Wale vijana wawili

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,353
Vijana wale wawili walikuwa wasomi, na walionekana kuwa asset kubwa katika chama kama ilivyokuwa kwa Tony Blair na Gordon Brown katika uongozi wa chama cha Labour. Vijana wale walipitia safari ndefu katika chama, hatimae waliwekwa makao makuu ya Chama Dodoma, mmoja akiwa msaidizi wa Pius Msekwa akiwa Speaker na mwingine akiwa msaidizi wa John Malecela akiwa waziri mkuu.

Wabunge wa wakati ule walipata shida sana ya usafiri wa kuwafikisha bungeni, magari yalisafiri usiku na wengi walilala njiani, wengine iliwachukua siku tatu/nne kufika bungeni. Ilipitishwa wabunge wote watakopeshwa mashangingi ili yawasaidie usafiri.

Waziri Mkuu alifanya biashara nzuri sana na kampuni ya Toyota, hakika wenye kampuni hawakutegemea kuwa kainchi masikini kale kanaweza kununua mashangingi zaidi ya 200 kwa mpigo tena kwa pesa taslimu. Makubaliano yalikuwa waziri mkuu apate 10% ya transaction ile.

Kama mnavyojua kuwa pesa za namna hii haziingizwi bank, basi wawakilishi wa kampuni ya Toyota walikuja na pesa kwenye briefcase wakimtamfuta waziri mkuu, bahati mbaya au nzuri waziri mkuu alikuwa safarini, lakini walipouliza, msaidizi wa waziri mkuu aliwakaribisha ofisini kwake, kijana mtanashati na mwenye sura ya kuvutia. Aliwaambia kama wana maagizo yeyote kwa waziri mkuu wamuachie yeye kwani yeye ni msaidizi wake. Ndipo briefcase lilipoachwa ofisini, msaidizi alifungua briefcase baada ya wageni kuondoka, alichokiona hakutegemea, alilichukua briefcase lile mpaka nyumbani kwake na kukaa kimya.

Waziri mkuu aliporudi aliuliza kama kuna wageni waliomfuata na kumkosa, alipewa habari yote lakini alipomuuliza msaidizi alikana, biashara yote ni ya mazabae, waziri mkuu hakuweza kulipeleka swala hili kokote.

Huu ndiyo mwanzo wa utajiri wa msaidizi na uhasama aliojijengea na watu wa chama.
 
Jamani, acheni umbea, na ujinga ujinga..!

 
Hahahahahaha vijana wale ni edward lowasa na john malecela hakika inasisimua
 
Lowassa dhuluma ndio kipaji chake kaanza zamani sana. Lowassa ndio good reflection ya CCM uroho, ulafi, kujilimbikizia mali na kutokuwa na huruma wala roho ya utu
Kabla sijakujibu ningejua jinsia yako ingenisaidia huoni michango ya maafa kule kwa kina kioo hakidanganyi wameifanya nini !??!
 
Reactions: dtj
Aiseeeee kumbe ndiko bifu la waziri mkuu na msaidizi lilikoanzia?
 


Moja jumlisha moja unapata mbili.... kama ambavyo Zanzibar na Tanganyika zilivyotoa serikali mbili.

Sasa natafuta mbili jumlisha moja ili nimjue kijana msaidizi wa spika...
 
Lowassa dhuluma ndio kipaji chake kaanza zamani sana. Lowassa ndio good reflection ya CCM uroho, ulafi, kujilimbikizia mali na kutokuwa na huruma wala roho ya utu
Acha wivu ...au ndio kawaida ya maskini kuhesabu Mali za matajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…