nisingekuwa hapa nilipo kimaisha na hata kuweza kuwasiliana kwa njia ya mtandao...Waalimu ni kweli wako katika hali ngumu kama ilivyo kwa kada nyingine mbalimbali...lakini mimi nashangazwa na baadhi ya watu wanaolalamika kuwa maisha ya walimu huko vijijini ni magumu...walimu ni watanzania kama ilivyo kwa watanzania walio vijijini...Tunachopaswa kuzungumzia ni kuimarisha au kuboresha maisha ya vijijini ili watanzania walioko vijijini maisha yao yawe mazuri...tupiganie ili huko vijijini kuwe na barabara nzuri, maji safi ya bomba, umeme na huduma nyingine...lakini siyo kulalamika kuwa eti walimu wanapata taabu vijijini, kwani watu wengine wakiwemo wafanyakazi kama mabwana shamba na wanavijiji kwa ujumla siyo watanzania?
 
Back
Top Bottom