Wakuu tushauliane hili suala

Wakuu tushauliane hili suala

Steven Robert Masatu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2009
Posts
2,458
Reaction score
1,826
HAPPY PEOPLE!!
Heri ya weekend na Happy JF party.

Wakuu nina kitu naomba tusaidiane kutoa ushauri. Naomba tusome taratibu ili tuelewe hasa kinachoongelewa.

Kuna mdada mmoja ni mpenzi wa rafiki yangu toka kitambo sana anaitwa NUSRA na jamaa anaitwa JOHN, kwa sasa wanamiaka 8 kwenye mahusiano yao. Hiyo miaka 8 wameifikia katika hali ngumu na nzuri, katika kupotezana bila taarifa na bila mawasiliano yoyoyte, (yani wanaweza wakakaa kimya hata miezi miwili bila hata kutumiana japo sms),wote wapo hapa Dar es salaam kila mmoja ameajiriwa sehemu tofauti.

Katika hali hiyo ya mapenz ya kupotezana na kutafutana na kukumbushia enzi, kuna issue ya utata ilitokea miaka mitano iliyopita. Issue hiyo ni kwamba miaka mitano iliyopita jamaa JOHN aliamua kufunga Ndoa ya kanisani na mdada mwingine tofauti, baada ya ndoa jamaa alikata mawasiliano kwa yule mdada NUSRA kwa muda wa mwaka mmoja, JOHN akiheshimu ndoa yake.Yule dada NUSRA alipoona JOHN yupo kimya sana ikabidi naye atafute jamaa mwingineaitwae RAMA, Sasa jamaa JOHN ikatokea wakarudiana tena kisirisiri na yule mpenzi wa awali(NUSRA) wakawa wanakutana kwa yule mdada NUSRA alipopanga(anapoishi mdada) na kufanya mambo yao jamaa anarudi home kwake kwa mke wake wa ndoa.

Miaka miwili iliyopita ukatokea mvurugano mkubwa katika familia ya JOHN ambayo ikasababisha hao wanandoa kutengana kila mmoja akiishi kivyake. Jamaa alienda kupanga na mke alirudi kwao hadi sasa.

JOHN katika kukaa mpweke na maisha mapya ya usingle huku akiendeleza mapenzi na yule mdada(NUSRA) wa awali kimya kimya bila kumjulisha kwamba alishafunga ndoa na sasa hivi wametengana na mke wake.

Last week jamaa kaenda kwa huyo mdada NUSRA bila taarifa yoyote akakuta kuna kidume(RAMA) ndani, jamaa kiroho safi akaondoka bila bughudha wala fujo akarudi kwake. Baadaye yule mdada akamtafuta mshikaji wayamalize kikubwa, sasa mdada ikabidi amueleze jamaa ukweli kwamba yule jamaa uliyemkuta ndani siku ile nipo naye huu mwaka wa sita sasa,nimekuwa naye baada ya kuona wewe upo kimya sana halafu hueleweki msimamo wako ( kumbuka awali nilisema walikuwa wanakaa kimya hata miezi miwili hadi mine bila mawasiliano)vile vile mie nakupenda wewe jamaa RAMA simtaki ila ananilazimisha tuu, naomba unisamehe mie nakupenda sana. Na kuanzia leo nakuwa na wewe tuu .

JOHN akatafakari kwa kina na kugundua ni makosa yake aliyafanya ya kuamua kumtelekeza yule mdada NUSRA kwa kipindi kirefu. Jamaa yangu JOHN akaridhika akamsamehe mdada yakaisha.

Jamaa naye ikabidi amueleze mdada NUSRA ukweli kwamba katika hicho kipindi alichokuwa kimya aliwahi kufunga ndoa na mdada mwingine ila kwa sasa wametengana, yule dada NUSRA akashtuka sana, ila jamaa akaomba msamaha na kumuahidi yeye anampemda na yupo tayari waishi wote kama mume na mke.

Sasa kilichomfanya aje tushauriane cha kufanya ni hivi, juzi jamaa kapata cash kidogo akaamua amtoe yule mdada NUSRA wakapate tusker kidogo( huo ndo ulikuwa mtoko wao wa kwanza katika kipindi chote cha miaka 8 ya mahusiano yao ya kuungaunga na superglue).

Wamepiga gambe kwa sana then wakashauriana waende kulala kwa mdada NUSRA, imefika usiku mkali simu ya mdada ikaanza kuita jamaa akapokea kikajitambulisha kidume (RAMA) naomba kuongea na mwenye simu, JOHN akasema amelala mpigie asubuhi then akakata simu.

JOHN akamuasha mdada na kumuuliza huyu ni nani anapiga simu usiku huu? Mdada akajibu ni jamaa uliyemkuta hapa ndani siku ile (RAMA). Jamaa akapotezea wakalala, asubuhi sana saa kumi na mbili kile kidume kingine kikatia timu kwa mdada na kubisha na kujitambulisha kabisa me Fulani fungua mlango, mdada akaenda kufungua mlango wakawa wanaongea baadaye yule jamaa akaondoka. Rafiki yangu ikabidi amhoji mdada ni nani huyo asubuhi yote hii mdada akamweleza jamaa ukweli kwamba ni jamaa(RAMA) yule aliyepiga simu jana usiku ndo kaja.

Rafiki yangu ikabidi arudi kwake kwanza kutafakari nini cha kufanya, Huku akimueleza yule mdada yeye anampenda sana na hawezi kumuacha, sasa amemwambia mdada NUSRA aende kwa akina mama watu wazima wenye hekima na busara awaelezee mazingira yote bila kuficha kitu wala kupunguza ili apate ushauri wa kuchagua ni mwanaume yupi atayemfaa kuwa naye (kati yake yeye ambaye alishawahi kufunga ndoa na kutengana au jamaa RAMA ambaye hampendi na wala hawana mipango yoyote ya kimaisha).

Sasa kaja kwangu kuomba ushauri afanye nini na jamaa JOHN anampenda mdada NUSRA, mwezi wa pili huu alikuwa amepanga amvute waishi wote rasmi kama mke na mume. Wote wapo njia panda jamaa hajui afanye nini? Wamekubaliana waonane next week huku wakiwa na majibu muafaka.

Wakuu naomba tusaidiane mawazo katika hili suala.

Cc watu8 Mtambuzi
 
Hapo hakuna mwenye penzi la dhati kwa mwenzie si john wala huyo nusra
HAWATAISHI WAKADUMU mtu alioa baada ya kuachana na mke wake ndo amuone mdada wa watu kipozoe cha maumivu aliyoyapata baada ya ndoa kuvunjika USALITI WA HALI YA JUU

Hapo kila mtu anatakiwa aanze maisha yake kila mtu atapata mwenza anaemstahili kuendelea kung'ang'aniana ni kukaribisha majanga huko mbele
wote wamepoteza sifa ya uaminifu

Huyo mdada nae hajitambui MIAKA NANE mwanaume anazama na kuibuka hata hafanyi uchunguzi nini kinaendelea
 
Kwa mdada nilijaribu kuongea naye jana kwa simu alinambia naye anampenda sana JOHN sababu ndo mwanamume wake anayeona anamlidhisha na kujiskia raha sana anapokuwa karibu yake, kiufupi anasema anampenda sana.

Miss neddy unaongeleaje upande wa pili kwa huyu RAMA.?
 
WAFUNGE NDOA TU
sometimes watu huja ku fall na wenza wao baadae
baada ya kuishi nao mda mrefu...

hawa wafunge ndoa tu kwanza

Kaka The Boss unachoongea ndicho nami nilimueleza JOHN, wote kwa pamoja wafunge tuu ndoa ili mambo yasonge, lakini rafiki yangu JOHN anakuwa na mashaka ushauri wangu,anasema sie ambao hatujaoa hatuwezi toa wazo zuri katika ndoa, sasa naye kaenda kutafuta wazee wenye busara zadi.

Halafu hivi kikristo inaruhusiwa kufunga ndoa tena kwa mara ya pili?
 
Kaka The Boss unachoongea ndicho nami nilimueleza JOHN wote kwa pamoja wafunge tuu ndoa ili mambo yasonge, lakini rafiki yangu JOHN anakuwa na mashaka ushauri wangu,anasema sie amabao hatujaona hatuwezi toa wazo zuri katika ndoa, sasa naye kaenda kutafuta wazee wenye busara zadi.

Halafu hivi kikristo inaruhusiwa kufunga ndoa tena kwa mara ya pili?

hapo shughuli ipo
 
Haya...nadhan ni watu wazimu ina maana wanajua kilicho sawa kati yao lakn..true love waits bhn..yani hatimaye wamepatana tn, ni sawa tu muhimu wapendane
 
hizi style hiz ndo zinaanza kushika kasi kwa sasa bongo.....sijui kuna nn.....ubongo hautumiki kabisa kwenye baadhi ya mahusiano siku izi... hamna mapenz hapo kwa wote ila kuna 'sintofahamu',,,kuna hatari mbeleni,,,,,,mdada hana msimamo,,mkaka nae hatumii ubongo saaana
 
kwanza ipi hali ya ndoa ya John na mke wake? Wametengana tu ama na talaka ishatolewa mahakaman?
 
kwanza ipi hali ya ndoa ya John na mke wake? Wametengana tu ama na talaka ishatolewa mahakaman?

Hali ya ndoa ya John kwa kweli bado tete talaka haijatolewa mahakamani hadi sasa.

Wasiwasi wa Nusra aliniuliza John kama ikijatikea akarudiana na mkewe itakuwaje kwa upande wake asije jikuta anapoteza muda wake tuu. Sasa ndo maana tena anaona hata kama RAMA hana msimamo wa kimaisha yani haujali future full gambe kila siku na hampendi kutoka moyoni, aende kwa RAMA aachane na John au atake risk kwa John.
 
Mkuu kwa uwazi kabisa bila kumung'unya maneno naomba nikueleze kuwa ni ngumu mno kumshauri mzinzi au muasherati suala la ndoa...

Kama mimi ningefuatwa na John na kuombwa ushauri, kwa uwazi kabisa ningemueleza amrejelee mkewe baaaasi.
hebu kula like elfu nane mia nane
 
Hali ya ndoa ya John kwa kweli bado tete talaka haijatolewa mahakamani hadi sasa.

Wasiwasi wa Nusra aliniuliza John kama ikijatikea akarudiana na mkewe itakuwaje kwa upande wake asije jikuta anapoteza muda wake tuu. Sasa ndo maana tena anaona hata kama RAMA hana msimamo wa kimaisha yani haujali future full gambe kila siku na hampendi kutoka moyoni, aende kwa RAMA aachane na John au atake risk kwa John.

ha ha ha haaaa...bi dada anapoteza muda wake kwa huyo john tu...
yani huyu hajamuacha anataka kuoa mwingine.!? mmmmmmmh sitaki kuamini kama kidini yake inaluusiwa.....
ndio maana yakusema wakufa na kuzikana,vipi yeye john hakusema....!?
 
Kaka watu8 kwa hali ilivyo wale wanandoa ni ngumu sana kurudiana sababu kipindi cha nyuma tulishwahi kumsihi John arudiane na mkewe lakini tulipata upinzani mkubwa sana. Kitu kingine mkewe John hawaelewani na ndugu wa John sababu mke wa John aliwahi kumfungia mlango dada yake John siku hiyo alichelewa kurudi kutoka kazini kipindi hicho John akiwa amesafiri kikazi mikoani, ikapidi ampangie dada yake hotel kwa muda. Na wazazi wake John nao hawaposupportive katika kutafuta suruhu kila kitu kaachiwa John aamue mwenyewe. Kiufupi pande zote za wazaz hawajawahi hata kuitisha kikao kusuruhisha iyo ndoa.
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha haaaa...bi dada anapoteza muda wake kwa huyo john tu...
yani huyu hajamuacha anataka kuoa mwingine.!? mmmmmmmh sitaki kuamini kama kidini yake inaluusiwa.....
ndio maana yakusema wakufa na kuzikana,vipi yeye john hakusema....!?

Kidini nahisi hairuhusiwi, Mkuu unashauri Nusra aende kwa RAMA ambaye hajaoa wayamalize then waanze taratibu zingine?
 
hayo ya ndugu yanasolvika mkuu cha muhimu huyo ni mke wa john na c wa familia!!!!!!!!!!!!
well said bna hyo!!!!!!!!!!!
Kaka watu8 kwa hali ilivyo wale wanandoa ni ngumu sana kurudiana sababu kipindi cha nyuma tulishwahi kumsihi John arudiane na mkewe lakini tulipata upinzani mkubwa sana. Kitu kingine mkewe John hawaelewani na ndugu wa John sababu mke wa John aliwahi kumfungia mlango dada yake John siku hiyo alichelewa kurudi kutoka kazini kipindi hicho John akiwa amesafiri kikazi mikoani, ikapidi ampangie dada yake hotel kwa muda. Na wazazi wake John nao hawaposupportive katika kutafuta suruhu kila kitu kaachiwa John aamue mwenyewe. Kiufupi pande zote za wazaz hawajawahi hata kuitisha kikao kusuruhisha iyo ndoa.
 
Hali ya ndoa ya John kwa kweli bado tete talaka haijatolewa mahakamani hadi sasa.

Wasiwasi wa Nusra aliniuliza John kama ikijatikea akarudiana na mkewe itakuwaje kwa upande wake asije jikuta anapoteza muda wake tuu. Sasa ndo maana tena anaona hata kama RAMA hana msimamo wa kimaisha yani haujali future full gambe kila siku na hampendi kutoka moyoni, aende kwa RAMA aachane na John au atake risk kwa John.

kwa wakristo, hakuna ndoa juu ya ndoa
 
Back
Top Bottom