Wale tunaomiliki Ford Raptor tukutane hapa

Nimenunua mwaka jana niliagiza.

Tatizo lililopo ni kuwa nikiwa katika mlima gari inapush kwenda spidi zaidi wakati hiyo hali haikuwepo. Niliipeleka kwa mafundi wa kompyuta wakanipa quote ya milioni 7 ili waagizie sensa na kuifunga.

Tatizo lilianza baada ya kupata ajali, bima walirekebisha nikaendelea kulitumia nimekuja kuanza kupata tatizo miezi miwili baada ya kutoa gereji wa bima ya Wachina Mikocheni.

Niliwarudishia wachina wakagoma wakasema wao kazi yao ishaisha nikubaliane nao upya.

Kuna mtu ambaye ashakutana na tatizo hili kama kuna fundi mzuri wa ford anayemjua ili niweze kucompare hizo cost za hawa milioni 7 ndefu aisee.
Hizi gari mostly zinatumika kwenye site woek ya migodi edition iyo ya Ford ni zao la South Africa tafuta dealer wa SA utapata maelezo na spare bei cheap..
NB:Sio gari la mjini ilo wala halina maajabu yoyote kwenye city.
 
Kuna mwamba mmoja hv mwanangu ana kaford focus kakipaki mwaka wa 3 sasa hvi,ameambiwa sensa ya ufunguo sijui atoe mil 4,hizi gari inaonekana wanatakiwa kuzipush kina Balhabou tu sio wa kipato cha chini kama sisi
Ford parts zake sio ghari kwa SA zipo za kumwaga mimi nipo na Ford na parts zake nanunua huko na gari ni ngumu sio ya kuharibika hovyo na kila siku ipo road ina nguvu na balance ya kutosha...hiyo focus niliiona moja Arusha wamepaki kwa ishu ndogo tuu sijui Pump...
 
Sasa hiyo hadi leo huyo mmiliki kaipaki,kaenda kwa dealers wameshindwa kumsaidia hadi amelisusa
 
Cruise auto spare ni wauzaji wa spear party za magari
Jeep,
BMW,
Audi,
Land rover,
Porsche,
Volkswagen,
Chrysler,
Range/Land rover

Duka linapatikana MAKAO MAPYA,EDEN ROAD jirani na cafe laziz restaurant,Arusha

Kwa mawasiliano piga +255743805465,+255786050747
Email:cruisespares@gmail.com
Fb&IG:cruiseautospareparts

Pia usisite kuwasiliana nasi pia tunatoa ushauri.
Spare za Mazda Tribute mnazo?
 
Kuna mwamba mmoja hv mwanangu ana kaford focus kakipaki mwaka wa 3 sasa hvi,ameambiwa sensa ya ufunguo sijui atoe mil 4,hizi gari inaonekana wanatakiwa kuzipush kina Balhabou tu sio wa kipato cha chini kama sisi
Eeh itafika muda hata starlet itaheshimiwa😂
 
Back
Top Bottom