Hii serikali haipati akili tu? si wawaandae walimu toka mikoa husika? Ama si wawape maslahi yanayoridhisha? MWalimu ni mtu muhimu sana katika jamii. Mwalimu akiharibu tujue na mwanafunzi ataharibu tu! Na ndio maana tunakuwa na dotcom wengi kwa jamii. katika nguzo mojawapo za uchumi, incentive ni muhimu sana. Nafaidikaje na jambo fulani?
Kila mmoja anahitaji motisha wa namna fulani na sio kudanganyana kujazana uzalendo na wito ambavyo katika hili soko huria ni mambo ya kutiliwa shaka. Wanasema tena hakuna vya dezo dezo. Nipe nikupe. Mwalimu anaizalishia serikali/jamii wasomi. Mpeni mazingira sahihi ya kutekeleza wajibu wake ili mwishho wa siku muweze kumbana. kwamba tulikupa vitendea kazi na rasilimali zote ulizotaka. wapi output yako? Lakini kwa mazingira ya sasa ni vigumu kumbana mwalimu kwa staili hii.
Hata hiyo wanayoita OPRAS-Open Performance Review and Appraisal System haina maana katika mazingira kama haya. Maana ili hiyo OPRAS ifanya kazi kwa ufasaha inabidi mwajiriwa apewe kila kitendea kazi anachohitaji ili mwisho wa siku mkikaa na mwajiri muanze kufanyiana tathmini bila mizengwe. Na hii si kwa walimu tu bali kwa sekta nzima ya umma. Sekta binafsi wanaweza kutekeleza hili maana wao hawana ruzuku toka serikalini.
Serikali inayajua haya yote ila sijui tatizo ni nini. Angalau mi naweza kujitetea sijui mfumo wa nchi unavyoendeshwa. Lakini hata rais hajui matatizo ya watz??????!!!!!!!!