Walaji wa chips mitaani!!

Kumbe ndiyo sababu chips za Kiseke PPF ni tamu sana, kale ka harufu ka viatu ni kama roast ya utumbo.
 
Mkuu Dragoon,, hizi ni nzuri kama mamsap ndo kakutengenezea, yaani hapo zilipo mpaka nimemeza mate! Lakini hizi za kutengenezewa mitaani sitakula hata siku moja (over my dead body),, yaani nilichokiona jana hadi kinyaa [halafu likaanga chips lilivyo lijinga linaoshea viatu (YEBOYEBO) kwenye karai la chips na watu wanaliona]. Mkuu kama unakula hizi za stendi haki ya nani unalishwa vima (isomwe kutokea mwisho).
 
Ni hapa Msamvu yakopaki mabasi ya Nyehunge! Nilishindwa kukapiga picha maana kangegundua kwamba nimekaphotoa!

Ni vema kuwafatilia mkuu, mtu ni afya na asilimia kubwa ya watanzania huwa tunakula chips yaani haiepukiki ni vyema ukaonana na uongozi husika ili wafanye uchunguzi walipishwe faini hlf wazingatie usafi.
 
Si afadhali huyo alikuwa anaosha viatu kwenye karai ambalo mwisho lingewekwa jikoni kukaanga hizo chips.
Nilimuona muuza chips mmoja akichota ile marination ya mishikaki anaweka kwenye kachumbari
 
Walaji wa chips mitaani kazi mnayo! Kwa hiki nilichokiona kwa kweli ni kazi kweli kweli, kumbe hawa vijana wakimaliza kuuza chips wanaoshea viatu kwenye vyombo vya kupikia chips? Wauza chips na nyie hebu kuweni waungwana basi!

Na kuku...
 

Aiseeeeh.

Hivi vyakula vya kitaaa ni kujisahaulisha njaa ila wakati uo huo kukalibisha majanga!!

Utasikia, vijana katika stori zao, Mwana eeeh leo, nimekula, chips, kuku nusu na juice, viepe vilikuwa vitamu sana "

Daaaah, kumbe hapo ndipo kuku wanapotunzwa!?
😳😳😳
 
Watu tumeacha kula chips na vikuku visivyo na afya
 
Unadhani ni chips pekee? Je vyakula vingine kwa mama ntilie,? Nakuhakikishia ukichunguza kidogo tu namna vyakula vinavoandaliwa kwa mama ntilie, uoshaji wa vyombo nk hutakula.
 
Si afadhali huyo alikuwa anaosha viatu kwenye karai ambalo mwisho lingewekwa jikoni kukaanga hizo chips.
Nilimuona muuza chips mmoja akichota ile marination ya mishikaki anaweka kwenye kachumbari
Matination ndio nini?
 
Dah aisee njaa imenishika ghafla

😱😱😱😱

Duuuuuuh,.
Hakika, nimeamini kuwa tunatofautiana sana katika hii "Dunia ya Mungu' vitu vya mzungu koko!!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…