Wakuu move linaendelea....

Wakuu move linaendelea....

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
3,367
Reaction score
4,072
MAMBO 10 KUHUSU PRESS YA IGP SIRRO.

1. Ukimtizama usoni kama una just elementary knowledge ya Psychology utagundua kuwa hakuwa anamaanisha anayoongea. Maneno ya kinywa chake na lugha ya mwili wake vilipingana kabisa.

2. Picha aliyoonesha Sirro sio ya CCTV. Ni picha tu ya kuokota mtaani ambayo probably imepigwa kwa simu.

3. Kama ni cctv kwanini haina footage? Kwanini haina tarehe wala muda wa tukio?

4. Na kuanzia lini cctv camera inapiga picha horizontal kama za kuweka instagram? Cctv footage must be aerial kwa sababu camera za cctv hazikai sakafuni, huwa zinatundikwa juu. Tizama hata zile za Bashite akivamia Clouds.

5. Awali polisi walisema CCTV zilishindwa kudetect tukio hilo. Lakini leo Sirro anasema Cctv zilionesha hadi keepleft cha Kawe. Why contradiction? Hizo zilizoshindwa kudetect mwanzoni ni zipi, na hizo zilizoonesha hadi keepleft cha Kawe ni zipi?

6. Gari iliyooneshwa na Sirro inaonekana imepaki nyumbani kwa mtu, hapo sio Collesium Hotel.

7. Gari hiyo ina pancha tairi moja na imepigwa jeki. Je wahalifu waliziba kwanza pancha then wakapiga kwanza selfie gari yao ndipo wakambeba MO?

8. Hizo plate number ni za Msumbiji lakini taarifa za TRA zinaonesha hakuna gari yenye namba hizo iliyotoka Msumbiji na kuingia Tanzania tarehe 1 September. Sirro ametudanganya.

9. Inaweza kuwa hizo ni namba za Bodaboda ama Bajaj za Tanzania zimegeuzwa.

10. Kama polisi wameona gari hiyo hadi keepleft cha Kawe na hawajui ilipoenda, kwanini wasiruhusu wachunguzi wa kimataifa ambao watatumia satelite kujua uelekeo wa gari hiyo kutokea hapo keepleft?

Tusubiri kesho watakuja na move lipi....
 
Move-Movie

Natafuta vidio ya Sirro nimzoom maana nilikuwa machungani wakati akipress mubashara...
 
Hapa wenye IQ 100000 ndo wataelewa wengie. Wote chenga tupu
 
Sijafanikiwa bado kukutana na arifa inayohusu hii press but kama ni kweli,basi itakuwa ni zaidi ya movie la kihindi yale wanayoanza kucheza cheza kwenye miti mirefu huku mvua ikiwanyeshea.
 
Kamanda Siro is among the best in case you know any, tuaminiane tushirikiane kwa upendo kwa ajili ya ndugu yetu Mo
 
Kamanda Siro is among the best in case you know any, tuaminiane tushirikiane kwa upendo kwa ajili ya ndugu yetu Mo
Probably he Is among the best ila kujiingiza kwenye siasa ndiyo kumemharibu yeye na jeshi zima.
 
Kamanda Siro is among the best in case you know any, tuaminiane tushirikiane kwa upendo kwa ajili ya ndugu yetu Mo
Vipi alishajua Azory Gwanda yupo wapi, Alishahitimisha swala la Lissu? Akiweza hayo ataaminika ila kama amefeli basi hakuna huo ubest unaousema
 
Sawa kunaweza kuwa na hoja nyingi tu ila hili laweza jibu zote ngoja tuonee mwisho wake tuombe heri tu liishe mapema zaidi Castr &Lyamber
 
Gari iliyooneshwa na Sirro inaonekana imepaki nyumbani kwa mtu, hapo sio Collesium Hotel.

7. Gari hiyo ina pancha tairi moja na imepigwa jeki. Je wahalifu waliziba kwanza pancha then wakapiga kwanza selfie gari yao ndipo wakambeba MO?

Wewe!! Khaa! Nnani kakuambia ukayachunguze hayo yote?? Huoni tairi zilivyo kwisha?? Tupige dua tu MO asidhurike au ipatikane lift ya kumrudisha ka alifanikiwa kufika mpakani. Hiyo gari haiwezi mrudisha hapa dar.
 
Back
Top Bottom