Wala nchi wanateketeza Pesa Arusha kwa sasa

Wala nchi wanateketeza Pesa Arusha kwa sasa

Nipo hapa Arusha, kwa kifupi Viongozi wa Kitaifa wote wako hapa kuja kushuhudia Uzinduzi wa Filamu, Kuna V8 Zisizo kuwa na Idadi kwa sasa zimejaaa mji.

Hawa Viongozi wengine wako kwenye sekita ambazo hazona uhusiano hata kidogo na Utalii ila wamekua kutumia pesa za umma.

Mfano Mkuu wa Jeshi la Magereza na utaluu wapi na wapi?

Hawa wana teketeza pesa za walipa Kodi hapa Arusha huku kukiwa na watu wamelala vitandani wanakosa pesa za kwenda kutibia hata hapi Muhimbili tu.

Hawa watumbua pesa za Umma wata move tena kwenda Dar kutumbua tena pesa siku ya kuzindua Filam Dar, na huenda wa ka move wakaebda Zanzibar tena.

Billion of Money zinateketezwa hapa Arusha, wakati vijana kwa makumu 1000 hawana ajira baada ya kumaliza masomo vyuo vikuuu.

Hakuna kiongozi wa nchi hata mmoja anaye umia kuona vijana hasana kazi, Viongozi wanawaza wanatumbua vipi pesa za umma.

Huyu Chifu hana chembe ya Uchungu na raia wanao teseka katika nchi hii,
Una hoja ya msingi juu matumizi mabaya ya pesa. Rundo la viongozi wengi ni upotevu kiaiana.

ILA kusema magereza wanafanya nini? hapa sio sawa kila sector inahusika kwenye utalii, kumbuk magereza ni wazalishaji wazuri sana, wanaweza pia anzisha au ingia kutoa huduma ya utalii
 
Siku tukiweza kutengenaisha siasa na professional, siasa na majukumu tutapiga hatua sana.

Utakuta adi waziri wa tamisemi na timu yake ya watu 10 wameenda arusha kuweka kambi.
 
Uzinduzi wa Royal tour nje ya nchi nasimama na Hangaya 100%
Ila huu uzinduzi wa hapa Nchini na hizo ratiba sisimami nae.
Bora angeenda nchi nyingine akazindue tena kwa gharama hizi zinazotumika kuzindulia cc ambao bado tunapigana na kampeni ya Choo na Maji
 
Acheni hela zije mtaani acha kulialia, tafuta namna ya kuzikinga!!

Wewe wakati unalialia watu wanatafuta fursa kupitia hapo na kufaidika,

Wageni wanapokuja wengi, watalala kwa wingi kwenye nyumba za wageni, walioajiriwa watafaidika, watakula wenye migahawa watafaidika, chakula kwa wachuuzi wadogo wadogo sokoni watauza kwa wingi watapata, mkulima wa mboga mboga naye atauza kwa wingi, wafugaji watauza mifugo maana nyama zitaliwa pia, etc etc,
Hadi leo nashangaa huu uchumi wenzetu mnaousema wa sherehe kuleta pesa mtaani.

Uchumi hukua na pesa kuongezeka kwa nchi kuzalisha sana kupitia viwanda, kilimo na sekta nyingine.

Marekani au china Wana uchumi mkubwa na wananchi Wana pesa sio sababu wanafanya sherehe za watu kulala hotelini bali kwa kuzalisha.

Utofauti wa nchi maskini na nchi zilizoendelea ndio upo hapo
 
Back
Top Bottom