Wakuu wa mikoa wamemdanganya Mh Rais juu ya watumishi hewa!

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
843
Wanaboard nina uhakika kuwa sehemu kubwa ya taarifa iliyowasilishwa kwa Rais ya watumishi hewa haina uhalisia wowote, wengi wao wamewasilisha taarifa ya mezani bila kujilidhisha. Mfano kuna halmashauri mojawapo ijapokuwa taarifa imeshawasilishwa bado mpaka sasa watumishi wanaendelea kufika kuhakikiwa. Pia taarifa ya mkoa Dar hiyo ndiyo ninauhakika nayo haina usahihi!, kama kweli we are serious na hili swala ili kujua uhalisia na ukubwa watatizo hebu taasisi zenye uwezo wa kutupa uhalisia zimusaidie Mh Rais, zingie Dar na Njombe kupata angalau picha ya nini kilichofanyika kitaifa juu ya zoezi zima maana taarifa zilizopo wengi wa viongozi waliotekeleza agizo la Mheshimiwa wameogopa kutoa uhalisia ili wasitumbuliwa jipu!.
 
ukiwa likizo siku boss kaja ofsini unaonekana hewa ukiwa likizo ya masomo unaonekana hewa kama unalikizo la ugonjwa ndio kabisa na hr alivyomuoga kwa mkuu wa mkoa anakua mnyonge
 
Hiyo wala haishangazi. Kuna njia nyingi za kufanikisha jambo. unaweza kutumia vitisho, au unaweza kuweka mikakati kuhakikisha unafanikisha unalotaka kufanikisha, bila kuwafanya hao unaowaagiza wajisikie woga, bali wachape kazi inavyotakiwa, kwa uhuru na kujiamini. ni muhimu pia, kama ulivyogusia, kutumia taasisi husika, zenye mamlaka katika eneo husika. sidhani kama mkuu wa mkoa ana mamlaka juu ya taasisi zote zilizoko katika mkoa wake.
 
Mkuu kwani hiyo taarifa iliyotolewa si walisema ni ya awali!! Au mimi ndio sikuilewa??
 
Nina uhakika, walimu wengi walioko masomoni, wengi wao waajiri huwakataza kwenda masomoni, mpaka walimu wanaamua kwenda masomoni bila ruhusa. Hii imetokea halmashauri nyingi, baada ya waajiri kuwaahidi walimu waendelee kuvumilia kituoni hadi miaka 5, lkni kwenda kusoma waajiri hawawapi ruhusa na hivyo kuamua kujiondokea. Hivyo naamini, wapo wengi ambao wataitwa hewa, lkni si hewa kama wananchi wanavyoelewa. Maafisa utumishi waache uoga
 
Kutaja idadi ya wafanyakazi hewa bila kuwakamata waliokuwa wanalamba hizo hela ni kazi bure. Lazima wahusika wajulikane
 
Nina uhakika, walimu wengi walioko masomoni, wengi wao waajiri huwakataza kwenda masomoni, mpaka walimu wanaamua kwenda masomoni bila ruhusa. Hii imetokea halmashauri nyingi, baada ya waajiri kuwaahidi walimu waendelee kuvumilia kituoni hadi miaka 5, lkni kwenda kusoma waajiri hawawapi ruhusa na hivyo kuamua kujiondokea. Hivyo naamini, wapo wengi ambao wataitwa hewa, lkni si hewa kama wananchi wanavyoelewa. Maafisa utumishi waache uoga
Nina wasi wasi hata kwa mkoa wa Mwanza ni takwimu za uwongo.Napendekeza waliotoa takwimu hizo iwe ni kwa uoga ama uzembe watumbuliwe.Maana hatuwezi kuwa na maafisa wasio makini kiasi hiki.Mshahara hulipwa bank,kama ni hewa,mbona ni rahisi kuwabana wahusika?Hii inaonesha wakuu wa idara ni wazembe kupita kiasi.Kwa kweli haikubaliki hata kidogo kutoa takwimu za uongo.Wawajibishwe kuanzia mkuu wa mkoa,wilaya,wakurugenzi na wakuu wa idara wote walioshiriki uzembe huu.
 
Mheshimiwa magufuli awaulize tena, je kwenye hao hewa walimu walioondoka kwenda masomoni bila ruhusa ni wangapi na ni kwa nini?? Ukifatilia, utakuta mkuu wa shule ana diploma, sasa anaona huyu mwalimu mwenye diploma akienda kusoma digrii anahisi labda akirudi atachukua ukuu wa shule. So, hata muda wa mwalimu kujiendeleza umefika, utaona mkuu wa shule kila siku lazima aende kwa DEO kupeleka uongo. "pale mwaka huu nina upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi" sa Ole wako mwalimu upeleke barua yako ya ruhusa kwa DEO. Utazunguka halmashauri mpaka viatu viishie
 
ukiwa likizo siku boss kaja ofsini unaonekana hewa ukiwa likizo ya masomo unaonekana hewa kama unalikizo la ugonjwa ndio kabisa na hr alivyomuoga kwa mkuu wa mkoa anakua mnyonge
ki ukweli watumishi hewa wapo , lakini sio wengi kiivyo, mi nafikiri serikali itafunguliwa kesi nyingi kuhusu hili suala
 
Yaani kuna mtumishi mmoja nasikia alipewa barua ya kuhamia kwenye kata na mkurugenzi, yeye akasema elimu yake hastaili kukaa kimya wenye kata. Hivyo, yeye pia hakuhakikiwa na ni mtumishi hewa. Huu ni mwaka wa sarakasi, hakika tutaona mengi.
 
Pawepo na utaratibu utakaonesha mfanyakazi yupo kazini na anaonekana kila mwezi,akitoweka kwa namna yoyote taarifa zifike haraka zinakohitajika ili mshahara usitolewe.
 
Back
Top Bottom