Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Wakuu wa idara watatu wa idara za ujenzi,maji na barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ujiji wamesimamishwa kazi na kuamriwa kufunguliwa mashtaka baada ya kutuhumiwa kuhusika katika upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni moja nukta tatu za miradi ya maendeleo zilizotolewa na serikali.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha dharura cha baraza wa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ujiji bada ya kupokea ripoti ya mkaguzi wa ndani ambapo meya wa Manispaa ya Kigoma ujiji Hussein Ruhava amesema fedha hizo zimepotea katika kipindi cha mwaka 2013 hadi 2016 ambapo baadhi ya watendaji wa manispaa hiyo wamekuwa wakijihusisha na ubadhirifu
Mapema akitoa taarifa ya kamati ya maadili katibu wa baraza la madiwani Mussa Hamad amesema uchunguzi umebaini upotevu katika miradi ya maji,barabara,afya na manunuzi ambapo maafisa kadhaa wamehusishwa na wanatakiwa kufungulkiwa mashtaka huku madiwani wakiomba kibali cha kufanyika ukaguzi maalum.
Chanzo: ITV