Walimu Dodoma kuandamana kesho

Walimu Dodoma kuandamana kesho

nyatidume

Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
6
Reaction score
0
Waalimu wote wa secondari waliosimamia mitihani ya kidato cha pili wamejipanga kuandamana Kesho kuelekea manispaa kwa DED kudai Malipo yao ya kusimamia mitihani. Pamoja na kufanya kazi bila Malipo lakini hata Malipo yalipoanza kutolewa Leo, DED amekata kila mwalimu elfu kumi na elfu ishirini ya Malipo ya semina bila maelezo yeyote.
 
Hii nchi walimu wanasota kweli kweli. Mwenzao Gratian Mkoba anakula good time tu.
 
Walimu ondoeni takataka pale CWT ndipo mdai haki zenu..! Mukoba anawaangusha na Chama chake cha CCM!
 
[h=2]Walimu hawa hawa hawakujitokeza kudai malipo yao lakini hapa wamejitokeza!!

Walimu Dodoma waandamana kumuunga mkono Lowassa.[/h]


Na Thobias Mwanakatwe



8th June 2015


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa






Lowassa-08June2015.jpg

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.


Mamia ya walimu wa Manispaa ya Dodoma wamefanya maandamano ya amani na kutoa tamko la kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika mbio zake za kuwania urais uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Maandamano hayo wameyafanya kupitia umoja wao ujulikanao kama Vuguvugu Maalum la Mabadiliko ya Walimu Tanzania (Vumwawata), ambalo linajumuisha walimu wa shule za msingi, sekondari na wale waliopo vyuoni ambao wanasomea ualimu.

Walimu hao walifanya maandamano hayo jana kuanzia viwanja vya Barafu hadi Nyerere Square wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali wa kumuunga mkono Lowassa.

Ujumbe katika mabango hayo ulisomeka, ‘Lowassa, walimu Mkoa wa Dodoma tupo nyuma yako, elimu kwanza iendane na posho za walimu, nyumba, mishahara minono, malipo ya madeni ya walimu pamoja na kupandishwa madaraja kwa wakati'.

Mabango mengine yaliandika kuwa, ‘Walimu mkoa wa Dodoma tunakuunga mkono Mhe. Lowassa, walimu tuna imani kubwa na wewe ndio maana tunakuunga mkono katika safari hii ya matumaini.'

Akisoma risala kwa niaba ya walimu wenzake kwenye viwanja vya Nyerere Square mjini hapa, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kikuyu, Frank Lusajo, alisema wameamua kumuunga mkono Lowassa kutokana na kutambua mahitaji ya walimu na jinsi alivyosimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata.

Alisema kutokana na ujenzi wa shule hizo, kumesaidia walimu wanapohitimu mafunzo yao katika vyuo kuwa na uhakika wa kupata ajira tofauti na miaka ya nyuma.

Lusajo alisema sababu nyingine ni kutokana na kutangaza msimamo wake wa kuweka kipaumbele cha elimu kwanza iwapo atachaguliwa kuwa rais hali ambayo itasaidia walimu kuwa na uhakika wa kupata maslahi bora.

"Walimu Tanzania tumegundua Lowassa ni mwalimu mwenzetu kwani shahada yake ya kwanza ilikuwa ni ya ualimu, amesimamia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) na leo hii Watanzania wanyonge wana uhakika wa kupata usaili katika chuo hicho," alisema.

Alisema ukosefu wa nyumba za walimu limekuwa ni tatizo sugu na la muda mrefu na linazorotesha maendeleo ya walimu na hivyo kuchaguliwa kwa Lowassa ataweza kusimamia ujenzi wa nyumba hizo kama alivyofanya katika ujenzi wa shule za sekondari.

Walimu hao walitoa ombi kwa Lowassa kama atafanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais aweke utaratibu wa kuwaanzishia maduka maalum ya walimu kama ilivyo kwa wanajeshi na polisi.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom