Wale mapacha walioungana wafariki Muhimbili!

Wale mapacha walioungana wafariki Muhimbili!

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,097
Watoto mapacha ambao walizaliwa mkoani Morogoro wakiwa wameungana maeneo ya tumboni wamefariki dunia ktk Hospitali ya Taifa Muhimbili walipokuwa wakisubiri matibabu na jaribio la kutenganishwa.

Haikuwa rizki!

=========================
Habari za awali kuhusu watoto hao;
=========================

Watoto mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana mkoani Morogoro imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhary alipokuwa akitoa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa takribani wiki nzima.

Daktari huyo amesema kuwa baada ya kufanya vipimo, imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha watoto hao mapacha.

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya pacha hao kupimwa vipimo vya radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray kipimo cha moyo (ECO) pamoja na vipimo vyote vya damu.

Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21 mwaka huu wamenaza kuchukuliwa vipimo mbalimbali vya awali kabla ya upasuaji huo.
 
si nilisikia kuwa wamefaulu vzur mthan Wa kidato cha sita?upasuaji umewasababishia umauti!!

mungu walaze mahala pema pepon!
 
Pole kwa wazazi,Mumtwishe Mungu fadhaa zenu,maana yeye hujishughulisha sana na mambo yetu.mpumzike kwa amani watoto wazuri.
 
si nilisikia kuwa wamefaulu vzur mthan Wa kidato cha sita?upasuaji umewasababishia umauti!!

mungu walaze mahala pema pepon!

Sio hao mkuu wale wamesha kuwa wakubwa ila kuna wengine wamezaliwa mkoa wa morogoro na niwadogo kabisa
 
habari kama hii inanitia uchungu mno,uwezekano wa kuwaokoa ulikuwepo why vipimo vimechukua muda mno ?huu ni uzembe someone amezembea hapa,why mpaka karne hii nchi yetu haina hospitali maalum kwa ajili ya watoto tuu,can any one tell me please may be iam missing something here?mbona wenzetu wameweza hapahapa Afrika kuwa na hospitali za watoto tuu,na uchelewesho huu pamoja na uzembe umechangiwa na foleni ya vipimo kuchukuliwa ,bila shaka vipimo vyao viliwekwa foleni moja na watu wazima,mtoto au watoto wanapofariki katika mazingira ambayo wangeweza kuokolewa huwa inaniuma mno,halafu utaona wanasiasa wanagongana kweny familia hii kujifanya wameguswa mno ,F*** and S***,poleni mno waliofiwa but nchi nyingine hawa viongozi wa hospitali hii wangekuwa na wakati mgumu wa kuelezea hili,but in our country they don't take a s***.
 
si nilisikia kuwa wamefaulu vzur mthan Wa kidato cha sita?upasuaji umewasababishia umauti!!

mungu walaze mahala pema pepon!
Siyo hao,hao ni watoto wachanga kabisa fuatilia habari kwa kina.
 
Mungu awalaze mahali pema pepon malaika hawa

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
nadhani ni vyema wamepumzika, roho ilikuwa inaniuma nikifikiria watakavyokua na kukua na kuzeeka
 
dah !nimeumia sana jaman!laleni pema matwin wenzangu!
 
Watoto mapacha ambao walizaliwa mkoani Morogoro wakiwa wameungana maeneo ya tumboni wamefariki dunia ktk Hospitali ya Taifa Muhimbili walipokuwa wakisubiri matibabu na jaribio la kutenganishwa.

Haikuwa rizki!

=========================
Habari za awali kuhusu watoto hao;
=========================

Watoto mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana mkoani Morogoro imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhary alipokuwa akitoa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa takribani wiki nzima.

Daktari huyo amesema kuwa baada ya kufanya vipimo, imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha watoto hao mapacha.

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya pacha hao kupimwa vipimo vya radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray kipimo cha moyo (ECO) pamoja na vipimo vyote vya damu.

Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21 mwaka huu wamenaza kuchukuliwa vipimo mbalimbali vya awali kabla ya upasuaji huo.


Napata shida kuelewa inakuaje watoto wafariki wakiwa katika hospital kubwa kama Muhimbili baada ya kuishi hapo kwa wiki moja ila wameweza kuishi hospital ya Wilaya kwa zaidi ya mwezi mzima.
 
Back
Top Bottom