Wali wa sausage na mboga

Elizabeth Dominic

Platinum Member
Dec 7, 2007
4,555
3,649
[h=3]JIFUNZE KUPIKA WALI WA SAUSAGE NA MBOGA MAJANI MCHANGANYIKO[/h]


JIFUNZE KUPIKA MBOGA MAJANI NA MCHANGAKO WA WALI NA SAUSAGE
MAHITAJI

3 vipande vya sausage
1 fungu la majani ya vitunguu
1 kitunguu kikubwa
100 gram njegere
500 gram chele basmati
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
JINSI YA KUANDAA FATIKLIA PICHA NA MAELEZO

Muda wa mapishi dakika 45
Muda wa maandalizii dakika 15


Huu ndio muonekano wa majani machanga ya vitunguu​


Kaanga vitunguu maji katika kikaango kwa kuweka mafuta ya kupikia kiasi​


Kisha ongezea majani mabichi ya vitunguu kama inavyoonekana katika picha​


Baada ya kukaanga kwa dakika mbili vitunguu pamoja na majani vitoe tu harufu na sio kuungua kubadilika rangi kisha weka mchele na endelea kukaanga​


Kaanga mchele kwa dakika 3 mpaka 4 kisha weka maji ya wastani yazidi mchele wako kiasi na uendelee kukoroga ili maji yachanganyike na mchele wako​


Kisha funikia na weka moto wa wastani ili wali wako uive taratibu​


Kisha chukua sausage zako na kata kata vipande vidogo​


Huu ndio muonekano wa vipande vya sausage baada ya kukata​


Kisha tupia juu ya wali wako njegere zilizochemshwa pamoja na vipande vyoote vya sausage​


Kumbuka kuendelea kukoroga ili kila kitu kichanganyike, pia kama mpenzi wa blue band au samli unaweza weka kiasi ili kuongeza ladha na harufu safiu sana katika wali wako​


Safi sana hapa kila kitu kimechanganyika na ninaimani baada ya dakika 45 wakli wako utakua umiva kama haujaiva basi ongezea maji kidogo na endelea kupika katika moto mdogo​


Ukimaliza pakua na mpatie mlaji chakula hiki kikiwa chamoto​

​

waandalie famili au hotelini kila atakae kula atafurahia sana

Kwa hisani ya Activechefblog
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom