Walaji nguruwe watahadharishwa Dar

Kuntakinte

JF-Expert Member
May 26, 2007
701
30
2008-02-28 10:31:18
Na Joseph Mwendapole

Mkoa wa Dar es Salaam, umewatahadharisha wananchi dhidi ya ulaji wa nyama ya `kitimoto` kutokana na kuibuka kwa homa ya nguruwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni, ugonjwa huo hauna tiba wala chanjo.

Ilitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa kali, kushindwa kula, kuharisha na kutapika na kuvilia damu chini ya ngozi hususan sehemu za tumbo na miguu.

Ilitaja dalili zingine kuwa ni kupepesuka au kutetemeka, kupumua kwa shida, kutoa mapovu mdomoni, kukohoa na wakati mwingine kutoa machozi.

Taarifa hiyo ilisema kutokana na madhara na hasara kubwa za ugonjwa huo, halmashauri hizo zimepiga marufuku wafanyabiashara wa nguruwe kusafirisha ndani au nje ya Manispaa ya Ilala na Temeke nguruwe na mazao yake.

Mazao hayo ni nyama, mifupa, damu, soseji pamoja na mbolea.
``Hairuhisiwi kulisha nguruwe, mabaki ya nyama na mazao yake na hairuhusiwi kusafirisha nguruwe au mazao yake kutoka katika mashamba na maeneo yaliyoathirika na ugonjwa wa homa ya nguruwe bila kibali maalum kwa Daktari wa mifugo wa Manispaa husika,`` ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, ilisema wachinjaji wa nguruwe hawaruhusiwi kuchinja na kuuza nyama hiyo bila kibali cha Daktari wa mifugo wa manispaa husika.

Taarifa hiyo ilisema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayepuuza maagizo hayo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

SOURCE: Nipashe
 
Nilitaka kujua wangapi wamepoteza maisha au kuathirika kwa kula kitmotos. Ni nani huyu anayesema kitimotos wagonjwa mwislam au?

Kwa kifupi kila tuhuma dhidi ya kitimoto lazima ichunguzwe kwa makini isije wakaingiza itikadi zao za dini kuipiga vita.
 
Sasa kama imepita si iondolewe? Moderator unasubiri nini unataka wadau wa mnyama mkubwa washindwe kushiriki? Huu ugonjwa siku nyingi ushakuwa controlled wadau endeleeni kushiriki
 
Wakuu,

Umuhimu ni kujua ugonjwa upo na sio maswala ya tarehe... Is the
situation eradicated or controlled?
Kama ni controlled kama vile
klepto anasema basi the risk is still there and we should be on the
look out kuhusu maswala ya preparation of the Kitimotoz na mapishi yoyote mitaani.
Its an issue of hygiene!

Otherwise wakuu walaji,endeleeni kushiriki kitimotozz aste aste na ndizi za kukaanga!!!

Duh!!!..Bongo mwisho jamani!​
 
Swine Influenza (Flu)

Swine Influenza (swine flu) is a respiratory disease of pigs caused by type A influenza that regularly cause outbreaks of influenza among pigs. Swine flu viruses do not normally infect humans, however, human infections with swine flu do occur, and cases of human-to-human spread of swine flu viruses has been documented.

From December 2005 through February 2009, a total of 12 cases of human infection with swine influenza have been reported from 10 states in the U.S. Beginning in March 2009, a total of 5 laboratory confirmed human cases of swine influenza virus infection have been identified in California.

Source: www.cdc.gov/flu/swine

..... Pia soma hii link:

WEBMD NEWS ALERT - New Strain of SWINE
Thursday, April 23, 2009

SWINE Flu Case Count Rising

http://health.webmd.com/cgi-bin21/DM/y/e6wB0NO8gL0LTB0Bh2w0ER

The CDC is reporting five more cases of swine flu in California and
Texas separate from the two cases reported earlier this week. All
seven people cited by the scientists have recovered, but researchers
are saying this is a new type of swine flu that they've never seen
before.

Haya - kazi kwenu wala "kiti moto"!!
 
Hebu Wana JF Angalieni Ushahidi huu katika Qur-ani Mungu anasemaje Sura 5 Aya Ya 3

Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu

Sasa hiyo Nyama ya Nguruwe ni Haramu sio tu kwa Waislam hata kwa Wenzetu Wakristo imekatazwa na ndio Maana Mnapata Maradhi Ya kila aina kazi kwenu kwa Wala Nguruwe.

Kumbukumbu la Torati/ Chapter 14/8 8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse
 
Last edited:
Hakuna cha Kuraani hapa!

Mbona watu wengi tu wanakufa kwa malaria au mafua ya ndege??

Think beyond the box!
 
Hebu Wana JF Angalieni Ushahidi huu katika Qur-ani Mungu anasemaje Sura 5 Aya Ya 3
Sasa hiyo Nyama ya Nguruwe ni Haramu sio tu kwa Waislam hata kwa Wenzetu Wakristo imekatazwa na ndio Maana Mnapata Maradhi Ya kila aina kazi kwenu kwa Wala Nguruwe.

Na bird flue nao je? kuku ni haramu? Na TB ya kwenye ngo'mbe? Wanyama wengi wana magonjwa wala si kwa nguruwe tu.
 
MzalendoHalisi unasema hakuna cha Qur-ani Unasema mbona Watu wengi wanakufa kwa Malaria na Mafua ya ndege Umesahau kuwa Watu wengi Wanakufa Kwa Ukimwi? Na Ngoja kama haya Mengine ninayokwambia wewe sasa Angalia Mungu Anasemaje Katika Kitabu chake kitufu Qur-ani Sura 002 Aya ya 155 Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,

Unajuwa (Chembe ya Khofu?)Wasiwasi Wa Nchi kuwa na Vita nchi kwa nchi (Upungufu wa Mali) Unaona sasa Amerika ilivyoanguka Kiuchumi Sasa?Na Sio Tu Amerika Dunia zima sasa Uchumi wake upo Chini Hebu Angalia hapo Tanzania Tunaishi vipi? kama wanyama tu? na wanaofaidika ni Matajiri tu? Na (Upungufu wa Watu)Angalia dunia kila siku Watu wangapi wanakufa kwa Mafuriko kuanguka kwa ndege kUfa kwa Maradhi haswa Ukimwi na hapa kwetu Bongo Malaria ? Na Kitu cha Mwisho Mungu anasema Na (Matunda) Hebu wewe umesha angalia Mjomba wako Au babu yako au bibi alie mzaa mama yako au baba yako mkulima kwa kila mwaka Anavuna Mpunga au Mahindi Magunia mangapi? na alivyopanda na ndio anavyovuna? Jaribu kujiuliza wewe mwenyewe kisha ndio useme kuwa Tuiache Qur-ani Upo na mimi Mzalendohalisi? wewe una imani na Dini gani kwani wewe Mzalendo halisi?Unamjuwa Mungu lakini? Tujaribu kurudi kwake Mungu ili aache kutupa Mitihani hiyo ya kimaisha hiyo ndio Dalili ya mwisho wa dunia Asanteni wana JF Wenzangu.
 
Hebu Wana JF Angalieni Ushahidi huu katika Qur-ani Mungu anasemaje Sura 5 Aya Ya 3

Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu

Sasa hiyo Nyama ya Nguruwe ni Haramu sio tu kwa Waislam hata kwa Wenzetu Wakristo imekatazwa na ndio Maana Mnapata Maradhi Ya kila aina kazi kwenu kwa Wala Nguruwe.

Kumbukumbu la Torati/ Chapter 14/8 8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse

Kumbuka huyo nguruwe alipanda Safina. Ni hilo tu mjomba.
 
Torati iliandikwa kabla Yesu Kristo hajaja duniani, hakutoa maagizo ya kutokula visivyokua na kwato sisi ni "Wakristo" sio "Wamusa". You obviously have never tasted pork chops or bacon, you'd understand my love for the swine...
 
sasa why reference iwe Kuraani??

Duniani tuko over 6 bil. kila mtu ana ana imani yake! Kuna Wahindi, Makalasinga, Shintoism, wayahudi, Wakristo na Waislamu, wapagani n.k!

Think beyond the box zaidi ya dini ya mtu!
 
Mzizimkavu,

Kabla hujaenda mbali zaidi na ili tusikupuuze, tunakuomba uudhihirishie umma huu wa JF kwa ushahidi mwanana usio na shaka, ya kuwa Koran ni kitabu cha Mungu, baada ya hapo, at least, maybe utakuwa na hoja.
 
Torati iliandikwa kabla Yesu Kristo hajaja duniani, hakutoa maagizo ya kutokula visivyokua na kwato sisi ni "Wakristo" sio "Wamusa".

Mosi: Nkamangi inaelekea hata "Ukristo" haujui vizuri. Na je, "Amri 10 za Mungu" mbona alipewa Nabii Musa lakini Wakristo ndio mme-hijack as if it was Jesus who was given the Commandments??

Pili: Tuachane masuala ya dini na tujadili mada yangu. Mimi sikuwataja Wakristo ila nimewahatarisha "WALA KITI MOTO" - wawe wachina, wahindi, warusi ama waafrika bila kujali dini zao. Swali la kujiuliza ni "how serious is the swine flu or what steps should we Tanzanians take in the event it comes here?"

Over to U all .......
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom