maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Zama za utawala wa chama kimoja hasa ule wa mwalimu, majeshi yalikuwa moja ya mkoa wa kichama, uliojulikana kama mkoa wa Majeshi na jeshi lilikuwa likijihusisha moja kwa moja na masuala ya siasa.
Baada ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi majeshi yote yalifutwa kujihusisha na siasa ili kulinda maadili ya kazi zao. Kuanzia hapo ushirikishwaji wa wanajeshi katika mambo ya kisiasa ulisitishwa.
Kwa kawaida, siku zote tumezoea wakuu wa wilaya wakiteuliwa kutoka miongoni mwa makada wa chama kinachotawala, mimi binafsi na baadhi ya wengi tumeshindwa kuelewa na ningependa nieleweshwe sheria na utaratibu uliotumika kuwapa ukuu wa wilaya majenerali hao maana sidhani kama walikuwa makada wa CCM vinginevyo hata sisi tusiokuwa wanachama wa chama chochote tuna haki ya kuuliza tuzingatiwe katika uteuzi kama huu maana nasi tu watanzania.