Wakuu hii ndio yenyewe kabisaaaaaa

Duh! umenikumbusha mbali saaana tulikua tunaenda kuoga mtoni ndio yalikua maisha, asubuhi fasta unaenda unadumbikia unaoga unarudi, jioni ukitoka tena vile vile nikahamia boarding Magamba boys (sio CCM pls) now Sebastian Kolowa University College, huko nako kulikua na kajimto tunaenda tunapata maji then tunajianika kwenye mawe, watoto wa Mazinde Juu sio furaha hio wakipita kwenda Oaklands!!!! Asante mkuu umenikumbusha mbali saaaana, tulikua weusi usiseme, baridi ilikua kali sana na maji ya baridi sana
 
Ole wako sasa uwe hujajivua gamba, hapo hutaweza kuoga! Hapo ni wanaume halisi tu! Mambo ya wembe tulikua tunamalizia hapo hapo tena sometimes tuna share (usijaribu siku hizi mambo siyo) tulikua tunatumia topaz au shanghai
 
hizi zitakuwa pande za kwetu kanda ya ziwa, hasa ukerewe tumezoea mambo haya. tulikuwa tukipiga mbizi na walimu, baba wadogo, wajomba na kadhalika/ ila age ya hawa watoto sisi tulikuwa tukioga upande wa wamama. zidumu mila zetu!! msituponde. ndo raha ya kukulia kanda ya ziwa bwana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom