Walimu hawathaminiwi hapa Tanzania?

Walimu hawathaminiwi hapa Tanzania?

Mr Anold

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
218
Reaction score
47
SCIENCE AND MATHEMATICS

Hili ni swali nililojiuliza mara nyingi sana, nimeitathimini kazi ya uwalimu hasa sule za sekondary hapa nchini na mazingira ya ufundishaji kwa ujumla wake. Hayo tuyaache kwanza.

Hoja yangu ya msingi ni hii.

Hivi karibuni ulitoka waraka wa kuwapandisha mshahara ngazi moja zaidi wafanyakazi wa serikali baadhi ikiwemo Watu wa IT, Engineering n.k.

Yaani mshahara wa kuanzia kwa mtu wa IT degree ni E tofauti na wengine kama mipango, elimu n.k ambao ni D.

Sasa mimi najiuliza hivi walimu waliosoma Sayansi na Hisabati wao siyo wanasayansi?

Mwenye nafasi ya kuiinua sayansi zaidi siyo mwalimu anaefundisha sayansi?

Bila huyu mwalimu hawa ma Engineer na IT officers wangepatikana vipi?

Haya jamani ni hayo tu.
 
Poleni walimu,watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
 
Poleni walimu,watanzania daini katiba mpya ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana
Siyo hivyo inabidi wawe wanakimbia mmoja mmoja km mkulu alivyofanya.

Ona leo anawatamkia walimu na wanafunzi wao kuwa km mshahara ni mdogo wakalime,kasahau kuwa alikuwa mwanafunzi akimtegemea mwalimu na baadaye akawa mwalimu na akauacha ualimu.

Leo atakumbuka mwalimu ni nani kwake tuombe mungu amkumbushe kuwakumbuka walimu wake na walimu wenzake.
 
Kama waalimu wasiponeemeka awamu hii wasitegemee miujiza,rais alikua mwalim,waziri mkuu alikua mwalim wanajua fika taabu wazipatazo waalim labda wanafanyia kaz vuten subra one day yes.
 
Back
Top Bottom