Wakuu wote wa Vitengo Uhamiaji kuondolewa na wengine kuhamishwa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga ameagiza yafanywe mabadiliko makubwa katika Vitengo mbalimbali vya Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.

Mheshimiwa Kitwanga ametoa maagizo hayo wakati alipofanya kikao na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katika kikao hicho, Mheshimiwa Kitwanga ameagiza watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji walioko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, wahamishwe na kupelekwa maeneo mengine nchini, wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Wengine watakaohamishwa ni kutoka Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati za Ukaazi na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Aidha ameagiza pia kuwa Wakuu wote wa Vitengo vya Upelelezi vya wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam, na pia wale wa Vituo vya Tunduma, Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, na pia watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika Vituo hivyo.

Amesema hatua hii inayochukuliwa sasa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.

Amesema katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa na wale wasiowajibika.

Amesema kufuatana na utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa matatizo ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji yanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni matumizi mabaya ya madaraka. Asilimia 15 inahusisha vitendea kazi wa mifumo hafifu ya kufanya kazi, asilimia 10 huduma mbovu na asilimia 5 ukabila na upendeleo.

Amewataka Viongozi na watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi na waepuke vitendo vya kupokea rushwa na kusaidia wahamiaji haramu na wauza madawa ya kulevya.

uha1.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini (kushoto) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.​

Kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Mwezi Januari 2016 nilitoa mada kuhusu madudu ya uhamiaji katika Mada/Thread hii;
Comment yangu ilikuwa hii;
Tatizo la wahamiaji haramu ni kubwa sana nchini!

Tatizo hili limeendelea kuwa kubwa kwa sababu ya kuoza kwa Idara ya uhamiaji.

Viongozi wakuu wa idara ya uhamiaji ni JIPU linalohitaji kupasuliwa kwa haraka!

Rushwa na uzembe katika Idara ya Uhamiaji imekuwa ni moja ya sehemu ya kazi zao.

Idara hii inahitaji kwanza kusafishwa kabla ya idara yenyewe kuwasafisha wahamiaji haramu.

Commissioner General of Immigration Services lazima awekwe kando ili kufanyike uchunguzi.

Kunatakiwa kufanyike Independent Inquiry ili kufahamu kwa nini kuna wahamiaji wengi wana Residence Permit Class A-C lakini kiuharisia hawana vigezo au hawakidhi matakwa yake.

Sina uhakika kama wahusika walinisikia/kunisoma, lakini ninashukuru yale yote ambayo nilipenda yafanywe na Waziri wa Mambo ya Ndani yalifanyika na yameendelea kufanyika.

Commissioner General of Immigration Services alitumbuliwa na sasa wakuu wa vitengo vya uhamiaji wako mbioni kutumbuliwa.

Hakuna jinsi lazima watumbuliwe kwa sababu wamekuwa ni jipu kubwa.

Foreigners walikuwa wanapata vibali vya Makazi na Uraia kama njugu!
 
Hawa jamaa hawana uzalendo kabisa bora wametumbuliwa. Wao mhabeshi na msomali wanamuona dili kuliko Mtanzania....

Nilishangaa juzi kati mkenya mmoja kaenda kuomba kibali cha kufanya kazi akawa recommended haraka sana eti kwa vile ana masters ya DS. Jamaa likasema ingekuwa digrii moja tusingempendekeza, wakati ukiangalia sheria haitamki popote habari za vyeti
 
Hawa jamaa hawana uzalendo kabisa bora wametumbuliwa. Wao mhabeshi na msomali wanamuona dili kuliko Mtanzania....

Nilishangaa juzi kati mkenya mmoja kaenda kuomba kibali cha kufanya kazi akawa recommended haraka sana eti kwa vile ana masters ya DS. Jamaa likasema ingekuwa digrii moja tusingempendekeza, wakati ukiangalia sheria haitamki popote habari za vyeti
Hawa maofisa uhamiaji wanakera sana.

Wamegeuza rushwa,uvivu na ubadhilifu wa mali za umma kuwa ni moja ya Utaratibu na kanuni zao za kazi.
 
Idara ya Uhamiaji ni kati ya idara nyeti sana kwa nchi yoyote. Hivyo uadilifu na uzalendo ni vitu muhimu sana. Idara hii imelegea sana hasa kipindi cha mkwere. Go go magufuli..
 
Bora wabadilishwe tu maana Pakistan na wahindi wanaingia kama chooni wanafanya kazi ambazo zipo ndani ya uwezo wawatanzania huku wakiruhusiwa kuendeleza ubaguzi na pia vibali vya makazi na ajira vikaguliwe
 
Idara ya Uhamiaji ni kati ya idara nyeti sana kwa nchi yoyote. Hivyo uadilifu na uzalendo ni vitu muhimu sana. Idara hii imelegea sana hasa kipindi cha mkwere. Go go magufuli..
Inahitaji kusukwa upya kuanzia chini mpaka mwenye cheo cha juu
 
Hivi nauliza uhamiaji wana data base?Yaani mgeni akiingilia Holili basi wa Ngara anajua,au makao makuu???
 
Bora wabadilishwe tu maana Pakistan na wahindi wanaingia kama chooni wanafanya kazi ambazo zipo ndani ya uwezo wawatanzania huku wakiruhusiwa kuendeleza ubaguzi na pia vibali vya makazi na ajira vikaguliwe
Absolutely
 
Back
Top Bottom