jana Krismasi, wateja walikwenda banki ya CRDB Tawi la Mlimani City wakiamini itafunguliwa saa 4 asubuhi na kufungwa saa 8 mchana kama tangazo lao mlangoni linavyosema siku za wikiendi na sikukuu. cha ajabu, mlinzi mmoja akapewa jukumu la kuwatangazia wateja kwamba hawatafungua tawi hilo mpaka tarehe 26.
Hoja yangu si wao kutofungua bali nilishangaa ni kwa nini hawakubandika tangazo kama ilivyo utaratibu?
nilidodosa kutoka kwa mfanyakazi mmoja wa benki moja ya CRDB jijini Dar akasema utaratibu ni kwamba, inapotokea tawi linataka lisifunguliwe siku ya sikukuu, linapelekwa ombi kwa bosi wao, Charles Kimei, akikubali, wafanyakazi wanatangaziwa kisha wanabandika tangazo ili kutengue lile tangazo lao la kudumu mlangoni ambalo lina maelekezo ya muda wa kuingia kazini kuanzia Jumatatu-Ijumaa halafu Jumamosi, Jumapili na sikukuu.
wateja waliumia sana, tunaomba uongozi uliangalie hili.