walikuja Dar mkawafukuza!

walikuja Dar mkawafukuza!

kweli aisee ,wanawaita machingguy,halafu neema imepatikana kwao napo wanataka kuwadhulumu,wamewafukuza sana kule kongo na msimbazi tena kwa virungu na kumwagiwa bidhaa zao.
 
Gesi itanufaisha watanzania wote said jk, kwa hiyo anataka ijenDar kwani Mtwara sio Tanzania?
 
Walichangiwa nauli na ndugu zao wakasafiri mpaka bandari ya salama!
Wakafika Dar salama usalmini!
Wakaanza ujasiriamali mkawaita wamachinga!
Punde mkaona wamefanikiwa!mara mkawaona ni kero!
Mkawafukuza Dar kwa virungu vya mgambo!
Wakaona isiwe tabu!wakarudi Ntwara!
Wakaendelea na kilimo cha jembe la mkono!
Mara wakaambiwa Ntwara kuna hazina!
Hazina nyeti ya gesi!
Wakapumua na kusema ,sasa umasikini baasi!
Mkawafariji na kuwaahidi kwamba gesi ni mkombozi na viwanda mtavipata!
Wakawapa fursa kwa kuwachagua ili mtekeleze hayo mliyowaahidi!
Loh!mkawaacha kwenye mataa!
Tena mnajigamba Gesi lazima ikabwage moyo hukoo bagamoyo!
Sasa wanasema hapana 'Gesi haitoki hata kwa mrija wa pen'
HAO NDIO WAMACHINGA!

Hongera, uko sahihi kabisa!
 
Shairi zuri sana ila nasikitika linasomwa na sie tu
 
Walichangiwa nauli na ndugu zao wakasafiri mpaka bandari ya salama!
Wakafika Dar salama usalmini!
Wakaanza ujasiriamali mkawaita wamachinga!
Punde mkaona wamefanikiwa!mara mkawaona ni kero!
Mkawafukuza Dar kwa virungu vya mgambo!
Wakaona isiwe tabu!wakarudi Ntwara!
Wakaendelea na kilimo cha jembe la mkono!
Mara wakaambiwa Ntwara kuna hazina!
Hazina nyeti ya gesi!
Wakapumua na kusema ,sasa umasikini baasi!
Mkawafariji na kuwaahidi kwamba gesi ni mkombozi na viwanda mtavipata!
Wakawapa fursa kwa kuwachagua ili mtekeleze hayo mliyowaahidi!
Loh!mkawaacha kwenye mataa!
Tena mnajigamba Gesi lazima ikabwage moyo hukoo bagamoyo!
Sasa wanasema hapana 'Gesi haitoki hata kwa mrija wa pen'
HAO NDIO WAMACHINGA!

Ukimuudhi mwanadamu akafika mahali akasema basi imetosha ndio matokeo yake yanakuwa hivi, ni kama mnyama paka ukimfungia ndani ukaanza kumuadhibu atakimbiakimbia lakini akikubadilikia huwezi kuamini ndio yule aliyekuwa anakimbiakimbia maana atakurarua vibaya sana.

Serikali hii chini ya CCM wana kazi ya ziada katika kutuliza hili wanatakiwa watumie busara ya ziada waache visingizio eti wapinjani ndio wanachochea hili, ukweli uko bayana hata baba akileta nyama nyumbani mama humpendelea zaidi. Wananchi wa Ntwara pengine wanahitaji kitu kidogo tu mfano ajira za uhakika kwa watoto wao na umeme wa uhakika katika eneo lao ambapo itafungua njia na fursa nyingi za kiuchumi.

Huko nyuma kama mtakumbuka Ntwara ilikuwa kama ukanda wa adhabu kwa mtumishi wa umma aliyeonekana hafai, walikuwa wahamishiwa huko ambapo kufika tu ilikuwa adhabu, nyama ya ng'ombe ilikuwa hadithi kuipata nk. serikali sasa imeboresha usafiri sasa iangalie na hili la gesi kwa busara tatizo litaisha lakini kama itaweka ubabe mbele basi tutegemee kuona BOKOHARAM Ntwara.
 
Sio siri kusini bado sana! Waacheni tu walalamike jamani, tangu uhuru barabara haiishi tu, leo Mungu kajalia wamegundua rasilimali bado wanaitolea macho!
 
Mkuu Uda,

Sijui kama ni shairi, wimbo, kisa, au habari...all I know is good, and very true, and concrete thinking.
 
Last edited by a moderator:
Ni UAMSHO wa kweli kwa jamii ambazo zina HAZINA ya kweli na hawana maendeleo! Big Up sana wana NTWARA
 
Mpendwa Uda, umeandika maneno mafupi kwa mfumo wa ushairi fulani, lakini ni maneno mazito yanayoakisi ukweli, maana tunaambiwa ukweli daima utasimama milele.

Wana wa Mtwara wana haki ya kutoa kilio chao hadharani na jamii nyingine imewasikia na kuwaelewa, ambao bado hawataki kuelewa ni kwa sababu ya ubinafsi wao, kiufupi ni mafisadi na hawa ni wachache tu, sema wana pesa na nguvu ya dola. Ni hatari kwa nchi kuongozwa na kikundi kidogo cha watu, tena chenye mlengo binafsi wa kujitazama wao wenyewe kama wanavyofanya watawala wetu wa sasa, hapo ndipo serikali yetu ya ccm ya awamu ya nne chini ya JK, imetufikisha kama taifa.

Ni hatari, kwa vile watawala wanaamua kujifungia wenyewe na kuamua kujigawia raslimali zetu wenyewe, sioni ajabu hata wananchi wa kawaida wanapokosa imani juu ya hawa watawala na kusema sasa sisi basi, inatosha, watawala wanasababisha wananchi wameanza kufikilia kibinafsi kama ambavyo watawala wanatufundisha kwenye awamu hii ya nnne.

Wametufundisha mengi mabaya na sisi wanainchi tumekubali hilo somo na kuanza kulitenda, na tunapolitenda fundisho walilotufundisha wanaingiwa na hofu, kumbe hawakulifanyia upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kutufundisha. Wametufundisha kufikilia kikwetu zaidi, kila kitu kizuri Bagamoyo, wametufundisha kupeana nafasi kwa msingi wa mwenzetu, wametufundisha kupeana nafasi na mambo mazuri kwa msingi wa dini zetu na wapi tunapotoka, nk. Huko ndiko walipotufikisha, hakika dhambi hii itawarudia na kuwatafuna mpaka mwisho wao, wameanza wana wa Mtwara, kesho utasikia Loliondo na kwingine kwingwi.
 
Last edited by a moderator:
Well said sister,nguvu inayoelekezwa kuwatoa uhai ingeelekezwa kwenye kusikiliza mahitaji ya wana Ntwara serikali ya chama cha kijani ingekuwa kweli SIKIVU,lakini kumbe usikivu ni kwa MAFOGOO tu(mafisadi) sie wenye rasilimali tumebaki wa kupigwa mabomu na kumwagiwa maji wa kuwasha!
this is not fair,tumenyanyasika sana kwa miaka mingi,lets call it quits!kuna ubaya gani viwanda kujengwa Ntwara..?Dar si wanalalamika pamejaa....mafoleni...moshi mzito toka viwandani..msongamano mkuuubwa wa raia...uchafuzi wa mazingira!!!..sasa wanataka waongezee na wafuasi wa gesi hapohapo Dar?
kaka Ben Nkapa si atie neno apo maana naamini yeye is more a great thinker than ------!:yell:
 
Walichangiwa nauli na ndugu zao wakasafiri mpaka bandari ya salama!
Wakafika Dar salama usalmini!
Wakaanza ujasiriamali mkawaita wamachinga!
Punde mkaona wamefanikiwa!mara mkawaona ni kero!
Mkawafukuza Dar kwa virungu vya mgambo!
Wakaona isiwe tabu!wakarudi Ntwara!
Wakaendelea na kilimo cha jembe la mkono!
Mara wakaambiwa Ntwara kuna hazina!
Hazina nyeti ya gesi!
Wakapumua na kusema ,sasa umasikini baasi!
Mkawafariji na kuwaahidi kwamba gesi ni mkombozi na viwanda mtavipata!
Wakawapa fursa kwa kuwachagua ili mtekeleze hayo mliyowaahidi!
Loh!mkawaacha kwenye mataa!
Tena mnajigamba Gesi lazima ikabwage moyo hukoo bagamoyo!
Sasa wanasema hapana 'Gesi haitoki hata kwa mrija wa pen'
HAO NDIO WAMACHINGA!

watakoma nao, awape mgongo wabembee.
 
Wana mtwara tafadhalini sana msilegeze kamba, komaeni na hao wezi wa rasilimali za nchi yetu! Wamezidi kujimilikisha wao na familia zao.....
 
Ni hasira za simanzi la muda mrefu!
Wamekata tamaa ya kuishi......wamejiona hawapendwi.

Tunaweza kusema wanachochewa,sikatai ni kweli !
Swali ni moja tu kuna mtu aweza chochea pasipo moto?
Tuzime moto na sio wachochezi wa moto kwani hata upepo unaweza kulipuwa moto huo!

Waswahili wanasema "ukila na kipofu usimguse mkono", wakimaanisha hata kama mtu ni mjinga unamuibia, usimuibie kwa pupa mpaka hata yeye mjinga akajua unamuibia.

"Viongozi" waliweza kabisa kufanya mambo ya "kula mbakishie baba", wale vizuri tu na angalau vimakombo wawabakishie wananchi.

Sasa wao wanataka kuishi kama wafalme wakati wananchi wao hawana kitu.

Ona hapa wametumia shilingi bilioni 1.4 kukarabati nyumba ya mkuu wa mkoa.

Tsh. 1.4 billion spent on rehabilitating the Mtwara RC’s house http://fb.me/LI1whiVy
 
Walichangiwa nauli na ndugu zao wakasafiri mpaka bandari ya salama!
Wakafika Dar salama usalmini!
Wakaanza ujasiriamali mkawaita wamachinga!
Punde mkaona wamefanikiwa!mara mkawaona ni kero!
Mkawafukuza Dar kwa virungu vya mgambo!
Wakaona isiwe tabu!wakarudi Ntwara!
Wakaendelea na kilimo cha jembe la mkono!
Mara wakaambiwa Ntwara kuna hazina!
Hazina nyeti ya gesi!
Wakapumua na kusema ,sasa umasikini baasi!
Mkawafariji na kuwaahidi kwamba gesi ni mkombozi na viwanda mtavipata!
Wakawapa fursa kwa kuwachagua ili mtekeleze hayo mliyowaahidi!
Loh!mkawaacha kwenye mataa!
Tena mnajigamba Gesi lazima ikabwage moyo hukoo bagamoyo!
Sasa wanasema hapana 'Gesi haitoki hata kwa mrija wa pen'
HAO NDIO WAMACHINGA!

Eh! Nzuri hii, kama ile ya 'Nyuki wamechachamaa' ya Mzee Mwanakijiji. Kuwa Nabii sio lazima uandike Biblia au Msahafu!
 
Walichangiwa nauli na ndugu zao wakasafiri mpaka bandari ya salama!
Wakafika Dar salama usalmini!
Wakaanza ujasiriamali mkawaita wamachinga!
Punde mkaona wamefanikiwa!mara mkawaona ni kero!
Mkawafukuza Dar kwa virungu vya mgambo!
Wakaona isiwe tabu!wakarudi Ntwara!
Wakaendelea na kilimo cha jembe la mkono!
Mara wakaambiwa Ntwara kuna hazina!
Hazina nyeti ya gesi!
Wakapumua na kusema ,sasa umasikini baasi!
Mkawafariji na kuwaahidi kwamba gesi ni mkombozi na viwanda mtavipata!
Wakawapa fursa kwa kuwachagua ili mtekeleze hayo mliyowaahidi!
Loh!mkawaacha kwenye mataa!
Tena mnajigamba Gesi lazima ikabwage moyo hukoo bagamoyo!
Sasa wanasema hapana 'Gesi haitoki hata kwa mrija wa pen'
HAO NDIO WAMACHINGA!
99.9999999999999999999% unakaribia kwenye ukweli maana sidhani kama hao waliokuwa wakipigana ni wafanyakazi wa kwenye maofisi!Malipo ni hapahapa duniani tena unalipa wewe mwenyewe hakuna wa kukulipia.Ni mda wao kulipa waliyofanyiwa
 
Wana mtwara tafadhalini sana msilegeze kamba, komaeni na hao wezi wa rasilimali za nchi yetu! Wamezidi kujimilikisha wao na familia zao.....
siku hizi rasilimani za nchi zimeanza kuwa za kishemeji sio familia tu
 
Back
Top Bottom