Wale Mnaobeza Programu ya BBT ya Rais Samia/Bashe Someni Mageuzi ya Kilimo Malaysia Kwenye Makala Ifuatayo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,833
Makala ifuatayo kutoka The Chanzo inawatia Moyo wale waliothubutu kuleta mageuzi ya Kilimo Nchini Kupitia Mpango wa Vijana BBT.

Hapa Tanzania ukitaka kufanya jambo kubwa usiwasikilize loosers ambao hawana Msaada wowote licha ya maelezo yoa marefu ambayo hayana Tija.

Rais Samia na Bashe Songeni mbele ya hiyo Program ya BBT maana ndio itakuwa muarobaini wa kuondoa Umaskini na kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini kwetu.

Nchi ya Malaysia iligjaramia Kila kitu Kwa raia wake iloyowapa Ardhi na Sasa inavuna pesa tu.

===
Kilimo na Umasikini, Malaysia na Tanzania

Mnamo Februari 2017, miaka sita sasa imepita, niliandika, kupitia ukurusa wangu wa Facebook, makala haya kuelekea kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha. Niliamua kurudi kuisoma makala hii tena kutokana na sababu mbili haswa.

Moja, nilipokuwa katika ziara ya chama chetu cha ACT-Wazalendo, chama ninachokiongoza, katika mikoa nane ya Tanzania Bara, ziara ambayo imekamilika hivi karibuni, nilikutana na umasikini wa kutisha wa Watanzania.

Kama kawaida yangu, niliwaeleza wananchi kwamba umasikini wa Tanzania unatokana na Serikali kutojali sekta ya kilimo.

Nilipokuwa Tabora, kwa mfano, nilieleza hili kwa kina, kwamba sura ya umasikini wa Tanzania ni wakulima; kwamba sekta ya kilimo ni tegemezi kwa theluthi mbili ya Watanzania lakini mchango wake kwenye Pato la Taifa ni theluthi moja tu.

Kwa hiyo, kipato kidogo kinagawiwa kwa watu wengi sana. Kisha nikapendekeza suala la kisera kuwa, kama ilivyo kwenye sekta ya madini, au mafuta na gesi, Serikali itunge Sheria ya Maendeleo ya Kilimo itakayoweka mfumo mahususi wa kodi kwa sekta yetu ya kilimo tu.

Mfumo ambao utakuwa imara kwa muda mrefu ili kuvutia uwekezaji kwenye kilimo na kuhakikisha kuwa mkulima anapata angalau asilimia 80 ya bei ya bidhaa yake katika Soko la Dunia, kwa mazao ya biashara.

Mbili, Serikali ilikuwa inazindua rasmi mpango wa kuwachochea vijana kushiriki kwenye kilimo uitwao BBT-YAI. Mpango huu, pamoja na mambo mengine, una shabaha ya kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo mpaka kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Shabaha hii ikifikiwa, na ikawa endelevu kwa miaka mitano mfululizo, tutafuta ufukara kabisa nchini kwetu.

Ni muhimu kukumbuka kwamba tafiti zilizowahi kufanyika nchini zinaonesha kwamba iwapo sekta ya kilimo Tanzania itakuwa na kasi ya ukuaji wa kati ya asilimia sita mpaka asilimia nane kwa miaka mitatu mfululizo, asilimia 50 ya Watanzania wataondoka kwenye dimbwi la umasikini. Hali itakuwaje kasi ya ukuaji ikifika asilimia 10?

Ni dhahiri itakuwa ni mafanikio makubwa na kwa mara ya kwanza tutaweza kusimama kifua mbele na kusema kuwa umasikini sasa basi. Hata hivyo, mashaka ni mengi sana. Mzee Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, alipata kusema wasiwasi, au mashaka, ndiyo akili!

Kumekuwa na mipango kama hii hapa nchini katika miaka ya uhai wetu kama taifa. Nilitafakari kama tunapozindua mpango huu wa BBT-YAI tulijifunza kutokana na makosa ya nyuma yaliyopelekea mipango kama hii kushindwa. Ndipo nikakumbuka makala haya ya kulinganisha Tanzania na Malaysia miaka ya 1970-1990.

Nimeyasoma makala haya tena na tena na, kwa hakika, siwezi kubadili hata nukta. Ni makala natamani kila mtunga sera ayasome. Kuna mafunzo makubwa kutoka nchi ya Malaysia. Karibu usome makala haya na pia kunipatia mrejesho wako:

Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961, nchi ya Malaya ilikuwa tayari ina uhuru miaka minne kabla, ikipata uhuru wake mwaka 1957. Malaya ilijiunga na Singapore, Sabah na Sarawak mnamo Septemba 16, 1963, kuunda nchi ya Malaysia.

Tanganyika ilijiunga na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miezi saba baadaye. Hata hivyo, Singapore ilifukuzwa kutoka katika Muungano wa Malaysia hapo Agosti 1965 kutokana na kutofautiana kisera kuhusu watu wa asili na namna ya kuwalinda kiuchumi.

Viongozi wa Kuala Lumpur walitaka kuweka sera za kusaidia wazawa kwa kuwapa upendeleo maalumu, wakati viongozi wa Singapore, chini ya Lee Kuan Yew, walitaka kuwepo na Malaysia moja kwa wote bila upendeleo maalumu kwa Bumiputera, watu wa asili wa taifa hilo.

Singapore ina wakazi wengi zaidi wahamiaji kutoka China, hivyo ilipinga wazo hilo na ikajitoa kwenye muungano. Tanzania imeendelea kudumu na muungano licha ya changamoto kadhaa zinazoukabili! Tanzania na Malaysia zote zilitawaliwa na Mwingereza.

Wakati Tanzania inaundwa mwaka 1964, pato la wastani la mtu mmoja lilikuwa Dola za Kimarekani 63, sawa na Sh130,000, wakati Malaysia ilikuwa na pato la Dola za Kimarekani 113, sawa na Sh250,000.

Kimsingi, nchi hizi zilikuwa sawa kimaendeleo ingawa Tanzania ni kubwa kwa zaidi ya mara tatu ya Malaysia.

Hivi sasa [Februari 2017], Malaysia kipato cha wastani cha mwananchi ni Dola za Kimarekani 10,000, sawa na Shilingi milioni 22, na Tanzania ni Dola za Kimarekani 600, swa na Shilingi milioni 1.3.

Kwa Tanzania, pato la wastani limeongezeka mara kumi takribani na kwa Malaysia limeongezeka mara elfu moja! Nini tofauti ya mikakati ya maendeleo ya nchi hizi mbili?

Kilimo kilivyoivusha Malaysia

Leo tutaangalia eneo moja tu, la kilimo, na namna kilimo kilivyoweza kuivusha nchi ya Malaysia na kilimo hicho hicho bado hakijaweza kuivusha Tanzania.

Malaysia iliunda Shirika la Umma linaloitwa Federal Land Development Authority (FELDA), likiwa na wajibu mmoja mkubwa wa kuhakikisha wananchi maskini wanapata ardhi, wanalima kisasa, na kuongeza uzalishaji na hivyo kufuta umasikini.

Kila mwananchi maskini aligawiwa ardhi yenye ukubwa wa hekta 4.1, ardhi husika ikasafishwa na kuwekwa miundombinu yote muhimu ya kilimo, ikapandwa michikichi, na mwananchi akapata huduma za ugani ili kukuza michikichi hiyo.

Shughuli zote hizi zilifanywa kwa gharama za Serikali, na wananchi wale wakapewa kama mkopo ambao walikuwa wanaulipa kidogo kidogo kila wanapovuna na kuuza migazi/mawese kwa shirika hili la FELDA.

Hivi sasa FELDA ni shirika kubwa sana, lina thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3.5, sawa na takribani Shilingi trilioni 7.7, na kupitia ushirika wao, wananchi hawa waliopewa ardhi ya kulima michikichi, sasa wanamiliki asilimia 20 ya hisa za shirika hilo!

Malaysia iliweza kuondoa umasikini kutoka asilimia 57 ya wananchi wanaoishi kwenye dimbwi la umaskini mwaka 1965 mpaka chini ya asilimia tatu mwaka 2012. FELDA sasa ni shirika la kimataifa, maana linaanza kuwekeza duniani kote.

FELDA ilipouza hisa zake kwenye masoko ya mitaji, au IPO, ambayo ni mauzo ya hisa hadharani kwa mara ya kwanza, ilikuwa ni ya tatu kwa ukubwa baada ya makampuni ya Facebook na Japanese Airlines.

Shirika la umma linalomilikiwa na Serikali, wakulima na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (EPF) na linaloendeshwa kwa misingi ya utawala bora wa makampuni, FELDA limeweza kufuta umaskini kwa zao moja tu la michikichi.

Malaysia leo inaongoza kwa kuuza mawese duniani. Michikichi hiyo ilitoka Kigoma, Tanzania, na kupelekwa Malaya na Waingereza kwenye miaka ya 1950!

Tunapokwama Watanzania

Tanzania nasi tulikuwa na shirika la umma kwa ajili ya kilimo, leo tuchukulie Shirika la Chakula na Kilimo (NAFCO).

Kama FELDA, NAFCO walichukua ardhi kubwa maeneo kadhaa nchini. Tofauti na FELDA, hata hivyo, wao NAFCO walilima wenyewe mashamba haya na kuweka miundombinu ya kilimo.

Tuchukue mfano wa mashamba ya mpunga kule Kapunga, wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya. Mnamo mwaka 1985, NAFCO walikwenda kijijini Kapunga kuwaomba wananchi wawape ardhi ya kulima mpunga.

Wananchi wakawapa hekta 3,000 hivi, kwa mujibu wa muhtasari wa Mkutano Mkuu wa Kijiji niliooneshwa mwaka 2009 nilipokwenda kutembelea mashamba haya kufuatia mgogoro wa ubinafsishaji.

NAFCO wakapata msaada kutoka Serikali ya Japan na uwekezaji mkubwa ukafanyika, ikiwemo kuweka kinu cha kukoboa mpunga cha kisasa kabisa.

Hata hivyo, NAFCO ilijiendesha kwa hasara, kwa sababu ambazo sitazieleza kwenye makala haya, na ilipofika katikati ya miaka ya 1990 ikaamuriwa kubinafsishwa. NAFCO ikauza mashamba yale kupitia Mpango wa Ubinafsishaji kwa Kampuni Binafsi.

Katika uuzaji huo, NAFCO waliuza hekta 3,500 badala ya 3,000 walizopewa na wananchi, maana yake ni kwamba kijiji cha Kapunga nacho pia kiliuzwa!

Tofauti za kifikra

Mifano hii miwili inaonesha tofauti kubwa za kifikra na kimaendeleo kati ya nchi hizi mbili. Moja iliwezesha wananchi kumiliki ardhi na imefanikiwa.

Nyingine iliamua kufanya kupitia shirika la umma, na baada ya kushindwa, badala ya kurejesha ardhi kwa wananchi na kuwawezesha kulima, ardhi ile ikauzwa kwa kampuni ya mtu mmoja!

Ujamaa wa Malaysia ulikuwa ni wa kumilikisha wananchi wao ardhi na kuwawezesha kuzalisha. Ujamaa wetu hapa Tanzania ulikuwa ni wa kumiliki kwa pamoja na faida ya mavuno kufaidisha wananchi wote.

Njia iliyotumika Malaysia ilifanikiwa, njia yetu, kwa sababu ya ufisadi na kukosekana uwajibikaji, haikufanikiwa.

Badala ya kuboresha kwa kujaribu njia ya kijamaa ya Malaysia tuliona ni bora kufuata njia ya kibepari ya kugawa ardhi hovyo kwa wakulima wakubwa na wachache, na kuwaacha wananchi wetu wakiwa mafukara kabisa!
 
Si ndo yale yale ya utalii
We fikiria Alikiba ndo mkulima
Inamana hakuna vijana wako serious na kilimo - Waliopitia kila changomoto ya kilimo - kutoka zero to hero?
Unadhani BBT inachukua hayo matoto yenu mliyoyafuga kama.kuku wa Kisasa? Inachukua Watoto wa maskini ambao wengi wamekulia kwenye mazingira ya Kilimo..

 
Makala ifuatayo kutoka The Chanzo inawatia Moyo wale waliothubutu kuleta mageuzi ya Kilimo Nchini Kupitia Mpango wa Vijana BBT.

Hapa Tanzania ukitaka kufanya jambo kubwa usiwasikilize loosers ambao hawana Msaada wowote licha ya maelezo yoa marefu ambayo hayana Tija.

Rais Samia na Bashe Songeni mbele ya hiyo Program ya BBT maana ndio itakuwa muarobaini wa kuondoa Umaskini na kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini kwetu.

Nchi ya Malaysia iligjaramia Kila kitu Kwa raia wake iloyowapa Ardhi na Sasa inavuna pesa tu.



Kilimo cha kufa na kupona, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza nk, hayo yote bado hayakufanya maendeleo ya kilimo, badala yake wakulima ndio kada masikini kabisa hapa nchini. Acheni utapeli wa kijinga.
 
Makala ifuatayo kutoka The Chanzo inawatia Moyo wale waliothubutu kuleta mageuzi ya Kilimo Nchini Kupitia Mpango wa Vijana BBT.

Hapa Tanzania ukitaka kufanya jambo kubwa usiwasikilize loosers ambao hawana Msaada wowote licha ya maelezo yoa marefu ambayo hayana Tija.

Rais Samia na Bashe Songeni mbele ya hiyo Program ya BBT maana ndio itakuwa muarobaini wa kuondoa Umaskini na kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini kwetu.

Nchi ya Malaysia iligjaramia Kila kitu Kwa raia wake iloyowapa Ardhi na Sasa inavuna pesa tu.


Usishabikie vitu usivyo vijua. Big Results Now iliishia wapi? Dkt Kikwete alikuwa na nia nzuri ila utekelezaji ukawa mbovu. Hata Bashe tunampongeza sema shida iko pahala. Tukiweza kutatua basi kama nchi tutapiga hatua kubwa
 
Kilimo cha kufa na kupona, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza nk, hayo yote bado hayakufanya maendeleo ya kilimo, badala yake wakulima ndio kada masikini kabisa hapa nchini. Acheni utapeli wa kijinga.
Hao wote hawakuwa serious,walau JK alianzisha ila Mwendazake akavuruga.

Samia is serious business na pesa kaweka sio maneno na Kauli mbinu.

Agenda 10/30 Strong Legacy here we go.
 
B
shabikie vitu usivyo vijua. Big Results Now iliishia wapi? Dkt Kikwete alikuwa na nia nzuri ila utekelezaji ukawa mbovu. Hata Bashe tunampongeza sema shida iko pahala. Tukiweza kutatua basi kama nchi tutapiga hatua kubwaig
Big results now ilihusu nini!?..kipi kinakuaminisha mradi wa kilimo utafeli!?
 
Si ndo yale yale ya utalii
We fikiria Alikiba ndo mkulima
Inamana hakuna vijana wako serious na kilimo - Waliopitia kila changomoto ya kilimo - kutoka zero to hero?
Nimeshangaa Ali Kiba kutumia kama mfano ili hali anaigiza, mbona Kuna watu maarufu wengi tu wanajulikana na wako mashambani Ina maana wameshindwa kuweka uhalisia? Kwakuwa wameanza na igizo basi mradi mzima utakuwa wa maigizo na matokeo yake yatakuwa mabaya sana
 
Kilimo cha kufa na kupona, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza nk, hayo yote bado hayakufanya maendeleo ya kilimo, badala yake wakulima ndio kada masikini kabisa hapa nchini. Acheni utapeli wa kijinga.
Ni kivipi kilimo kwanza ilifeli!?..una namba za kilimo kwanza?!
 
Usishabikie vitu usivyo vijua. Big Results Now iliishia wapi? Dkt Kikwete alikuwa na nia nzuri ila utekelezaji ukawa mbovu. Hata Bashe tunampongeza sema shida iko pahala. Tukiweza kutatua basi kama nchi tutapiga hatua kubwa
Big Result now ilikuwa ni Kilimo? JK alianzisha programu ya Kilimo kwanza na aliianza kabla ya Mwendazake kuvuruga..

Wewe Ukiwa looser na failure usidhani wote ni failure.Kilomo.kinahitaji.pesa na Samia kaweka pesa unadhani Bajeti ya Bil.950 uliwahi Iona wapi hapo kabla?
 
Back
Top Bottom