Wakurugenzi wanne wafutiwa kesi

Wakurugenzi wanne wafutiwa kesi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
vigogo+pic.jpg
​

DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imezifuta kesi mbili zinazowakabili wakurugezi watendaji wa kampuni ya ENCC Consultants, Riziki Shemdoe na Deusdedit Kibassa wa Abshir Gure na Farhiya Warsame wa kampuni ya Lasar Logistic Limited.

Wakurugenzi hao na wenzao walifikishwa mahakamani na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Hakimu mfawidhi, Victoria Nongwa amezifuta kesi hizo kwa nyakati tofauti baada ya mawakili wa Serikali waliokuwa wakiziendesha, Dereck Mukabatunzi na Emma Msofe kuomba zifutwe.

Amesema ombi hilo ni kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yao, hivyo mahakama imeridhia na kuwaachia.

Pia, wadhamini wao watakuwa huru na kuendelea na shughuli zao.


Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom