Wakuu ushauri wenu katika changamoto ya kuendesha gari

Shukrani mkuu,sasa hizo gear za manual huwa wanaziweka za nini?

Huwa mara zote ni ili kumpa mteja Flavor zote kwa pamoja. Kwani kuna watu wanapenda tu manual kwaajili ya kufanya maneuvers , wakati watu wengine wanapenda Auto kwasababu unaendesha gari kwa utulivu na unaConcetrate zaidi na Steering na barabara badala ya kuwa bize na gia
 
Kwa hiyo auto ina uwezo wa kulitoa gari katika kikwazo chochote kile kama vile matope,utelezi,makorongo,vilima na kadhalika?
 
Kwa hiyo auto ina uwezo wa kulitoa gari katika kikwazo chochote kile kama vile matope,utelezi,makorongo,vilima na kadhalika?
Ndio.

Chukulia mfano gari yako ni 4-Speed AUTO.
Unapoanza kuondoka Automatically inaanza na gia no. 1 yenyewe.

Unapoendelea kwenda na kukanyaga mafuta inapandisha Gia kwenda gia no.2,....3.....4 yenyewe.

Unapokuwa kwenye mlima basi kulingana na mwendo wa gari ,mwinuko na ukinzani uliopo, gari lenyewe litashusha gia na kuweka gia yenye nguvu kama vile gia no. 2 au no. 1 ambayo ndio L.

Kwenye Tope, unapokuwa unakanyaga mafuta taratibu basi gari lenyewe litaendelea na gia ya kwanza (L) ambayo ndio gia yenye nguvu pia.
 
Shukrani mkuu!
 
D ni gia Salama kabisa ambayo Gari inajipangia kupandisha ama kushusha Gia yenyewe kulingana na Mwinuko na Mwendokasi. Usiwaze kabisa.

Kwenye mteremko mrefu ambao unahitaji kushikilia brake kwa muda mrefu bila kuachilia, unashauriwa kutumia gia ndogo kama vile D3 au D2 ili kuLimit speed (kwa kutumia Engine Braking) na kuepusha brake pads kuOver Heat na kuisha ovyo.
Gari yake haina D2 wala D3. Kuna D na option ya 'manual' which is really semi automatic
 
Shukrani mkuu,sasa hizo gear za manual huwa wanaziweka za nini?

Kaka mm nilijua unajua kutumia, kama hujui usiende kujifunzia huko milimani maana utajikuta umeweka gari Neutral ukaporomoka.

Kimsingi unasogeza kirungu huko pembe na kazi yako ni kupush kwe + au - lakini pia Gia hiyo bado ipo automatic

Usitegemee gari ikiwa imesemama ukaset gia namba 3 au 4 na zaidi, kuingia kwa gia kunategemea na Acceleration ya Gari. nina Gari yenye mfumo huo ni RAV 4 Miss TZ gia 7 inanibariki sana.

Pia ustegemee gari ipo spid kubwa lets say 100 af ww unataka uingize gia 1 kamwe haitakubali, Itaingia kwenye 5 au 6 na utatakiwa kuzishusha huku ikipiga brake au kuachia mafuta
 
Nyingi tuu hazina, na nyingine badala ya M +/- zina S +/- kwa mm nimeona gari za kuanzia 2001 ndio baadhi zinazo
Hivi mkuu S ni sawa na M?Kazi ya S ni nini?Ukiweka M pale kwenye dashboard huwa panaanza na gear namba moja by default,sasa ukiweka S pale kwenye dashboard huwa panaanza na gear namba ngapi?
 
Hivi mkuu S ni sawa na M?Kazi ya S ni nini?Ukiweka M pale kwenye dashboard huwa panaanza na gear namba moja by default,sasa ukiweka S pale kwenye dashboard huwa panaanza na gear namba ngapi?
S ni Sport mode...ukitaka ligi na mtu unamuwekea hio. Gari inakuwa sporty kiaina. Gear ni zile zile.
 
Maelezo muafaka kabisa 👍🏽
1. Ndio. Weka D kisha cheza na steringi, wese na breki, ukifika weka P.

2. Hakuna madhara yoyote.

Mzungu alivyoweka, ni kwamba penye kuhitaji gear ndogo gari itaweka gear ndogo penye gear kubwa itaweka kubwa.

Hizo Manual ni fancy mtu akipenda kucontrol gari lakini haita maanisha kwamba ndio ya kupanda mlima au bonde.

We control speed tu. Usikimbizane kama mashindano maana umesema wewe sio mzoefu.
 
Back
Top Bottom