Walemavu Wanatumika Vibaya Kwenye Uchaguzi Huu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walemavu Wanatumika Vibaya Kwenye Uchaguzi Huu!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mafuchila, Sep 29, 2010.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wanandugu,
  Nimekuwa nikifuatilia hizi kampeni za uchaguzi tangu zilipoanza. Moja ya vitu nilivyoshuhudia na kunisikitisha ni matumizi mabaya ya rasilimali watu, muda na fedha. Bila shaka wengine watasema matumizi ya vitu hivyo hayakwepeki katika kampeni za uchaguzi, hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Lakini, pamoja na hayo kuna baadhi ya mambo ambayo tunaweza kuyakwepa, na hivyo kuliepusha na fedheha taifa letu.

  Moja ya mambo ambayo wanasiasa wetu wanaweza kuyakwepa ni matumizi mabaya ya walemavu wetu. Hili nimeliona kuwa ni tatizo kwa kadiri siku zinavyoongezeka, kwani imekuwa ada kwa wagombea kujitanabaisha na walemavu kwa kiasi cha kuchefua. Suala hili 'kunyata' kwa sababu wengi kati ya hao wagombea tunawafahamu, hawana mapenzi na walemavu, na wanawatumia kwa ajili ya kununua huruma ya jamii katika kipindi hiki cha Kampeni.

  NI SUALA KISHENZI KUTUMIA WALEMAVU KUJIONYESHA UNAWAJALI, ONYESHA UPENDO WAKO KWAO KWA KUPAMBANA NA MAFISADI ILI RASILIMALI ZA NCHI ZIWANUFAISHE NA KUONDOKANA NA UNYONGE WALIONAO.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Mifano zaidi yahitajika ili tufanye uchunguzi wa kina na wahusika wachukuliwe hatua za kisheriaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...