Wakuu wa mikoa ya bara na fiesta, RC Dsm Makonda akaribia kukabidhi ofisi za walimu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Juzi kupitia luminga ya channel ilionekana kamati inayosimamia ujenzi wa ofisi za walimu Dsm ilikabidhiwa mabati 80,000 kwa ajili ya kuezeka ofisi za walimu ambao ni ubunifu wa RC Makonda.

Na jana radio ya Magic fm iliripoti taarifa ya watanzania waishio Marekani wakichangia samani za ofisini zikiwemo meza za umeme, viti, kabati za vitabu na mazagazaga mengine kibao vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya USD 800,000 ambayo ni karibia sh bilioni 2 za kitanzania.

Kwa maana hiyo tutegemee ofisi za walimu kukamilika na kukabidhiwa mapema kuliko ilivyotarajiwa. Naomba mwenye updates za mafanikio ya fiesta - fursa kuanzia sokoni huko bara atujuze, hapa ktk jiji la Makonda akisaidiana na UKAWA tunaisubiri hiyo fiesta maana hapa ndio sokoni penyewe demand inapo exist!!
 
Hizo ofisi ataenda kukaa nani? Maana wale waratibu elimu kata waliokuwa wanapewa posho ya laki mbili na nusu waliondolewa cheo kisa laki mbioi unusu, anataka ukiwa kiongoI uwajibike na kamshahara kako hako hako, sasa nani atakubali kuwa na cheo cha makaratasi
 
Wa mikoani wao wala hawana hata creativity za maana ndo kisa hawana vitu vikubwa vya kuibua kwa kasi wakavisimamia na vikalipa. Na ndio maana utaona watu wanatetea ule wehu wa ma DED waliotumbuliwa juzi Bukoba wakati wenzao Dar kuamshwa na kujibu ni kitu cha kawaida sana. Makonda ameweza kupanda mbegu ya kujituma, kujiamini na kujiongeza kwa watumishi wa Dar kitu ambacho kiukweli kinawalipa wanaoguswa katika maeneo yao.

Na hapa mleta uzi unazodolewa si kwassbabu hawajakuelewa ila ni kwasababu inamhusu mchapakazi na mbunifu Makonda ambaye wavivu, wenye husda na roho za kwanini inawauma sana. Mafanikio yake ndo vidonda vyao na sasa vimegeuka vidonda ndugu, haviponi hata kwa sayansi za kuzimu
 
Back
Top Bottom