Wale madaktari tiba mbadala enzi za Jakaya hivi sasa wapo wapi?

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,120
Ama hakika kila nabii na wakati wake na kizazi chake na watu wake.

Wakati wa uongozi wa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete tulishuhudia kuibuka kwa wimbi kubwa la watu au matabibu walikokuwa wakijinasibu kutibu watu magonjwa yao kwa njia mbadala ya miti shamba na TIBA lishe za mboga mboga za majani.

Wengi wao wakijiweka katika ku specialize magonjwa mbalimbali mpaka kufikia kujiita madaktari bingwa wa TIBA mbadala ikiwemo magonjwa sugu yasiambukiza, uzazi, wakina mama, watoto, vidonda vya tumbo na kadhalika

Ilikuwa haipiti dakika katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni bila ya kuona au kusikia matangazo ya hawa madaktari bingwa na wengine kufikia hadi kununua muda wa hewani na kutengeneza vipindi vya robo Saa,nusu au hata Saa nzima wakipigia porojo za TIBA zao.

Je, madaktari hawa hivi sasa wapo wapi?

Hii ni list tu ya Wale wachache ninao wakumbuka

Dr.ISAACK NDODI
Dr.JUMA J MWAKA
Dr.NG'WIZUKULU JILALA
Dr.MTAMBA NA MUNGU
Dr.RAHABU MWALUBAGO
Dr.TINDWA
Prof.MAJI MAREFU
Dr.MATUNGE
Dr.NGETWA

Na wengineo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kifo chake kilihusiana na kashifa ya utapeli kama sikosei.

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly.... Aliwazingua watu hko kusini
Unajua hakuna watu wanaamini ushirikina kama watu wa SA, ndomana Miaka ya nyuma kulikuwa na wimbi kubwa la waganga wanaenda hko kupiga Hela.....
Na syndicate yao ulikuwepo Uganda...
Huyo ngwizukulu alipozingua ndy Alikimbia hko
Ila inasemekana alitumiwa maninja....
Mwishowe ndy hivyooo.....

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom