Wakuu naombeni ushauri juu ya course ya Environmental Engineering


Sasa kaka tofauti kati ya environmental science na environmental engineering ni ipi
 
Sasa kaka tofauti kati ya environmental science na environmental engineering ni ipi
Mtu wa Environmental science hawezi fanya kazi za Environmental Engineer, kwa maana nyingine mmoja ni mhandisi wa mazingira mwingine ni mwanasayansi wa mazingira

Mfano tunataka kuimplement mradi Waste stabilization Pond, yaani tunaanza from scratch yaani planning, design mpaka ujenzi mtu wa Environmental science anaweza shiriki kwenye part ya maabara tu ( sample analysis )

But kwa Environmental Engineer atashiriki kuanzia mwanzo mpaka yaani planning, design mpka ujenzi
 
Wakuu kuna mtu anauliza vipi mtu aliye soma CBG anaweza kusoma EE...?
 
Wakuu kuna mtu anauliza vipi mtu aliye soma CBG anaweza kusoma EE...?
Kigezo ni uwe umesoma advanced physics na advanced maths. Kama kama kwenye cbg unasoma hayo masomo basi unaweza soma env engineering otherwise kasome env science.
 
Hiyo kozi sio ya maana sana kwa sasa. Utateseka kuisoma na utaishia kutafuta ajira kwa ugumu sana baada ya kumaliza shule. Mwisho wa yote ni vigumu kuweza kujiajiri. Kwa Tanzania bado sana kuitambua umuhimu wake.

Kama unaweza kwenda kusoma Civil Engineering au Electrical Engineering litakuwa ni jambo bora sana, tena maradufu. Ni kozi zinazojiuza zenyewe.
 
Dogo UDOM wameanzisha EE 2016, Ardhi EE ipo tangu miaka ya 90.

EE ya ardhi miaka 4, EE ya UDOM miaka 3.

Vitu vingi UDOM hawasomi mfano mambo ya workshop hawana wale jamaa.
Acha uongo, hakuna Kozi ya Engineering ya miaka mi3 kwa mujibu wa muongozo wa TCU. EE Udom ni miaka mi4 na benchmarking ya kozi ya EE iliyoanza UDOM mwaka 2015 imerandana na ya Ardhi kwa zaidi ya 90% na kama sikosei kuna wahadhiri wengi wa Ardhi wanaofanya part-time lecturing pale UDOM (I stand to be corrected). Kuhusu Workshops si anaweza kujifunza wakati wa field akiwa attached sehemu kama VETA?

Usimchanganye mwenzio binafsi naona kotekote sawa tu.
 
wakuu CBG anaweza kusoma Enviromental Egeneering
Usipoteze muda wako utafeli mwaka wa kwanza tu. Soma Environmental Science (ES). Bila kuwa na basics za physics ya advance utapata tabu sana. PCB yes but not CBG
 
Usipoteze muda wako utafeli mwaka wa kwanza tu. Soma Environmental Science (ES). Bila kuwa na basics za physics ya advance utapata tabu sana. PCB yes but not CBG
hakuna linaloshindikana as longer unapambana hakuna kigumu
 
Surveyor yupi? Quantity surveyor au land surveyor kama land surveyor usimdanganye land survey ni pana kuliko unavyofikiria wengi wenu mnadhani land survey ni levelling na setting out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…