Wakulima wananyonywa Halmashauri zakosa Ushuru

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,302
6,115
Vyombo vya serikali na mamla husika chukueni hatua

Mimi ni mdau mkubwa kwenye zao la ufuta na nimekuwa nafuatilia sana zao hili kwa muda sasa. kwanza nianze kwa msimu uliopita. Mwaka jana kiasi cha ufuta kilichouzwa nje ya nchi ni tani 139,200+ sawa na kilo 139,200,000. kutoka kwenye halmashauri kari 33 nchini zinazolima zao hilo kwa wingi hapa nchini zikiongozwa na na za Mkoa wa Lindi.

Takwimu zilizopo (kutokana na ushuru uliolipwa) ni Tani 77.3 hivi maana yake zaidi ya tani 62,000 hazikulipiwa ushuru wa mazao tukitumia kadirio la chini kabisa la TZS 70 kwa kilo zilikwepwa jumla ya 4.34 billion hazikulipwa na ni Kampuni sita tu zilizokuwa zinauza nje. takwimu zipo TRA na kwenye vitabu vya halmashauri msimu uliopita.

Msimu mpya umeanza

Mosi: Wakulima Lindi na Pwani wananyonywa na wanunuzi wadogo hasa wanatumia mizani zisizo halali kwa utafiti mdogo niliofanya wiki iliyopita na wiki hii kwa kila wanapopandisha mzigo kwenye mizani mkulima anaibiwa kati ya kilo 5 - 11 (Bungu, Kibiti, Ikwiriri, muhuro, Kilwa, Ngarambe, Mtama, etc) nimepitia kote huko na kujionea.

OMBI: Mamlaka ya Vipimo na Halmashauri za Wilaya tumeni task force kwenye maeneo yaho kuwanusuru wakulima na janga hilo.

Pili: Ukwepaji Ushuru wanunuzi hao hao wanaonunua kwa kutumia mizani mbovu ndio wanaongoza kwa kukwepa vizuizi vya kulipia ushuru kwa kutumia pikipiki na hata malori walimopakia ufuta. wanapakia ufuta kwenye magari wanasubiri hadi giza liingie ndio wanaondoka wakifika kwenye mageti ya ushuru wanadeclare kiasi ambacho sicho kwa mujibu wa mzigo waliobeba.

Mfano kwenye mizani kilwa fuso ilikua imesoma 6.73tons wanati net weight ya gari 2.25tons mzigo uliokuwa declared kwenye form ya malipo ya ushuru ni 2.5 tons hivyo kuwa na utofauti wa approx. 2tons ambazo kwa lugha ingine hazijalipiwa ushuru.

Pili kuna vijana wa boda boda kuanzia saa tatu usiku kwanzia Kimanzichana wanabeba hadi 600 - 800kg (viroba 6 - 8) kwenye pikipiki kuvusha kwenye vizuizi vya ushuru.

Ikwiriri, Kibiti, Kimanzichana na mwandege haijafahamika wanalipwa vijana hao kiasi gani lakini uchunguzi binafsi unaendelea; Halmashauri za wilaya fanyeni msako kwanza muwatambue wanunuzi wote kwenye wilaya zenu, kisha fuatilieni nyendo zao wakati wa ununuzi na usafirishaji mtaokoa kiasi kikubwa cha ukwepaji ushuru

Mawakala wa ushuru (sina hakika) lakini inawezekana wanashirikiana na wanunuzi hao kukwepa ushuru na ndio maana wanafanya nyakati za usiku kuficha kuonekana.

Hivyo vyombo vya mamlaka zifuatilie nyendo za mawakala hao kote nchini hasa kipindi hiki cha uuzaji ufuta. aidha kuna baadhi ya watu muda wote wanaonekana kuranda randa vituoni hapo na kuongea na mawakala hao (hii imetupa hofu kwamba hao ndio wanaotumika kuwasiliana na wafanyabiashara) hivyo vyomba vya uchunguzi navyo vimulike watu hao

Wakulima mbali na kudanganywa kwenye mizani pia wamekuwa wakitishwa kwamba msimu huu mavuno ni mengi hivyo pia itakuwa chini na kunununua kwa bai za chini baadhi ya maeneo yaliyo mbali na barabara kuu (Kilwa Road). wafanya biashara wa aina hii wamulikwe pia

Tatu kama sehemu ya uwajibikaji wa makampuni yenye kujihusisha na biashara ya ununuzi na usafirishaji wa zao la ufuta (kama ilivyo kwenye sheria ya makampuni, masharti ya leseni, TIN, VAT waliyopewa makampuni hayo) uhakikikishe kila lory linalopeleka ufuta kwenye maghala yao wanaonyesha stakabadhi ya ushuru inayolingana na kiasi cha ufuta wanachoshusha kwenye maghala yao. Hii itapunguza ujanja ujanja unafanywa na wanunuzi hao

Serikali kuu: Iwalazimishe makampuni (ikiwekana pamoja na fine) wawajibike kulipa kiasi chote cha ushuru ambao haukukusanywa kwenye halmashauri either kwa uzembe wa halmashauri ama ukwepaji kama nilivyoeleza hapo juu.


Mtu atahoji nafanya haya kwa maslahi gani

Kwanza zao la ufuta ni zao ambalo kwa sasa linaonekana kuwa na tija kwa mkulima na ni mdau mkubwa kwenye sector ya kilimo (Agri business Devel. Consultant) Na tumetaka kujikita support sector hiyo (oil seeds crops) hivyo tumeona ni fursa tukatoa yale tumeyaona kwa sasa ambayo yakifuatiliwa kwa karibu sana sector hii itapata mafanikio makubwa.

Pili ukiangalia zao husika kwa mtiririko wa Value chain kwa kuanzia kwa mzalishaji mbegu hadi mlaji mkulima ndio mwenye pato dogo kuliko wote wakati ndio mtu muhimu kuliko wote anapata TZS 364,000 kama faida ghafi wakati dalali kwa msimu mmoja anapata hadi 3.4million kwa kipindi kisichozidi wiki sita. Dalali hana mtaji (mtaji anapewa na wanunuzi kutoka Dar ambapo kwa kila kg moja anapewa TZS100 kama commission)

Tatu ni kuunga mkono serikali kuu juhudi za kukusanya mapato ambayo kama halmashauri zikikusanya fedha nzuri zinaweza kuboresha mazingira ya wakulima hao (20% inayotakiwa kurudi kwenye eneo la uzalishaji).

Hivyo kama mtanzania nimefanya kazi yangu, na jukumu la vyombo husika kufanya kazi zao lakini pia nitaendelea kutoa taarifa kadiri zinavyopatikana.

UFUTA UNAWEZA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO WA KAYA KAMA WAKULIMA WAKILINDWA
 
Back
Top Bottom