Walimu hatuna thamani

Yatosha... sukari imepanda bei acheni kulumbana...!!!
 
Kusahihisha madaftar kunafanyika jioni
 
Siyo walimu hawana thamani Tatizo walio wengi hawajitambui, pia hawatambui misingi yao ya kazi, Fikilia Ratiba inasema masomo yaanze SAA mbili hadi SAA nane na nusu, ila kwa kutojua haki zako Mratibu anakulazimisha madarasa ya mitihani ya Taifa kama std 7& 4 , waingine darasani kuanzia SAA moja hadi SAA kumi na moja na ww unakubali ,hiyo inaonyesha wengi wao ni waoga , fuata misingi ya kazi acha kulalamika.,kama ni mapunjo fuatilia ni haki yako, Kupanda daraja toa malalamiko yako , ingawa wengine unakuta ana grade A lakini ndani ya miaka 5 amepanda daraja hadi E, inahitaji kupambana sana ili kufikia malengo.

 
Ha ha haaa! Pole sana jiingize hatakijiti najua panawasha
 
Haya yote yanaletwa na Sera ya elimu bure kwahiyo walimu ndo tunagharamia hiyo elimu bure....
 
Mwalimu mwenyewe hajielewi serikali na watoto watamuelewaje??
 
mwalimu em fanyeni kufelisha madogo.. yaan hakikisheni watakaofeli mwakani wanavunja record ya mwaka huu... yaan mnaongea kwa vitendo mbona serikali itatia adabu... bampa tu bampa hakuna haja ya kulalamika!
Unajua mi walimu wa nchi hii nawaona wajinga kiasi cha kupindukia.

Nadiriki kuwafananisha na mpishi wa ndani, anayepika chakula cha bosi wake, anapakua chote anampelekea bosi bahati mbaya anamwambia hakitoshi, na wakati yeye ni mpishi tu halafu mpishi yule anahangaika kwenda kukopa dukani ampikie bosi cha kutosha,
Mpishi mzuri ni yule kwanza anahakikisha bosi wake anakula chakula ambacho hata yeye amekula, kisipo tosha aviache aone kama bosi asiposhiba mara mbili mara tatu na wakati mwingine akose kabisaaa uone ataamua nini.

Sasa tuje kwa walimu, utamkuta mwalimu anahangaika mpaka kununua vitu vya kufundishia halafu anabwabwaja eti mshahara hautoshi,
Mwalimu unajijua kabisaa nyie ndio chesesi ya nchi yoyote, mnaweza amua hivi:-
1. Wacheni maneno fanyeni kwa vitendo.
Sio kufoka tu kwenye kibodi kama watoto huko mnadai haki zenu.
2. Tafute miaka kama 7 au 10 ya kuhakikisha hakuna divi 4 yaani zianzue 0 kushuka chini. Na atakaewauliza mumwambie bayana.
Ili ualimu uheshimike, kwanza nyie vizazi vya walimu mliopo mjitoe muhanga sawasaw na wale wazee waliouza maisha yao kutafuta ukombozi.
Wazee walikufa sanaa ndio maana sisi leo tupo hapa tunafurahi,

3. Daini masilahi mapana na sie yale ya kiu tuu.
Eti mwalimu unasimama unadai hela ya likizo, na ambaye hajaenda likizo jee ajitoe kwenye harakati?? Muache ubinafsi
Mnakua na kiu kama ya mvuta sigara, atahaha kuitafuta weeee hata kwa gharama akivuta mikupuo miwili akianza kurudi alichokipata hakipo tena??
4. Amueni kufanya mapinduzi kifikra kwanza kabla ya kitu kingine.
Walimu waliowengi wametekwa ki fikra kuliko kada yoyote ile, mi mwanzoni nilifikiri kutojiamini kwa mwalimu kunatokana labda kwa kuwa matokeo yake huko nyuma sio mazuri.
Lakini wapo watu ambao mwalimu anawazidi ki elimu kwa mbaali sana, matharani ulinzi na usalama, afya hasa hawa wa chini, nafundi n.k
Lakini wao wanajiamini tatizo ni kwa walimu tuu

5. Kataeni kutumika kisiasa
Hii itawafanya mjisimamie vema katika maamuzi yenu.


Mwishooo

Kama haw wasikii tafuteni miaka kama 7 au 10 ya kufelisha kwa kiwango cha divi zerooo.

Pia,
Daini haki zenu kwa pamoja sio kila mtu anakuja na vilisiti vyake, utakuta unapiga kelele weee unachodai hakifiki hata milioni tatu, hiyo ni njaaa itakua inakusumbua.

Fanyeni mapinduzi na maamuzi magumu kama babu zetu.

MASLAHI MAPANA NA MAZINGIRA BORA YA KUFANYIA KAZI KWA WALIMU, YAKO NDANI YA FIKRA PEVU MTAVYOTAKA NINYI NA SI SERIKALI
NYINYI NDIO MNAPASWA MUIAMBIE NINI SERIKALI CHA KUFANYA NA SI SERIKALI KUWAAMBIA CHA KUFANYA.


MFANO TU MDOGO

UKIMUAJIRI FUNDI AKUJENGEE NYUMBA, MWISHO WA SIKU ATAKUELEKEZA VITU VYA KUFANYA NA KUKUSANYA, NA SIO WEWE KUANZA KUSHIKA PIMA MAJI NA KUMUELEKEZA FUNDI CHA KUFANYA.






NARUDIA TENA WALIMU JIVISHENI MIOYO YA KISHUJAA KUWAANDALIA MAZINGIRA MAZURI WALIMU WAJAO.

UKOMBOZI HAUJI BILA KUMW........
 
Siku hizi walimu mkileta mada zenu za kulaumulaumu humu ndani viboko.
Kila kitu kinakwenda kwa sheria na taratibu .Kama unaona unaonewa au unadai haki zako nenda sehemu husika ili wakupe taratibu za kufuata
Hivi angekuja kulaumu mwanajeshi ungemwambia habari za viboko??? Embu muwache dharau kwa walimu.


Hafu na nyie walimu muamke muache ujinga sasa, felisheni ili heshima yenu ije.
 
Sio siri mi ningekuwa serikali ningepunguza mishahara kwa walimu haiwezekani shule ipo mjini kila kitu kipo alafu matokeo ya necta wanatoka wanafunzi kum Kati ya mia mbili alafu mda wenu wa kazi ni kidogo Sana almost masaa sita hadi Saba kwa siku
Walimu wajinga sana.

Hao wa mjini wangeungwa mkono na hawa wa vijijini maana halisi ya mwalimu ingekuwepo, sasa utakuta usaliti kati yao kibao tuu

Mwalimu felisheni kwa kipindi cha miaka kumi mfululizo tuone hao wa kuwalipa mamilioni watawatoa wapi
 
!
!
Pole bwana mkubwa.........ila ni uvivu wako ndio uliokuponza mpaka ukaishia kuwa mwalimu, ungekuwa na alama nzuri usingekuwa mwalimu. Komaa tu haina jinsi
Acha dharau, sema hivi mialimu ni mijinga tuu,
Hivi polisi ana alama gani?
Mwanajeshi ana alama gani??
Mtendaji ana alama gani?
Ma bibi na mabwana shamba wana alama gani??
Wale wazee wa baraza huku kwenye mahakama zetu wana alama gani??
Ma FFU wana alama gani?
Madereva wa serikalini wana alama gani??
Wale madada wa mapokezi wana alama gani?
Hawa manesi huku hospitali na vituo vya afya wana alama gani??


Tatizo walimu wametawaliwa na ujinga ulio juu sana, kazi kukinga migongo kwa wanaokuja kuwatuna tu

Inajulikana dunia kote hakuna wasomi bila mwalimu,
Walimu wengine duniani wanajielew lakini wa huku kwetu kama MAZUZU tu.

Nikupelekwa pelekwa tuuuuuuu.
 
Kwa ushauri huu mwalimu atakae ufuata kesho tuuu atakuwa ni mtu mwingine katika jamii

Tatizo ya kaxi ya ualimu ni kama uteja ambao arosto yake hutolewa na kuwa bize na madaftari ya vitoto.

Ukiona hulizika fanya mishe zako maanake walimu mumeongea sanaaaa sasa ilikuwa ni wakati mfanye mambo yatakayofanya wengine wawasaidie kupaza sauti,

Felisheni sana ili wazazi, serikali na wadau wengine wapaze sauti kwa kuliona tatizo.

Sasa nyie na vi here here vyenu mnafoka mazingira magumuu ooo sijui nini, huku mitihani ikija inaonyesha mumefaulisha. Atakayekuelewa ni mjinga tuuu, FELISHENI SANAAAAAA ILI MTAKAPOULIZWA MSEME MAXINGIRA NI MAGUMU, MTASIKIKA ANGALAU.


UTAKUTA HUKO MIKOANI AMBAKO HAKUNA MIUNDO MBINU NDIO MMEFAULISHA HAFU MNALIA LIA

FELISHENI KWA BIDII NA IKIWEZEKANA MCHANGISHE KA HELA KIDUCHU KA KUZAWADIA MWALIMU ALIYEFELISHA SANAA

HII ITACHUKULIWA KAMA NEGATIVE REINFORCEMENT KWA SERIKALI,

MAANA YAKE MMETUMIA POSITIVE REINFIRCEMENT KUONYESHA KUWA KUFAULISHA MBAWEZA JAPO MAXINGIRA NI MAGUMU, LAKINI SERIKALI HAIONI MSAADA WENU.

BADILISHENI MBINU KUONYESHA KWELI MNAUMIA.
 
yaan kwa commet hizi nilizozisoma... kama kuna mwalimu atakuja kulalamika tena basi huyo atakuwa anahitaji matusi... tushachoka na malalamiko ya mdomo.. fanyeni kweli kama mmechoka..!
 



!
!
umenisaidia sana kusema nlichotaka kusema...mijinga mno
 
askari yuko mbali sana ndgu maana hata ile posho ya askari katikati ya mwenzi tofauti ni ndogo sana na takehome ya ticha.
Binafsi nawalaum viongozi wao WCT wamekaa kiukada sana.
Chama chao ndo kinawaumiza
 
"Mchawi wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe"Tafakarini.
 
Ualimu ni wito





.............endeleeni kuvumilia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…