Walimu kupewa laptop nchi nzima

Walimu kupewa laptop nchi nzima

yamindinda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
1,589
Reaction score
1,320
WIZARA ya Elimu nchini imeahidi kusambaza kompyuta mpakato kwa walimu 400 kila mwaka, kwa ajili ya kusaidia kupata uelewa wa masuala ya Teknolojia ya H abari na Mawasiliano (Tehama) na kuwarahisishia kazi zao.

H atua hiyo imebainishwa katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani yaliyofanyika katika wilaya ya G asabo na kuhudhuriwa na walimu wa wilaya hiyo na viongozi mbalimbali wa serikali.

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Elimu ya Msingi na Sekondari, Isaac Munyakazi, alisema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuimarisha mitaala ambapo Tehama ikiwa ni muhimu kusaidia walimu kupata uelewa utakaosaidia wanafunzi.

“Wanafunzi hawawezi kupata uelewa na masomo hayo ikiwa walimu hawana uelewa wake, katika miaka michache iliyopita tuliweka mkazo kwa wanafunzi, lakini sasa tunataka walimu na wanafunzi kwenda sambamba kupata elimu hiyo,” alisema.

Alisema kwa kuwawezesha walimu katika matumizi ya teknolojia hatimaye wanafunzi watanufaika na elimu hiyo, lakini kutokana na changamoto ya kifedha, wizara haitaweza kusaidia walimu wote kwa wakati mmoja.

Katika maadhimisho hayo, walimu walitaka serikali kuangalia upya mishahara yao kutokana na viwango vya maisha vya sasa, hivyo serikali kuahidi kufanyia kazi suala hilo.

Chanzo: Habari Leo
 
Kama ni serikali haiwezekani..
Wameshindwa kutoa zile mil 50 wataweza kwa walimu.
Halafu tatizo la walimu sio laptop
 
kenya waliahidi laptop kwa kila mwanafunzi sijui iliishia wapi
 
[emoji16][emoji16][emoji16] Labda wapewe Flash GB 2 kila mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
nia ni nzuri tatizo lipo kwa utekelezaji na changamoto ya miundo mbinu ya nchi sehemu nyingi hamna umeme labda maeneo ya mijini ndio walengwa
 
[emoji108][emoji108][emoji108]
_20181008_094042.JPG
 
naomba kujuzwa idadi ya waalimu nchi nzima ni kiasi gani.natanguliza shukrani
 
Write your reply... Bora nipate laptop yangu nasikia kuna movie mpya kibao Venom, Acquarman
 
Write your reply... Bora nipate laptop yangu nasikia kuna movie mpya kibao Venom, Acquarman
 
Shule nyingj zipo vijijini network shida hata kama sio shida inayopatikana sehemu kubwa ni 2G hizo laptop watachezea magemu au wanawapa waanzishe miradi ya burning studio?
 
WIZARA ya Elimu nchini imeahidi kusambaza kompyuta mpakato kwa walimu 400 kila mwaka, kwa ajili ya kusaidia kupata uelewa wa masuala ya Teknolojia ya H abari na Mawasiliano (Tehama) na kuwarahisishia kazi zao. Chanzo: Habari Leo
Kwanza wangehakikisha umeme umeunganishwa katika shule zote. Hapo ndio wagawe laptop.
 
Back
Top Bottom