Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Upo msemo humu JF kwamba kuna vijana 46 ambao hulipwa buku saba (tshs 7,000) kila wanapoleta habari za kuitetea CCM au kila wanapoiandika vizuri. Lakini kwenye siasa za vyama vingi nadhani kwamba CCM hawapo peke yao katika kuwa na vijana wa kazi kwenye mitandao. Ikiwa wale wa CCM wapo 46, Upinzani una vijana wangapi?. Maana nadhani kwamba ni wengi zaidi hata ya mara kumi kulinganisha na hao 46 wa CCM.
Wakati wa kampeni ulinaswa mtandao fulani ambao kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, hao waungwana walikuwa ni mafundi wa masuala ya mitandao ya internet. Walikamatwa na nadhani kesi yao ipo mahakamani mpaka sasa. Hivyo ikiwa CCM inao vijana 46, nadhani wale wa upinzani watakuwa ni wengi zaidi, ingawa wanaoshambuliwa ni hao wachache.
Propaganda za kisiasa zinakuwa na faida na hasara zake kwa jamii ile ile moja. Mtu anakifaa chama kwenye mitandao ya habari na chenyewe kinamfaa maishani. Hizi ni fursa zilizoibuka katika ulimwengu wa siasa za vyama vingi.