nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Mwandishi Wetu Toleo la 291 24 Apr 2013
ASILIMIA kubwa ya walimu katika shule za sekondari nchini hawaridhishwi na aina ya mitaala wanayoitumia kufundishia, na lakini pia hawana imani na mfumo unaotumika kusahihisha mitihani ya Taifa na aina ya walimu wanaoteliuwa kuisahihisha, mambo ambayo yamedaiwa kuchangia hali ya matokeo mabaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza mwaka 2012.
Utafiti wa kiuandishi wa habari uliofanywa na gazeti hili katika mikoa 13 ya Tanzania Bara na Visiwani umeonyesha kwamba mbali na miundombinu mibovu inayoikabili sekta nzima ya elimu kwa ujumla, wengi wa wakuu wa shule na walimu wa kawaida hawaridhishwi na aina ya mitaala inayotumika katika ufundishaji nchini, jinsi mitihani inavyotungwa, mfumo wa usahihishaji na wanaoteuliwa kusahihisha pamoja na malipo wanayolipwa walimu kwa kazi yao hiyo.
Kwa mfano, katika idadi ya wakuu wa shule na walimu wa kawaida walioulizwa swali katika dodoso za utafiti huu kama wanaridhishwa na mitaala wanayotumia katika ufundishaji wao, asilimia 92 walisema hawaridhishwi, ni asilimia nane tu ya wote waliohojiwa walisema wanaridhishwa.
Aidha, katika swali lililotaka kujua kama wanaridhishwa na mfumo wa usahihishaji, kwa maana ya walimu wanaoteuliwa kusahihisha, malipo ya posho kwa kazi hiyo na ‘marking schemes,' asilimia 67 ya waliohojiwa, walisema hawaridhishwi, huku asilimia 17 wakisema wanaridhishwa na wengine asilimia 16 pia wakisema hawajui.
Eneo jingine ambalo linaonyesha kuwakatisha tamaa walimu hao na hivyo pengine kuwa chanzo cha matokeo mabaya hayo, ni malipo ya mishahara na stahili zao nyingine. Katika swali lililowataka kueleza kama wanaridhika na mishahara na stahili zao nyingine wanazolipwa kwa kazi hiyo, asilimia 89 walisema hawaridhiki na wanacholipwa na Serikali, huku asilimia nane (8%) tu wakisema wanaridhika.
Raia Mwema, pamoja na kwamba Serikali imeunda Tume ya kutafuta kiini cha matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza mwaka jana na matokeo yao kutangazwa mwaka huu, limeamua kufanya utafiti wake wa kiuchunguzi katika takriban mikoa hiyo 13 ya Tanzania Bara na Visiwani, ili pamoja na mambo mengine kubaini walau sababu za matokeo hayo.
Katika utafiti huo wa gazeti hili, mambo kadhaa yamebainishwa kusababisha matokeo mabaya hayo, lakini kubwa zaidi ikiwa ni mabadiliko yaliyofanywa na mamlaka zinazohusika na elimu, katika viwango vya madaraja ya ufaulu kutoka viwango vya zamani vilivyozoeleka kwa siku nyingi, na kuja na viwango vipya bila kuwaandaa wala kuwapa taarifa mapema walimu na wanafunzi.
Kwa mfano, viwango vya madaraja ya ufaulu kabla ya mabadiliko hayo yaliyoanza kutekelezwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza mwaka jana, ilikuwa ni asilimia 21 hadi 40 kwa daraja D, asilimia 41 hadi 60 kwa daraja C, asilimia 61 hadi 80 kwa daraja B na asilimia 81 hadi 100 kwa daraja A. Wakati daraja F ilikuwa ni kwa asilimia 0 hadi 20.
Lakini sasa, ili mwanafunzi aweze kupata daraja D, analazimika kupata alama kati ya 36 na 44, wakati daraja C ni kwa mwanafunzi anayepata alama 45 hadi 64, daraja B ni kati ya alama 65 na 84, huku daraja A ikianzia alama 85 hadi 100. Mwanafunzi anayepata alama 0 hadi 35, huambulia daraja F.
Walimu kadhaa waliozungumza katika utafiti huu wameonyesha hofu kwamba huenda matokeo kama hayo ya mwaka jana yakajirudia mwaka huu, kama Serikali, kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haitachukua hatua za haraka za kurekebisha kasoro hizo zote zinazowaathiri walimu pamoja na wanafunzi hao wa kidato cha nne mwaka jana.