Wale Watu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Ni usiku wa saa 6 nimetoka katika pilika za maisha za kila siku , gari linasimama katika mataa ya magomeni mapipa , ghafla watoto wadogo zaidi ya 5 wanakuja upande wa dereva kama vile wanahitaji sana msaada , dereva amefunga kioo , mimi namwangalia dereva kumuuliza kunani .

Nilipokuwa namwangalia dereva upande wangu watoto wengi zaidi ya 3 wakaja wakawa wanajaribu kufungua mlango wa upande wangu lakini ulikuwa umelokiwa wakashindwa kufanya hivyo .

Gari lilivyoondoka kumbe kulikuwa na mtoto mwingine nae anajaribu kufungua mlango wa nyuma kabisa wa gari lile , gafla akaachia buti likajifunga mwingine akachukuwa jiwe na kurushia gari lile , kioo cha mlango wa nyuma kilivunjika .

Kumbuka ukipita mchana eneo hili huoni watoto hawa , ni vijana tu wanaouza maji , magazeti na bidhaa zingine hawa vijana wakienda kupumzika sasa ndio watoto wadogo wakulipwa wanaanza kuja kufanya kazi zao pia .
………………………………………………………………………………..

Saa 6 mchana nimetoka zangu mtaa wa jamhuri naenda azikiwe , nilikuwa nalamba ice cream , ghafla mtoto mmoja wa miaka kama 7 – 10 hivi akaja mbele yangu akaniomba ile ice cream nilipopiga hatua mbele zaidi akanifuata kwa mbele akitaka ile ice cream ninayolamba mimi .

Nikamsihi asininganganie sana nitampa , nikaingiza mkono mfukoni nikampatia hela nyingine lakini pale ilikuwa ni karibu na mgahawa mmoja wa chakula nikamwambia twende katika mgahawa pale nikakununulie chakula , mtoto akakataa katu akasema anataka ice cream au hela lakini hataki kwenda kula .

Nilikuwa niko katika safari zangu nikasalimu amri nikampa hela ya kwenda kununua ice cream na nyingine ya kula kwa sababu aliniahidi ataenda kula , nikapiga hatua zingine mbele nikageuka kuona anaenda wapi .

Ndio mama mmoja mtu mzima akaja pale akachukuwa zile hela kutoka kwa yule mtoto , ndio maana yule mtoto akawa anataka hela kwa sababu alijua kuna mtu amemtuma .

……………………………………………………………………………….
Ukipita barabara ya ali hassan mwinyi kuelekea mwenge au mwananyamala unaweza kukutana na watoto wadogo wamebeba watoto pia , wengine wanajifanya ni watoto wao wengine wanajifanya ni watoto wa ndugu zao , sikumoja nilipata nafasi ya kwenda kuongea na mmoja wao .

“ mambo? “
“poa shikamoo ?”
“ marahaba ujambo “?
“sijambo “?

“ huyo mtoto uliyembeba ni wa nani ?”
“ni mtoto wangu “
“ una uhakika ? wewe una umri gani ?
“nina miaka 15 “
“mtoto wako ana miaka mingapi ?”
“ana mwaka mmoja karibu unusu “

“niambie ukweli mbona hulingani na mtoto “
“sawa , huyu mtoto ni wa yule mama aliyelala pale chini ya mti “
“ sasa kwanini unambebe wewe ?
“ nimemkondisha kwa ajili ya kuombea hela jioni namrudisha kwa mama yake na kumpa yule mama hela kidogo ?”

“ huwa unapata shilingi ngapi na yule mama unampa shilingi ngapi ?
“ siku zingine alfu 5 au zaidi “ mama huwa tunampa alfu 2 kila siku “

“ munampa ina maana mko wengi ?”
“ ndio hao wengine nao wamekodisha hao watoto nao wanamlipa yule mama “?

“ yule mama amewapata wapi watoto wote hao ?”
“ amewatoa hospitali “

“ una maanisha amewaiba hospitali kutoka kwa wazazi wengine ?”
“ ndio hospitali ya mwananyamala “

Sintoweza kuweka maongezi mengine yaliyoendelea hapo baada ya hapo lakini ukweli ndio huo wale watoto sio wao wanakodishwa kwa ajili ya kuombea hela wengine wameibiwa katika mahospitali sasa nashangaa wazazi wao huwa wanakuwa wapi au inakuwaje kuwaje .
 
Usanii wa jinsi hiyo umeshamiri sana kwa sasa kila sehemu ya Tanzania ila tu style zinatofautiana kidogo. Last week nilipita kahama kwa basi, tukasimama mizani kama kawaida kupima uzito. Tukiwa kwenye foleni, tukaona vijana (wenye nguvu na akili timamu) takribani 15 hivi wanazunguka zunguka pale eneo la mizani, mmoja mmoja wanasogea dirishani na kuomba hela ya chakula. "...nina siku tatu sijala.....nimetoka mwanza kwa miguu....naomba unisadie.....nisaidie ndugu yangu sisi sote ni watanzania......"

Sababu:
1. Hali halisi ya maisha ya mtanzania wa kawaida
2. Kuna uhakika kuwa nikiomba lazima nitapewa, hasa pale watoto wanapotumika kwenye hiyo biashara.
3. Kupitia hii njia, wanapata kipato kikubwa kuliko kiwango cha mshahara wa kima cha chini kwa mwezi.

Nafikiri yakifanyika yafuatayo tatizo litapungua:
1. Wenye mamlaka kuchua nafasi zao na kufanya kazi zao kama walivyo kula viapo na kusign TOR zao.
2. Watanzania tuache tabia ya kuwapa pesa hawa watu maana ndo tunazidi kufanya tabia hii iote mizizi. Kwa kufanya hivi wataona hawapati kitu.
 
Jamani haya mambo ni kweli yapo.Mazingira kama haya yamekwishanitokea zaid hata ya mara tano na nikule TBR,kwamba watu wazima wanawatumia watoto wadogo kuomba misaada.Mf.dada mmoja niliyekutana naye alidai kwamba ametoka kulazwa hosp hivyo alikua anaomba msaada wa nauli ili aweze kurudi nyumbani kwao,kumbe ilkua uongo.Watu hawa wamefanya hii kama ndio kitega uchumi chao.

Kama NGO'S zetu zingekua za kujituma na kujitoa basi wangeweza kulishughulikia suala hili kwa makini lakini NGO'S zetu ziko mifukoni mwa watu kwa hiyo watu hawa wataendelea kutesa kwa kuwanyanyasa watoto wasiokua na hatia.

Suala la vipi wanawaiba watoto ni kwamba wezi hao wa watoto wadogo huanza kujenga mazoea na wazazi kama wanakwenda kuwapa pole,akiona amezoeleka ndio mwanya anaoutumia kutoweka na watoto.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom