Wakuu wa mikoa simamieni mipango miji

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,480
4,161
Ningependa wa kuu wa mikoa wakisaidiana na RAS, DC, DED na Watu wa mipango miji kuwa na mipango endelevu ya kupanga miji, kusimamia public places Kama open spaces, sehemu za wapita kwa miguu na kuendeleza sehemu za Biashara.

Mfano pale Mwenge ilipokuwa stendi ya mabasi sasa hivi pamevamiwa na wauza mitumba na biashara za kila aina, na sehemu Kati ya ITV na Mwenge magereji ya kutengeneza magari nk

Ukija Mwenge ipande wa ya Sam Nujoma karibu na Equity bank na Halotel office magari yana park kwenye eneo la watembea kwa miguu, na wauza Mbao nao wanaweka mbao kwenye eneo la watembeao kwa miguu

Ukija majengo opposite na kijiji cha Makumbusho waliojenga upande wa kulia Kama unatoka mjini kwenda Mwenge kuna Watu wametengeneza parking kwenye eneo la public na kuyahodhi maeneo hayo ka sehemu binafsi na maeneo mengine wenye sehemu karibu na barabara wameongeza maeneo yao kwa kuweka biashara zao kiasi kwamba watembea kwa miguu inabidi kupita kwenye barabara za magari.
 
Back
Top Bottom