Wale madaktari tiba mbadala enzi za Jakaya hivi sasa wapo wapi?

Wengi wao bado wapo, kilichofanyika ni kuwa, pamoja na kuweka utaratibu wa hao madaktari kufuata taratibu rasmi za usajiri wa kutoa huduma zao kutoka wizara ya afya, serikali pia ilizuia matangazo ya aina yoyote redioni na kwenye tv kama ilivyo kwa hospital za kawaida.

Hili la kuzuia matangazo ya huduma zao kwenye tv na redioni ndo limesababisha washindwe kusikika lakini jamaa bado wapo na wanatoa huduma kama kawaida, japo sio kwa kasi kubwa kama enzi za jakaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dokta ndodi alipiga hela za wajinga na akanenepeana kweli kweli baada ya hapo sijui alipotelea wapi na dokta mwaka pamoja na kuwa alitiwa jambajamba na kigwangalla lakini bado mbishi na yupo analiendeleza japo si kwa ile kasi ya mwanzo...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya kwanza uchunguzi kisha ndio ulete uzi
Umemtaja Dr tamba na Mungu kazi yake ni mnajimu wa nyota na mambo ya majini na pete
Sio tiba mbadala

Watu wa Tiba mbadala ni
Dr juma mwaka
Dr Abdallah mandai
Dr John Lupimo
Dr sigwa
hawa ndio watu wa Tiba mbadal
Na mm ni mdau wao nimeshawai kutibiwa sana

Kwa kutumia mkaa
Muharobaini
Mdarasini
Asali nyuki wadogo
Shubiri ( alovera
Tunda la avacado
Majani ya sanamaki
Mm nawakubari sana uwa wanatibu chanzo
Sio wanatibu presha wanatafuta chanzo cha presha wanazibiti hapo kwanza

Moyo hakuna operesheni
Wanatibu kwanza chanzo cha ugonjwa wa moyo
Nawakubari sana kwa kutibu magonjwa sugu kwa kutumia mitishamba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wao hawa hawana tofauti na babu wa Loliondo.
Fanya kwanza uchunguzi kisha ndio ulete uzi
Umemtaja Dr tamba na Mungu kazi yake ni mnajimu wa nyota na mambo ya majini na pete
Sio tiba mbadala

Watu wa Tiba mbadala ni
Dr juma mwaka
Dr Abdallah mandai
Dr John Lupimo
Dr sigwa
hawa ndio watu wa Tiba mbadal
Na mm ni mdau wao nimeshawai kutibiwa sana

Kwa kutumia mkaa
Muharobaini
Mdarasini
Asali nyuki wadogo
Shubiri ( alovera
Tunda la avacado
Majani ya sanamaki
Mm nawakubari sana uwa wanatibu chanzo
Sio wanatibu presha wanatafuta chanzo cha presha wanazibiti hapo kwanza

Moyo hakuna operesheni
Wanatibu kwanza chanzo cha ugonjwa wa moyo
Nawakubari sana kwa kutibu magonjwa sugu kwa kutumia mitishamba.


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameua sana watu nakumbuka Buguruni alikuwepo Dkt. Yoyo na Kimara kalikuwepo kadaktari fulani kanaitwa Benard ila kafa nae alishindwa kujihudumi...walikuwa wahuni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama hakika kila nabii na wakati wake na kizazi chake na watu wake.

Wakati wa uongozi wa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete tulishuhudia kuibuka kwa wimbi kubwa la watu au matabibu walikokuwa wakijinasibu kutibu watu magonjwa yao kwa njia mbadala ya miti shamba na TIBA lishe za mboga mboga za majani.

Wengi wao wakijiweka katika ku specialize magonjwa mbalimbali mpaka kufikia kujiita madaktari bingwa wa TIBA mbadala ikiwemo magonjwa sugu yasiambukiza, uzazi, wakina mama, watoto, vidonda vya tumbo na kadhalika

Ilikuwa haipiti dakika katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni bila ya kuona au kusikia matangazo ya hawa madaktari bingwa na wengine kufikia hadi kununua muda wa hewani na kutengeneza vipindi vya robo Saa,nusu au hata Saa nzima wakipigia porojo za TIBA zao.

Je, madaktari hawa hivi sasa wapo wapi?

Hii ni list tu ya Wale wachache ninao wakumbuka

Dr.ISAACK NDODI
Dr.JUMA J MWAKA
Dr.NG'WIZUKULU JILALA
Dr.MTAMBA NA MUNGU
Dr.RAHABU MWALUBAGO
Dr.TINDWA
Prof.MAJI MAREFU
Dr.MATUNGE
Dr.NGETWA

Na wengineo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo 'wapigaji' wapya
 
Back
Top Bottom