Wakulima wafunguka kuhusu bei ya korosho

Wakulima wafunguka kuhusu bei ya korosho

Papaa Muu

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
243
Reaction score
292
Wakulima wa zao la Korosho Mkoani Mtwara wamefurahishwa na maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta John Magufuli, kuwa serikali inabeba jukumu la kununua zao hilo kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo.

Gracee.jpg

Rais Magufuli​
Wakizungumza eatv Ibrahim Sabuli na Abdurlahman Ally ambao ni wakulima korosho baada ya kusikia kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa mapema leo katika zoezi la kuwaapisha Mawaziri na Naibu mawaziri, wakulima hao wamesema awali walikatishwa tamaa na mwenendo wa hali ya ununuz wa zao hilo.

Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kwa maamuzi aliyotufanyia wakulima wa korosho, tunamshukuru sana,” amesema Ibrahim Sabuli, ambaye ni mmoja ya wakulima hao.

Kwa upande wao, viongozi wa vyama vya msingi, Ally Mnyachi ambaye ni mjumbe wa bodi muungano AMCOS amesema kuwa,

Hatua hiyo itaongeza kasi ya wakulima kuwasilisha korosho katika maghala yao, tofauti na ilivyokua kabla ya tamko la Rais Magufuli.”
 
Attachments

  • safe_image.jpg
    safe_image.jpg
    15.4 KB · Views: 64
zanzibar24.co.tz
Maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kuwa serikali inabeba jukumu la kununua Korosho kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo imewafurahisha Wakulima wa zao hilo Mkoani Mtwara. Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya wafanyabiashara kuonekana wakiwalalia wakulima wa Zao hilo kwa kutaka kununua Korosho kwa bei isiyoridhisha ambapo awali waligomea uamuzi wa Rais Magufuli alipowataka wanunue kwa Tsh......
http://zanzibar24.co.tz/wakulima-waungana-kumpongeza-rais-…/
Kuna wana ukiwa lazima wapinge na hili pia...
 
Ni habari Chungu sana kwa Vibaraka wa mabwanyenye.
Kusini Kucheleeeeeeee...
 
Hiki ndo 98% ya watu wanatakiwa wakiamini kwamba alieleta tatizo ndo huyo huyo anaesifiwa kulitatua, baada ya kuwatoa kafara mawaziri, itachukua miongo mingi sana watu kujitambua
 
kiongozi wa chama cha msingi kanifurahisha sana, anafurahia wakati wakulima wanalipwa cash na madeni watakuja kulipa baadae

najiuliza kama mkulima alichukua pembejeo za m.1 ila mauzo yake ni laki 8 na amepewa cash je? atapeleka laki 8 zote ama atauchuna
 
Hiki ndo 98% ya watu wanatakiwa wakiamini kwamba alieleta tatizo ndo huyo huyo anaesifiwa kulitatua, baada ya kuwatoa kafara mawaziri, itachukua miongo mingi sana watu kujitambua
“A man who stands for nothing will fall for anything.” By Malcom X
 
Ujenzi wa viwanda huko huko inakolimwa ndio ukombozi wa uhakika. Kinachofanyika sasa ni hatua za muda tu.

Hii ndio fursa kwa wasomi wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wajipange kwa kutafuta vitendea kazi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Wadau wa maendeleo wa mikoa hii yenye kulima korosho, ipo haja ya kuandaa kitu kama kongamano la kubadilishana mawazo juu ya namna za kuweza kupata mtaji wa kujenga viwanda.

Haifurahishi kuona wadosi ambao ni watu wa kati wanatajirika halafu mkulima anaishia kufa na umaskini wake.
 
Mwaka kesho pia wanunue sio korosho tu, Bali pia na ubuyu jamani.
ubuyu WA vimto utaitoa Tanzania kimasomaso kiuchumi
 
Sifa ni kwa watanzania wote ambao ni walipa kodi wa nchi hii na siyo za mtu mmoja utafikri kanunulia kwa fedha zake za mfukoni.
 
Hiki ndo 98% ya watu wanatakiwa wakiamini kwamba alieleta tatizo ndo huyo huyo anaesifiwa kulitatua, baada ya kuwatoa kafara mawaziri, itachukua miongo mingi sana watu kujitambua
Yeye ndiye aliyeshusha bei soko la dunia?Unaweza kuja na uchanganuzi ukionesha kwanini wafanyabiashara waligoma bei ya 3000 na walikua sahihi?
 
kiongozi wa chama cha msingi kanifurahisha sana, anafurahia wakati wakulima wanalipwa cash na madeni watakuja kulipa baadae

najiuliza kama mkulima alichukua pembejeo za m.1 ila mauzo yake ni laki 8 na amepewa cash je? atapeleka laki 8 zote ama atauchuna
Deni halifungi
 
Hayo ni makubariano ya anayetoa mkopo na anayepokea, mnunuaji hayamhusu na hajui na Hana haja ya kujua muuzaji anadaiwa wapi na ni kiasi gani, kwani alipokuwa anakopa huyo pembejeo, mnunuaji alipewa taarifa ?? Iweje Leo yupo katika kununua umjie na habari zako hizo?? Mtadaiana huko mlikokopeshana
 
Yeye ndiye aliyeshusha bei soko la dunia?Unaweza kuja na uchanganuzi ukionesha kwanini wafanyabiashara waligoma bei ya 3000 na walikua sahihi?
Wewe kilaza pesa zilizokwapuliwa kwa sheria ndo ilibidi zi subsizide hio tofauti ya bei kama soko la dunia bei imeshuka tofauti inatolewa hapo
 
Wewe kilaza pesa zilizokwapuliwa kwa sheria ndo ilibidi zi subsizide hio tofauti ya bei kama soko la dunia bei imeshuka tofauti inatolewa hapo
We ndio kilaza na pimbi. Nimekuuliza bei iliyotajwa ya 3000 ni bei isiyowezekana?Nimeomba uje na ufafanuz kwanini iwe 2700 na serikali iongezee 300 na kwanini isiwe 3000 na kisiongezwe chochote?Kwamba wewe na genge lako ndio mnauelewa mpana wa bei ktk soko la dunia kuliko serikali?Acha kukarrshwa nyumb***** wewe.
 
Ujenzi wa viwanda huko huko inakolimwa ndio ukombozi wa uhakika. Kinachofanyika sasa ni hatua za muda tu.

Hii ndio fursa kwa wasomi wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wajipange kwa kutafuta vitendea kazi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Wadau wa maendeleo wa mikoa hii yenye kulima korosho, ipo haja ya kuandaa kitu kama kongamano la kubadilishana mawazo juu ya namna za kuweza kupata mtaji wa kujenga viwanda.

Haifurahishi kuona wadosi ambao ni watu wa kati wanatajirika halafu mkulima anaishia kufa na umaskini wake.

Phillipo hebu kaa kimya tu kaka yangu. Nakumbuka ule utapeli ulifanyika kwa kuwaaminisha watu kuhus fursa za uchumi wa gas. Watu walikwenda kwa fujo huko Mtwar na kuchukua maeneo kwa ajili ya uwekezaji uchumi wa gas ukishika kasi. Watu walienda kwa hamasa kubwa, lakini wamerudi kimya kimya na ukimuuliza mtu hata kuongea hataki. Sasa kama uchumi wa gas imekuwa hadithi, itakuwa mtu akajenge kiwanda kwa zao llinaloangalia hali ya hewa na wakati huohuo siasa haikawii kuingia kati? Nadhani jeshi ndio linafaa zaidi kujenga kiwanda huko. Anyway sipingi mawazo yako lakini umakini unatakiwa kwenye hilo.
 
Back
Top Bottom