Walibya waandamana kupinga uingiliaji wa Ufaransa

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,187
Reaction score
24,580
Walibya waandamana mjini Tripoli kulaani hatua za Ufaransa dhidi ya nchi yao
Apr 27, 2019 12:58 UTC
Raia wa Libya wamefanya maandamano katika medani kuu ya mji wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njazo kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya serikali ya Paris dhidi ya nchi yao.
Washiriki wa maandamano hayo wamelaani vikali operesheni za Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi linalojiita 'Jeshi la Kitaifa la Libya' pamoja na uungaji mkono wa kijeshi wa Ufaransa dhidi ya nchi yao. Mtu mmoja katika maandamano hayo amenukuliwa akisema: "Sisi wazawa wa Tripoli kama walivyo wakazi wa miji mingine ya Libya, tumekuja hapa kuonyesha upinzani wetu kwa utawala wa mtutu wa bunduki wa Haftar na mashambulizi yake." Siku chache zilizopita, kanali ya televisheni ya Al Jazeera iliripoti kwamba, meli ndogo ya kivita ya Ufaransa ilituma silaha na zana za kijeshi kwa wapiganaji wa Khalifa haftar nchini Libya.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, boti ndogo za mwendo kasi zilitumika kupakua shehena ya silaha kutoka kwenye meli hiyo ya kivita ya Ufaransa. Aidha wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Abdelkrim Zbidi alinukuliwa akisema kuwa maafisa wa usalama wa nchi hiyo waliwatia mbaroni watu 13 wakiwa na pasi za kusafiria za Ufaransa kwenye kivuko cha Ra's Ajdir katika mpaka wa Libya. Wiki iliyopita serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya ilitangaza kukata ushirikiano wake wa kiusalama na Paris kutokana na hatua ya Ufaransa ya kuliunga mkono kundi la wapiganaji wa Khalifa Haftar. Wapiganaji wa kundi hilo walianzisha mashambulizi makali tarehe nne ya mwezi huu dhidi ya mji wa Tripoli sambamba na kushambulia makao makuu ya serikali ya Maridhiano ya Kitaifa mjini humo. Hujuma hizo hadi sasa zimepelekea karibu watu 270 kuuawa na wengine 1300 kujeruhiwa, sambamba na watu elfu 35 kuwa wakimbizi.
4bsg04363e490b1eqso_800C450.jpg
 
Walibya waandamana mjini Tripoli kulaani hatua za Ufaransa dhidi ya nchi yao
Apr 27, 2019 12:58 UTC
Raia wa Libya wamefanya maandamano katika medani kuu ya mji wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njazo kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya serikali ya Paris dhidi ya nchi yao.
Washiriki wa maandamano hayo wamelaani vikali operesheni za Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi linalojiita 'Jeshi la Kitaifa la Libya' pamoja na uungaji mkono wa kijeshi wa Ufaransa dhidi ya nchi yao. Mtu mmoja katika maandamano hayo amenukuliwa akisema: "Sisi wazawa wa Tripoli kama walivyo wakazi wa miji mingine ya Libya, tumekuja hapa kuonyesha upinzani wetu kwa utawala wa mtutu wa bunduki wa Haftar na mashambulizi yake." Siku chache zilizopita, kanali ya televisheni ya Al Jazeera iliripoti kwamba, meli ndogo ya kivita ya Ufaransa ilituma silaha na zana za kijeshi kwa wapiganaji wa Khalifa haftar nchini Libya.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, boti ndogo za mwendo kasi zilitumika kupakua shehena ya silaha kutoka kwenye meli hiyo ya kivita ya Ufaransa. Aidha wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Abdelkrim Zbidi alinukuliwa akisema kuwa maafisa wa usalama wa nchi hiyo waliwatia mbaroni watu 13 wakiwa na pasi za kusafiria za Ufaransa kwenye kivuko cha Ra's Ajdir katika mpaka wa Libya. Wiki iliyopita serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya ilitangaza kukata ushirikiano wake wa kiusalama na Paris kutokana na hatua ya Ufaransa ya kuliunga mkono kundi la wapiganaji wa Khalifa Haftar. Wapiganaji wa kundi hilo walianzisha mashambulizi makali tarehe nne ya mwezi huu dhidi ya mji wa Tripoli sambamba na kushambulia makao makuu ya serikali ya Maridhiano ya Kitaifa mjini humo. Hujuma hizo hadi sasa zimepelekea karibu watu 270 kuuawa na wengine 1300 kujeruhiwa, sambamba na watu elfu 35 kuwa wakimbizi.View attachment 1082968
Acha laaana ya Gadafi iwatafune pumbafu zaoo
 
Wamechelewa! Wangeandamana wakati NATO walipojiingiza huko Libya wakitumia mwavuli wa UN kumg'oa Ghaddafi mwaka 2011 ila kwa sasa wanapoteza muda tu, maji wameshayavulia nguo waoge tu hamna namna.
 
Huyu Generali Khalifa Haftar ndio amekalia sehemu ya Libya yenye visima vya mafuta! Mafuta yanamwezesha anunue silaha na ndio maana Ufaransa na Trump kimya kimya wameanza kumsogelea.
Walibya wamejitakia wenyewe na wachache sana wataojitokeza kuwatetea! Hawasemi lakini wanajua Gaddafi pamoja na kasoro zake aliwatakia mema!
 
Walibya waandamana mjini Tripoli kulaani hatua za Ufaransa dhidi ya nchi yao
Apr 27, 2019 12:58 UTC
Raia wa Libya wamefanya maandamano katika medani kuu ya mji wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njazo kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya serikali ya Paris dhidi ya nchi yao.
Washiriki wa maandamano hayo wamelaani vikali operesheni za Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi linalojiita 'Jeshi la Kitaifa la Libya' pamoja na uungaji mkono wa kijeshi wa Ufaransa dhidi ya nchi yao. Mtu mmoja katika maandamano hayo amenukuliwa akisema: "Sisi wazawa wa Tripoli kama walivyo wakazi wa miji mingine ya Libya, tumekuja hapa kuonyesha upinzani wetu kwa utawala wa mtutu wa bunduki wa Haftar na mashambulizi yake." Siku chache zilizopita, kanali ya televisheni ya Al Jazeera iliripoti kwamba, meli ndogo ya kivita ya Ufaransa ilituma silaha na zana za kijeshi kwa wapiganaji wa Khalifa haftar nchini Libya.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, boti ndogo za mwendo kasi zilitumika kupakua shehena ya silaha kutoka kwenye meli hiyo ya kivita ya Ufaransa. Aidha wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Abdelkrim Zbidi alinukuliwa akisema kuwa maafisa wa usalama wa nchi hiyo waliwatia mbaroni watu 13 wakiwa na pasi za kusafiria za Ufaransa kwenye kivuko cha Ra's Ajdir katika mpaka wa Libya. Wiki iliyopita serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya ilitangaza kukata ushirikiano wake wa kiusalama na Paris kutokana na hatua ya Ufaransa ya kuliunga mkono kundi la wapiganaji wa Khalifa Haftar. Wapiganaji wa kundi hilo walianzisha mashambulizi makali tarehe nne ya mwezi huu dhidi ya mji wa Tripoli sambamba na kushambulia makao makuu ya serikali ya Maridhiano ya Kitaifa mjini humo. Hujuma hizo hadi sasa zimepelekea karibu watu 270 kuuawa na wengine 1300 kujeruhiwa, sambamba na watu elfu 35 kuwa wakimbizi.View attachment 1082968
Hawa jamaa wanateseka sana. Walishindwa kusoma alama za nyakati za iraq
 
Huyu Generali Khalifa Haftar ndio amekalia sehemu ya Libya yenye visima vya mafuta! Mafuta yanamwezesha anunue silaha na ndio maana Ufaransa na Trump kimya kimya wameanza kumsogelea.
Walibya wamejitakia wenyewe na wachache sana wataojitokeza kuwatetea! Hawasemi lakini wanajua Gaddafi pamoja na kasoro zake aliwatakia mema!
Mkuu huyu Generali khalifa Haftar je anamtambua mtoto wa Gadafi, na wakati wa utawala wa Gadafi alikuwa na cheo gani?
 
Naomba kujuzwa undani wake huyu khalifa, ni nani haswa na ametokea wapi je wakati wa utawala wa Gadafi alikuwa na nafasi gani?
Mbona upo uzi humu unaomuhusu huyo jamaa tu.
Tafuta humu, utaupata
 
Kwa kweli walivyomsaliti Gaddafi wacha wanyoroshwe mpaka waombe POO na wasahau kuishi kwa raha kama zamani
 
Mkuu huyu Generali khalifa Haftar je anamtambua mtoto wa Gadafi, na wakati wa utawala wa Gadafi alikuwa na cheo gani?

Mkuu, kwa ufupi Generali huyu alishirikiana na Gaddafi kuipindua serikali ya kifalme mwaka 1969. Alipewa cheo cha juu kwenye jeshi ya Libya, lakini mwaka 1987 alikorofishana na Gaddafi kwenye uvamizi pale Chad. Haftar alishutumiwa kutimia silaha za kemikali na Gaddafi alimuona kama mtu hatari ambaye anaweza kuwa mpinzani. Hakuruhusiwa kurudi Libya na alikimbia Marekani, na aliishi pale miongo miwili. Mwaka 2011 alirudi Libya na alikuwa mwongoni ya wale waliompindua Gaddafi. Mwaka 2014 alijitoa kwenye Serikali na alianzisha vita vva wenye kwa wenyewe (civil war). Anashutumiwa na mauaji ya kimbari (mass murder) na anajulikana kama War Lord mkali na hatari sana. [Chanzo: Wikipedia]

Mkuu, kwa ufupi huyu jamaa ni kibaraka ya Marekani na anatetea maslahi ya mabeberu!
 
Back
Top Bottom