WAKUU WENZANGU KUNA DADA KATAKA HUU USHAURI NIMJIBU VIPI? NIPENI USHAURI WENU JAMANi

nimejikuta nacheka sana kusikia mpira katupiwa mama mwenye nyumba.
Kila kitu kinaonekana wazi otherwise huyo dada hataki kukubali ukweli, maamuzi yapo mikononi mwake.

kweli kabisa!mdada hataki kukubali ukweli!kwanza mwanaume muongo.pili si mwaminifu,tatu hamheshimu hata kidogo!yani nije kwako uniambie niondoke nirudi kesho?
 
"Nimekuta Chupi ya kike kwenye chumba cha Boyfriend wangu, yeye anadai hajui ilipotokea, Nifanyeje?".....Mdau


No body is guilty until proved.
Ushahidi ulioletwa kwenye jukwaa hili hautoshelezi kumtia mtuhumiwa hatiani kwa sababu kweli kuna 'Room for errors' kama vile inawezekana anachosema ndugu mtumuhiwa wa uzinzi ni kweli na hatujasikia utetezi wake kwa habari ya safari ya ghafla ya kikazi.
Hivyo nashauri uchunguzi zaidi kufanyika na ushahidi kuletwa mbele yetu tena
 
je aliporudi safarin alikuwa na begi?

Aseme aliposafiri alimwacha mshkaji ndo kachinjia njiwa wake humo gheton.

NB usijepeleka magendo ghetto.....utaabika siku si zako
 
kwa kifupi huwezi mshauri mtu aachane na mtu wake maana kama huyo jamaa bado ana nia ya kuendelea na kumuoa aimeze tu kisabuni iyo tukio akishaolewa labda ndo ahoji ili isijirudie lakini kumshauri waachane utaingia lawamani ya maisha yako yote maana anaweza asipate mwingine wa kumuoa hivi karibuni au akaangukia pabaya zaidi sasa ataanza kutafuta sababu kwa nn hakuendelea na yeye utakuta unaanza laumiwa!!!
 
hakuna aliye mwema , cha msingi asijipaize kwa hasira na kufanya maamuzi ya hasira. ampe nafasi zaidi na asemehe
 

huyo dada nae hamnazo
kila kitu kiko wazi asichoelewa ni nn
kwamba wana share?eti mama mwny nyumba
aamue yy kusuka au kunyoa coz huyo jamaa
sio muaminifu hta chembe!!ukiona manyoya ........!!
 
Urais-Tanzania-2015.jpg.jpg
 
wazee wetu zamani kule vijijini walikuwa na busara sana. Akirudi kutoka katika pilika zake au katika vijiwe vya wazee jioni utamsikia anaimba akiwa yungali mbali au hata kumwita mtoto wake mmojawapo bado yungali mbali na nyumba yake. Au kama alikwenda safari kidogo alirudi atakuja na chochote mkononi basi akikaribia kwake atampatia mtoto kile alichobeba ili ampelekee nyumbani wakati yeye akisalimiana na majirani. Hii ilikuwa ni kupeleka ujumbe kwa mkewe kwamba "mwenzio niko karibu, weka mazingira sawa, sitaki ugomvi usio wa lazima..."

Sasa wewe mchumba kakwambia nimesafiri ghafla, bado wewe wang'ang'ana kutaka kuhakiki hadi wakaa kwa mlango hadi usiku mwingi hata ukasinzia hapohapo mlangoni.....! Mchumba alikuwa na nia njema kusema kasafiri maana hakupenda kumuudhi demu wake ampendaye kwa sababu ya mpita njia wa siku moja....

Hapo hakuna ushauri ni yeye kutafakari mwenyewe na kuchukua hatua kulingana na moyo wake umtumavyo....
 
Ndoa yenyewe mpaka mwakani mwezi wa tisa, mbona atakoma na stress, hizo pete wengine wanavalishwaga tu lakini hakuna lolote, Mungu kinusuru hiki kizazi, sometime huwa nasema kuzini sio dhambi sana dhambi kubwa ni kuzini kwenye kitanda unacholala na mke/mme/mchumba wako, nikigundua hiki kitu sijui naweza chukua uamuzi gani. Mungu mwenyewe anajua, tushee mme na kitanda pia!
 
jamaaa kanifurahisha sana...inaelekea mama mwenye nyumba uchawi wake uko advance sana....

Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni vya nani,
itakuwa mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na bado anasisitiza eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa tisa.
 
"Nimekuta Chupi
ya kike kwenye chumba cha Boyfriend wangu, yeye anadai hajui ilipotokea,
Nifanyeje?".....Mdau





Wadau hapa
nilipo nimechanganyikiwa na nisijue cha kufanya, naombeni ushauri wenu,
nilikwenda field huko Tabora, nikamwacha mchumba wangu Tanga(ndiko
kwetu) tulikuwa tukiwasiliana kama kawaida, na niliondoka nikiwa
nimeshavishwa pete.



Nilipigiwa simu baba yangu ni mgonjwa sana, watoto
wake wote tulio mbali, tunatakiwa kurudi Tanga, basi nami nilirudi, na
kukuta kweli hali ya baba si nzuri, nikampigia simu mchumba wangu
kumuuliza yuko wapi, ili tukutane nae hospitali, akasema kwamba
amesafiri kikazi gafla kwa siku moja tu then kesho yake angegeuza,
nikamuuliza inakuwaje huniambii, akasema nimesafiri gafla, hata hivyo
nilitaka nikujulishe maana nimeondoka leo.





CBP1015764_P.jpg



Niliumia
sana kwa alichokifanya, sasa kuna rafiki yangu mmoja akaniambia, mbona
mimi nimemuona jana super market? Akiwa na msichana? Nilijisikia huzuni
sana ila nilijipa moyo



nilikwenda moja kwa moja hadi kwake, nikamkuta mtoto
wa mwenye nyumba, nikamuuliza kama kweli mchumba wangu
amesafiri,(nikajua labda alikwenda supermarket kununua vitu vya safari)
akasema mbona yupo? Na asubuhi nimemuona?, nikampigia simu kuwa nipo
pale kwake, akasema atachelewa sana kurudi, hivyo nirudi nyumbani kesho
ndio nije, nikamwambia namsubiri, ilifika saa sita mimi niko mlangoni
nimekaa namsubiri, aliponikuta nimesinzia mlangoni alishtuka sna, na
kuanza kunifokea kwanini nisingesubiri hadi kesho.



Ile naingia tu! Ndani, nikakutana na sandols za
kike, na kwenye mto kuna chupi ya kike, niliumia na kuanzisha ugomvi
mkubwa,



Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni
vya nani, itakuwa mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na
bado anasisitiza eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa
tisa.



Sasa mimi hata sijui nifanyaje, naombeni ushauri
wenu?


WAKUU WENZANGU HUYU MDADA ANATAKA NIMPE USHAURI JE MNASEMAJE NIMPE

USHAURI UPI MZURI? AACHANE NA MCHUMBA WAKE KWA SABABU AMEMSALITI?AU

AMSAMEHE? NINAWAOMBENI USHAURI WENU ASANTENI...............


aisee..mwiteni dokta manyaunyau awasaidie...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom