Wakuu naombeni ushauri wenu

Wakuu naombeni ushauri wenu

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
311
Reaction score
335
Habari za asubuhi.

Kwa kweli nimefikia katika hatua ngumu sana katika mahusiano yangu (japo huenda isiwe sahihi kwa mimi kuita ni mahusiano kutokana na hali iliopo hivi sasa.

Ishu yenyewe iko hivi, Hapo katikati ya mwaka nilikutana na mwanamke mmoja katika mazingira fulani na kiukweli baada ya mazungumzo kadhaa nilimpenda sana, basi tukabadilishana namba tukaanza kuwasiliana, baada ya mawasiliano kwa muda fulani tukaanza mahusiano ya kimapenzi ambayo mwanzoni yalikwenda vizuri tu.

Lakini changamoto ikaanza kujitokeza, pale nilipogundua yeye ni mtu mwenye wivu sana au naweza sema hana imani sana nami kwakuwa alianza kukasirikia mambo madogo madogo sana kwa mfano akinipigia simu akaona inatumika lazima ataanza kuuliza kwa ugomvi, akiona niko nae nikawa najibu sms basi anakasirika anahisi nachati na mwanamke mwingine. Kuna siku moja nilimfanyia surprise anakokaa nikampigia simu nikiwa stand lakini kwa sababu sikumwambia ukweli kuwa ningekuja siku hiyo ili nimsurprise akaanza kunihisi labda nimetoka kwa mwanamke mwingine mpaka nilipomuelewesha akaelewa akanyamaza

Sasa kisanga kimetokea juzi tumekutana zetu baa kunywa supu ya samaki. Mara ya kwanza tumepiga stori vizuri tu na tukaongelea mambo mbalimbali, baada ya muda hamu ya sex ikampata akanambia anataka nikamwambia hapa tuko bar subiri kwanza tukitoka. Hakunielewa akaanza kunikalia mapajani, nikamwacha alipoanza kunilalia akiwa amekaa mapajani nikamwambia kaa kwenye siti yako tukitoka tutakwenda ku-do. Nilipomwambia hivyo alikubali ila ALIKASIRIKA SANA, kwa hasira akanambia lete simu yako niikague, akaanza kuikagua akakagua sms za kawaida akaona hamna chochote cha kunikamatisha.

Akataka kukagua na whatsapp, nikamwambia whatsapp hapana. Kiukweli nilikataa si kwa sababu nilikuwa na mwanamke mwingine, la hasha, nilikataa kwa sababu sikufuta sms za whatsapp za ma X wangu(mimi ni mvivu kufuta sms za whatsapp) hivyo niliogopa ikiwa angeziona na kwa jinsi nilivyomjua asingenielewa hivyo nilikataa yeye kukagua sms za whatsapp akawa anang'ang'ania nikamnyang'anya simu akawa anang'ang'ania tena huku akiniambia 'usiponiachia nikague simu yako basi jua mi na we ndo basi', nikamnyang'anya akaondoka kwa hasira. Kujaribu kumfata sikumuona.

Baadae nikaanza kumpigia simu ikawa inaita hapokei alivoona kero akaniblock, nikapiga kwa namba ingine alipogundua kuwa ni mimi akaikata na hakupokea tena. Nikamfata anapoishi nilopofika mlangoni alipogundua kuwa ni mimi akafunga mlango kwa ndani halafu KIMYA. Tangu hapo akawa hataki mawasiliano nami, nikaja nikampigia kwa namba ingine akapokea akanambia 'sitaki mahusiano nawewe' akakata nikapiga tena akapokea akasema 'sitaki hata mawasiliano na wewe na tukionana kila mtu kimpango wake, endelea na wanawake zako.'

Sasa ndugu zangu huko ni KUACHWA, kinachoniumiza ni kuwa naamini sina kosa na kwa kweli sina/sikuwa na mwanamke yeyote zaidi yake. Na mie bado NAMPENDA SANA TENA SANA, mpaka nimefikia hatua hii ya kuleta hapa sina la kufanya kwa kuwa hapokei simu yangu wala hataki mazungumzo nami na wala simjui ndugu yake yeyote ningemjua ningemwomba anisaidie kwa kweli kwa sababu nampenda sana, tulipanga tufunge ndoa mwakani 2020.

Na tulikuwa tunapanga maswala ya kutambulishana. Sasa naombeni mnishauri nifanyeje ndugu zangu kwa kuwa mie inaniuma sana nimejaribu kumwambia kuwa nili kataa asikague simu yangu kwa sababu hangeamini ambacho ningemwambia lakini hakunielewa.

Mnisamehe kwa kuandika maneno mengi sana kwa sababu nilitaka kueleza kila kitu.

Naomba mnishauri wakuu.
 
Kwanza polee...

Ila mkuu hao ma ex zako tangu mmeachana ni mda,sasa inakuaje useme hujafuta sms zao WhatsApp? Hivi inawezekanaje kukaa na masms ya ex zako? Hapa kuna kitu umetuficha na wahuni tushajua

Pili, huyo bibie kama unataka kumuoa basi ukubali tu mapungufu yake otherwise utaona ana kukera...Wivu ukizidi kila siku mtagombana

Mwisho mwache uyo bibie hata wiki moja au mbili zipite apoe hasira zake...ni ngumu kutaka akusikilize saiz na wakati umesha mtibua na ukizingatia ana kisirani sana uyo mwananke..mpe muda apoee kisha nenda kwake mkayamalize..

Akigoma,achana nae mkuu,hawa viumbe pasua kichwa...Kama hakupendi tena ,mwambie wanao bado Tunakupenda..
 
Yan hizo ni indicators za kukuonesha kua hakutaki na alikua anatafta sababu kwako kisa tu ameshajua unampenda vibaya baya

Ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni, ni hivi hebu fanya mambo yako inauma lakini ona kama Mungu anakuepusha na kikombe kisicho chako mkuu, wewe kaa kimya usimtafte huko kuhangaika kwako ndio mana unaumia bure waswahili wana msemo wao ukiachwa achika huna namna, hujamuoa hali ni hiyo ukimuoa itakuaje?
 
Unaonekana kwenye game la mapenzi bado underground..mabaharia hua hatujitosi mazima kwenye mapenzi..mana mwisho wa mapenzi ya dhati na maumivu na chuki...kimsingi hutakiwi kupenda mademu wa kibongo..pia kosa kubwa kuwa na demu mmoja..eti kisa mapenzi ya dhati...
 
Unaonekana kwenye game la mapenzi bado underground..mabaharia hua hatujitosi mazima kwenye mapenzi..mana mwisho wa mapenzi ya dhati na maumivu na chuki...kimsingi hutakiwi kupenda mademu wa kibongo..pia kosa kubwa kuwa na demu mmoja..eti kisa mapenzi ya dhati...

Umeongea ukweli kabisa. Yaani full experience hapo. Hongera kwa kutambua kuwa mwanamke hapendwi
 
Stori za kitoto.
Yan hizo ni indicators za kukuonesha kua hakutaki na alikua anatafta sababu kwako kisa tu ameshajua unampenda vibaya baya

Ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni, ni hivi hebu fanya mambo yako inauma lakini ona kama Mungu anakuepusha na kikombe kisicho chako mkuu, wewe kaa kimya usimtafte huko kuhangaika kwako ndio mana unaumia bure waswahili wana msemo wao ukiachwa achika huna namna, hujamuoa hali ni hiyo ukimuoa itakuaje?
 
Umeshaona tabia zake then unataka kumuoa r u serious dude kosea kujenga sio kuoa Cha kufanya hapo kula bati do ur thing mpaka ashangae kwann umtafuti ye SI ana wivu ukikaa kimya ndo ataona umepata mwingine kabisa mwisho wa siku atakutafuta mwenyewe
 
Umeshaona tabia zake then unataka kumuoa r u serious dude kosea kujenga sio kuoa Cha kufanya hapo kula bati do ur thing mpaka ashangae kwann umtafuti ye SI ana wivu ukikaa kimya ndo ataona umepata mwingine kabisa mwisho wa siku atakutafuta mwenyewe
Ukweli mchungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom