Wakulima wagomea bei ya Korosho

Wakulima wagomea bei ya Korosho

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,768
Mshtuko umewakuta wakulima baada ya Kuletewa bei ya Tsh 1680 kabla ya makato ambapo baada ya makato huenda mkulima ikamfikia 1380, Zoezi hilo la mauzo ya Korosho liliendeshwa wilayani Tandahimba katika kijiji cha Mitondi.

Wakulima wamegomea bei hiyo hivyo korosho hazijauzwa leo.
 
Korosho na Bibo msimu wa 2022 / 2023


Bodi ya Korosho Tanzania yatoa maelekezo kwa wakulima wa Korosho uvunaji ufuate mbinu bora.

KIKAO CHA SITA CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA​

October 20, 202261
3Q3B1869-1-960x640.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce Damian Mwanjile ndc ameongoza kikao cha Bodi ya Wakurugenzi tarehe 19 Oktoba 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Tanzania kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu Mtwara.

Menejimenti imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazigo ya kikao kilichopita, taarifa ya utekelezaji wa robo ya kwanza, mipango ya utekelezaji kwa robo ya pili ya mwaka 2022/2023.


Pia Bodi imepitia utekelezaji wa maagizo ya viongozi yaliyotolewa huko nyuma ikiwa ni pamoja na maandalizi ya msimu wa mauzo ya korosho ya mwaka 2022/2023.

Akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti amesisitiza kuongeza ufanisi katika kutekeleza shughuli zilizopangwa na kupitishwa ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti ameipongeza Menejimenti kwa uwajibikaji mzuri katika kutimiza majukumu yao ya kazi.

1666358274325.png

Source : habari na picha kwa hisani kubwa ya Bodi ya Korosho Tanzania KIKAO CHA SITA CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA - Bodi Ya Korosho Tanzania


TOKA MAKTABA : 27 December 2019

Mwaka 2019 ulivyotingisha sekta ya korosho Tanzania​


Dar es Salaam. Sekta ya korosho nchini inaendelea kuuguza madhara ya matukio ya msimu wa 2018/19 wakati Serikali iliponunua tani 222,000 kati ya tani 225,000 za korosho zilizozalishwa nchini.

Hatua hiyo ilichukuliwa na Serikali ili kulinda maslahi ya wakulima baada ya wanunuzi kutoa bei ndogo katika minada ya awali, hali iliyotafsiriwa kuwa ni mpango wa kutaka kuwanyonya wakulima.
Uamuzi wa kununua korosho hizo ulitangazwa Novemba 2, 2018 na Rais John Magufuli na kuiagiza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali kununua korosho zote kwa bei ya Sh3,300 kwa kilo
 

8 October 2022​

Dodoma, Tanzania

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATOA MWONGOZO WA USIMAMIZI WA MASOKO NA MAUZO​


BODI ya Korosho Tanzania ikishirikiana na Bodi ya Usimamizi wa stakabadhi za ghala na Tume ya Maendeleo ya Ushirika zimeandaa na kutoa Mwongozo wa Pamoja wa Usimamizi wa Masoko na Mauzo ya korosho ghafi kwa msimu 2022/2023.

Hayo yalisemwa leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred Wakati qkitoa taarifa ya utekekezaji wa Shughuli za bodi hiyo kwa mwaka 2021/2022.

Alisema Bodi ya Korosho imetoa miongozo mingine ambayo ni mwongozo wa usimamizi na udhibiti ubora wa korosho pamoja na Mwongozo wa upatikanaji wa korosho ghafi kwa wabanguaji wa ndani kupitia soko la awali kwa msimu 2022/2023.

" Miongozo yote mitatu tayari imesambazwa kwa Sekretarieti za Mikoa, Vyama vikuu vya Ushirika, Waendesha ghala, wanunuzi na wadau wengine katika mnyororo wa zao la korosho. Aidha miongozo hii inapatikana katika tovuti ya Bodi ya korosho ambayo ni www.cashew.go.tz,"alisema

Na kuongeza "Bodi tayari imeanza kusajili na kutoa leseni kwa wanunuzi wa korosho ghafi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na kubangua nchini ambapo hadi kufikia tarehe 07 Oktoba, 2022, jumla ya kampuni 48 zimejisajili na kati yake, kampuni 18 tayari zimepata leseni na zilizosalia zipo katika hatua mbalimbali za kukamilisha upataji wa leseni," Alisema Mkurugenzi huyo.

Alibainisha kwa Upande wa minada ya mauzo ya korosho inatarajia kuanza tarehe 14 Oktoba, 2022 kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Aidha bodi inatoa rai kwa Vyama Vikuu vya Ushirika kuhakikisha maghala ya vyama vya msingi yanaanza kupokea korosho za wakulima na ghala za minada ambazo tayari zimepata leseni kufungua ghala kwa ajili ya kuhifadhi korosho hizo, tayari kwa mauzo.

Alisema bodi itaendelea kushirikiana na wadau wote katika mnyororo wa zao la korosho kuhakikisha mkulima anazalisha na kuuza korosho zake kwa tija kwa maendeleo ya tasnia ya korosho nchin

Hata hivyo Bodi ya Korosho Tanzania imekasimiwa jukumu la kusimamia maendeleo ya zao la korosho katika ngazi zote za uzalishaji, ubanguaji/usindikaji, masoko na utafiti ili kuhakikisha kuwa zao la korosho linatoa mchango wake katika kuinua pato la mwananchi na Taifa kwa ujumla.
 
Halafu bei ya mazao huamuliwa na soko na uhitaji sioni sehemu ya kuilaumu serikali tena niisihi Serikali isiingilie biashara kama Magufuli kipindi kile alisababisha kuua kabisa soko la korosho na wakulima kudhulumiwa hadi leo, hivyo wauze kwa bei ya soko.
 
Mshtuko umewakuta wakulima baada ya Kuletewa bei ya Tsh 1680 kabla ya makato ambapo baada ya makato huenda mkulima ikamfikia 1380, Zoezi hilo la mauzo ya Korosho liliendeshwa wilayani Tandahimba katika kijiji cha Mitondi.

Wakulima wamegomea bei hiyo hivyo korosho hazijauzwa leo.
Wanapaswa kutumia busara tu, bei ya korosho haijawahi kuwa fixed, na haitokuwa fixed milele.

Wakikaa na hizo korosho halafu misimu ikakutana na ya nchi nyingine wategemee makali maumivu mnoo.

Consumption ya korosho inaweza kuwa imeathiriwa pakubwa na Corona hivyo walaji kuwa wachache. Petrol yenyewe ilipata kuathirika pakubwa sana mpaka kufikia 1500 licha ya uwepo wa tozo.
 
Back
Top Bottom